Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Attaboy

New Member
Joined
Jul 26, 2024
Posts
1
Reaction score
9
Mimi ni kijana bado natafuta kwa ajili ya familia yangu hivi karibuni nilihamishwa kazi na kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu nyumbani akiwa mjamzito.

Kutokana na ukata wa maisha ili tubidi kuuza baadhi ya vitu ambavyo ilikuwa gharama kuhamisha na nikampeleka mke wangu nyumbani kwetu wakati akisubiri kujifungua

Kabla na baada ya mke kujifungua huwa natuma pesa za matumizi madogo madogo ya nyumbani kupitia namba ya simu ya mama yangu jambo ambalo linamkera sana mke wangu licha ya kwamba na yeye huwa namtumia pesa za vocha na vitu vidogo vidogo

Mke wangu hataki kukaa nyumbani anatishia kurudi kwao na mimi bado sijarudi kwenye mstari bado sijawa na maisha ya kumleta mke wangu huku nilipo

Naombeni ushauri wenu wana jujwaa
 
Umekosea kumpeleka mke kwa wazazi wako. Wanawake wawili hawawezi kuishi pamoja hata kama ni mtu na mama yake.

Kosa lingine ni kumtumia mama yako hela ili anunue mahitaji ya mke wako. Huko ni kumuonyesha dharau mke wako.

La mwisho ila siyo kwa umuhimu, Vijana wenzangu kama bado unajiona uchumi wako haujaeleweka usioe.
 
Ukisikia lugha gongana ndio hapo ,kila mmoja anaweza kukupa jibu kulingana na mtazamo wake kama unampatia mkeo fedha za mahitaji madogo madogo ili aweze tatua mahitaji yake madogo madogo hapo ukweni sioni baya kama utampatia mama yako fedha maana yeye ndiye malikia katika mji huo na ukimpa mkeo ni kama umezarau mamlaka ya mama yako katika himaya yake.
 
Unatakiwa kumtumia Pesa mkeo siyo Mama yako!
Kwanini wakat navofahamu mwenye nyumba ndie anajua matumizi ya nyumbani
Uhalisia Hela za matumiz za jumla ziende Kwa mama ila mkewe awe anamtumia za kwake Kwa emergency siku kashikwa na uchungu sukari hakuna ataweza kununua na Yuko leba
Mkew aache uchoyo na sikuzote mtu ukiwa mchoyo mchoyo huwez ishi na watu
Lakin pia huenda ana vikoba au Michezo Kwa Siri hivo Kodi ya meza ndio suluhisho lake kutokumpa unamtesa
 
Kwanini wakat navofahamu mwenye nyumba ndie anajua matumizi ya nyumbani
Uhalisia Hela za matumiz za jumla ziende Kwa mama ila mkewe awe anamtumia za kwake Kwa emergency siku kashikwa na uchungu sukari hakuna ataweza kununua na Yuko leba
Mkew aache uchoyo na sikuzote mtu ukiwa mchoyo mchoyo huwez ishi na watu
Lakin pia huenda ana vikoba au Michezo Kwa Siri hivo Kodi ya meza ndio suluhisho lake kutokumpa unamtesa
Mkuu huo ni uchanga katika ndoa! Fahamu katika ndoa Mme na Mke wanamilki cho chote pamoja hata kama Mme ndiye anatafuta.
Mama au Baba hawana sehemu kabisa katika mali au fedha ya Mme na Mke!
Wazazi wanapewa msaada tu.
Kwa hiyo hapo Mme anatakiwa kumtumia fedha mkewe kwa ajili ya matumizi yake binafsi anapokuwa mjamzito siyo Mama.
Pili katika ndoa,Mme na Mke lazima waaaminiane siyo kuchungana au kutuhumiana.
Bila kuzingatia hayo ndoa kama kama hizo huwa hazidumu.
 
So wife akitamani chipsi mpaka amuombe mama mkwe? Mimi mara nyingi huwa nawatumia wote. Ila nawawaweka wazi matumizi. Mfano laki moja hiyo ni manunuzi ya mahitaji muhimu kama chakula Sabuni n.k. hiyo elfu hamsini ni ya Mambo yako binafsi.
Nilimtumia wife namuambia kabisa hiyo yako hiyo ya mahitaji ya nyumbani. Jitahisi kuwa muwazi unapotuma pesa
 
Back
Top Bottom