Ni halali kujengea makaburi?

Ni halali kujengea makaburi?

Kwani mimi nimeandika chochote zaidi ya kupost picha? Wapi nimesema kuna tatizo? Kwanini unakuwa na negativity juu yangu? Mimi nilikuwa na reinforce tu point yako.
Mimi nimekueleza, silioni tatizo hapo. Au huelewi unachokisoma?
 
Naam, haujaacha kitu.

Penye hitilafu za maamuzi, kuna kitu kinaitwa "Qiyas" kwenye Uislam. Anaachiwa kadhi aamuwe, kama hakuna kadhi, wanaachiwa Maulamaa waamuwe.

Hakiharibiki kitu kwenye Uislam.

allah alisahau kuleta utaratibu wa kaburi la mja wake linatakiwa likengwe au lisijengwe?? Hao kadhi au maulamaa wanaleta qiyas zinazokinzana baina yao wenyewe na waumini pia.
 
Hili swali nalileta kwa waumini wa pande zote Waisilamu na wakristo,ili tulijadili kwa pamoja ni halali au hairusiwi kujengea makaburi?
Kuandika majina ya marehemu,tarehe walizozariwa na tarehe za siku waliyokufa?
Mtizamo wako ni upi juu ya hilo?
 
Kabuli ni moja ya kumbu kumbu za muhusika.
 
waulizw serikali kwanza viongozi wakubwa huwa wanajenga au wanaacha tu makaburi bila alama
Haitakiwi kuacha alama ya mtu akifa,maana kusema tu lile kaburi la fulani ni shiriki
Lakini huwa nasikia mnasema Uislamu haujaacha kitu.
kabla ya miaka 5 ya kufa mtume Muhamad (S.A.W)alikataza kabisa kuhusu kujengea makaburi ili watu wasije wakayaabudu na kugeuza sehemu za kutatulia shida zao

Lakini siyo kwamba mtu anakatazwa kwenda kuyatembelea makaburi,anaruhusiwa ila ambacho hakitakiwi ni kule kusema lile la shangazi lile la baba lile la fulani,hii ndiyo imekatazwa
 
allah alisahau kuleta utaratibu wa kaburi la mja wake linatakiwa likengwe au lisijengwe?? Hao kadhi au maulamaa wanaleta qiyas zinazokinzana baina yao wenyewe na waumini pia.
Hakuna kwenye Uisilamu kilichosauliwa,ila watu wanajisaulisha,ingekuwa kuna ruhusa basi tungeyaona makaburi ya mitume waliotangulia
 
Haitakiwi kuacha alama ya mtu akifa,maana kusema tu lile kaburi la fulani ni shiriki

kabla ya miaka 5 ya kufa mtume Muhamad (S.A.W)alikataza kabisa kuhusu kujengea makaburi ili watu wasije wakayaabudu na kugeuza sehemu za kutatulia shida zao

Lakini siyo kwamba mtu anakatazwa kwenda kuyatembelea makaburi,anaruhusiwa ila ambacho hakitakiwi ni kule kusema lile la shangazi lile la baba lile la fulani,hii ndiyo imekatazwa
Asiseme la shangazi aseme ni la mbwa sio?
 
Makaburi ya mitume na manabii wengi yamejengewa jee wasomi(Maulama) wamekosea?.
swali lako zuri sana...,
1. kwenye suala la kujengea makaburi watawala pia huusika na si wanawachuoni pekee.
2. hao wasomi hutofautiana katka kauli zao kulingana na mapokeo ya elimu (kuna waliopokea elimu kutoka kwa watu waliopotea kwenye haki).
 
Asiseme la shangazi aseme ni la mbwa sio?
Yaani kusema tu lile la fulani ni dhambi,sababu yule mtu ategeuka na kuwa mafuvumbi,sasa kuna uhalali gani hapo wa kujua aliyelala ni furani,lakini ni haki kuwasalimia kwa ujumla watu wòte wa makaburini,mu hali gani sisi wote huku ni wazima na si mda mrefu tutaungana nanyi pamoja makuburini
 
Kwahiyo hilo kaburi lina tofauti gani na la mbwa sasa.., hao walikuwa binadamu na kuna memory zipo vichwani mwa watu.., lazima wawe adressed accordingly
 
Naamini inategemea la lengo na dhamira ya Mtu, Hata Yesu alizikwa kwenye well structured Kaburi
 
Binadamu aliumbwa kwa udongo na atarudi kuwa udongo,maana yake mtu anapokufa, anazikwa.Mwili wake na mifupa yake yote hubadilika kuwa udongo ndiyo tafsiri yake

Maana yake haina haja ya kumzika na nguo au jeneza na mavitu ya ghalama, maana siku ya kufufuliwa kila mtu atafufuliwa uchi wa mnyama

Ukija upande wa kaburi, hairuhusiwi kujengewa wala kuandika majina ya marehemu, maan uzuri wa marehemu au ubaya wake unatokana na yale matendo aliyoyafanya akiwa hai duniani, siyo kujenga na kuremba kaburi tukitarajia labda tunamuhesimisha marehemu.

Na kama marehemu aliiacha kizazi chema mfano watoto waliosoma dini au Quruani basi watatumie elimu yao kumuombe mzazi wao,
Niliwahi kutakiwa na idara fulani kuonyesha kaburi la babu yangu.
Kilichoniokoa ni waliojengea makaburi na kuyaandika majina.

Kwa usalama wa kizazi chako nakusihi ujengee na uweke jina la marehemu.
 
Marehemu Babu yangu alikuwa anakataza kujengea makaburi. Baada ya kumhoji alituambia mafundisho ya dini yalitaka iwe hivyo ili ardhi iweze kutumika kwa shughuli nyingine pale kaburi lako linapokuwa limepotea. Ilikuwa ngumu kumeza ila nilielewa mantiki ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom