Binadamu aliumbwa kwa udongo na atarudi kuwa udongo,maana yake mtu anapokufa, anazikwa.Mwili wake na mifupa yake yote hubadilika kuwa udongo ndiyo tafsiri yake
Maana yake haina haja ya kumzika na nguo au jeneza na mavitu ya ghalama, maana siku ya kufufuliwa kila mtu atafufuliwa uchi wa mnyama
Ukija upande wa kaburi, hairuhusiwi kujengewa wala kuandika majina ya marehemu, maan uzuri wa marehemu au ubaya wake unatokana na yale matendo aliyoyafanya akiwa hai duniani, siyo kujenga na kuremba kaburi tukitarajia labda tunamuhesimisha marehemu.
Na kama marehemu aliiacha kizazi chema mfano watoto waliosoma dini au Quruani basi watatumie elimu yao kumuombe mzazi wao,