Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Mama ndio atumiwe na sio mke.

Haiwezekani huko aliko eti mama yako amkodolee jicho mkeo pesa ya matumizi.

Mama ndio ataratibu mambo yote na mke utamtumia pesa ambayo ni ya matumizi binafsi na sio yale ya nyumbani kila siku.

Mke lazima umtumie kiwango kadhaa kwa sababu naye atataka siku moja moja kujisikia kula kitu fulani ama kununua kitu fulani so haimake sense akaombe kwa mama
 
Wanawake wengi hawapendi kukaa na mama mkwe kwasababu wanakosa freedom.
Suala la kutuma pesa mimi ninafikiri anayepaswa kutumiwa pesa ya matumizi ni yule anayehusika kununua mahitaji ya nyumbani kama vyakula,sabuni n.k
Freedom ya aina gani? Unaweza kutoa mifano?
 
Mkuu huo ni uchanga katika ndoa! Fahamu katika ndoa Mme na Mke wanamilki cho chote pamoja hata kama Mme ndiye anatafuta.
Mama au Baba hawana sehemu kabisa katika mali au fedha ya Mme na Mke!
Wazazi wanapewa msaada tu.
Kwa hiyo hapo Mme anatakiwa kumtumia fedha mkewe kwa ajili ya matumizi yake binafsi anapokuwa mjamzito siyo Mama.
Pili katika ndoa,Mme na Mke lazima waaaminiane siyo kuchungana au kutuhumiana.
Bila kuzingatia hayo ndoa kama kama hizo huwa hazidumu.
Hapo hayupo kwenye mjiwake
Sijasema asitumiwe ila atumiwe za matumiz yake binafsi diapers,vocha na mambo mengine sio chakula mama amuulize mkwewe na ni mgeni
Kuna vitu vinahitaji uungwana tu wazaziwako ni Mungu wako wa pili ndio wamekuzaa na kukulea vitu vidogo kma hivo sio vya kutolea macho
 
Nyege zimeisha!! Akili imerudi sasa.
Eti uku niliko cjajipanga BIG NO chukua mkeo ivyo ivyo ndio muhimu kwenu kama mme na mke!!

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Hapo hayupo kwenye mjiwake
Sijasema asitumiwe ila atumiwe za matumiz yake binafsi diapers,vocha na mambo mengine sio chakula mama amuulize mkwewe na ni mgeni
Kuna vitu vinahitaji uungwana tu wazaziwako ni Mungu wako wa pili ndio wamekuzaa na kukulea vitu vidogo kma hivo sio vya kutolea macho
Mkuu hata mimi sijasema tusiwapende Wazazi wetu! Lazima tuwaheshimu na kuwasaidia kadri tunavyoweza! Bado ni wajibu wetu kufanya hivyo!
Lakini fahamu mbele za Mungu ukishaoa wewe na mke ni Mwili mmoja! Mnaachana na wazazi,(Mwanzo2:21-24)
Cho chote unachofanya,unachopanga lazima umshirikishe Mkeo bila kimficha hasa hasa fedha.
Mali au fedha unayotafuta ni ya kwako na Mkeo SIYO YA WAZAZI.
 
Mkeo mchoyo mchoyo
Wanawake wawili hawawezi kuishi pamoja
Hilo suala la kumtumia mama yake hela ndiyo afanye matumizi ya hapo nyumbani. Hayupo mwanamke atakayekubali hata huyo mama angekuwa anafanyiwa na baba yake na jamaa asingekubali.
 
Kwa ushauri wangu kama mtu mzima ni hivi, Mtumie mke wako kama mama ndiye ananunua mahitaji yeye ndio ampe .

Kimsingi kwa sasa mke wako ndio mtendaji mkuu kwenye hiyo familia.
Jambo la mwisho fanya Juu chini hata kama hauko vizuri uishi na mke wako Mama wakwe hawawezi kukaa na wakwe zao kwa zaidi ya wiki moja.

Pole sana Mungu akusaidie Ufanikishe mipango yako
 
Mkuu hata mimi sijasema tusiwapende Wazazi wetu! Lazima tuwaheshimu na kuwasaidia kadri tunavyoweza! Bado ni wajibu wetu kufanya hivyo!
Lakini fahamu mbele za Mungu ukishaoa wewe na mke ni Mwili mmoja! Mnaachana na wazazi,(Mwanzo2:21-24)
Cho chote unachofanya,unachopanga lazima umshirikishe Mkeo bila kimficha hasa hasa fedha.
Mali au fedha unayotafuta ni ya kwako na Mkeo SIYO YA WAZAZI.
Kumshirikisha Iko sawa,
Lakini sio ishu kubwa kiasi mke alalamike kutokupewa yeye yaani Kwa Mimi sijaona tatizo labda sababu watu hatufanani
Kama vitabu vimesema hivo mimba alipeleka kwao ya Nini asingekaa na mkewe akamlea mwenyewe
 
So wife akitamani chipsi mpaka amuombe mama mkwe? Mimi mara nyingi huwa nawatumia wote. Ila nawawaweka wazi matumizi. Mfano laki moja hiyo ni manunuzi ya mahitaji muhimu kama chakula Sabuni n.k. hiyo elfu hamsini ni ya Mambo yako binafsi.
Nilimtumia wife namuambia kabisa hiyo yako hiyo ya mahitaji ya nyumbani. Jitahisi kuwa muwazi unapotuma pesa
Wewe ndo umeongea s la maana watumiwe wote Kwa chakula ielewek ni ya chakula na anaehusika ni mama mwenye nyumba yeye ndo anajua tembele linapatikana wapi
Ya mke atumiwe akitak kuku atajiongeza ila kuwepo na uwazi
 
Tumia akili. Mama ni mama na mama ndio mwenye nyumba hapo kwenu na mahitaji yote ni juu yake sio mkeo. Hivyo ni sahihi kumtumia pesa mama yako. Huyo mkeo kama ana shida nyingine binafsi zaidi ya huduma za hapo kwenu then itakuwa sawa kumtumia pesa yeye kama yeye.
 
Mtumie mkeo mama mpe tu hela kidogo ya mahitaji yake.

Mwelezee mama yako sasa asijisimbue sana mahitaji yote atafanya mkwe wake.

All in all ni kashesh
Duh!! Kumbe unawazaga hivo? Pole yako.
Kwanza mwanamke hana adabu. Alitakiwa atambue yupo kwa nani. Wewe inakuingia akilini,mtu aje kwako,na aanze kukupangia namna ya kuishi. Alichofanya kuwatumia wote ni sahihi.
Mjamzito yeye anaweza nini? Na hili ni wazi ni jukumu la mama mkwe kumhudumia. Kama yeye anaona si sahihi,kuna kutojishusha na kutambua kuwa akiwa kwa watu,hawezi kuishi kama yupo kwake. Mwanaume kasema hayupo vizuri. Jamani,kaficha nini hapa? Ina maana mwanamke hataki kuishi kwa mama mkwe.
 
Kabla na baada ya mke kujifungua huwa natuma pesa za matumizi madogo madogo ya nyumbani kupitia namba ya simu ya mama yangu jambo ambalo linamkera sana mke wangu licha ya kwamba na yeye huwa namtumia pesa za vocha na vitu vidogo vidogo.

Komaa na huu utaratibu. Kwenu,mwenye majukumu ni wewe na mkeo. Kwa mama yenu,mwenye majukumu ni wewe na mkeo. Na mama yako,akikususia,utalia. Na ni wazi,huyo mwanamke hataki kuishi kwenu,analazimisha tu. Unadhani atajifungulia hapo? Ndo hapo familia inaanza kuvurugika sasa. We mwache aende anakotaka,ila jiulize. Itaacha picha gani kwa mama yako? Japo huenda nae kuna vitu hasemi,ila pamoja na hayo,atakuwa ameshamuona,huenda nae anaomba umpe uhuru. Lakini,kosa kubwa sana kwamba yeye ndo aamue ukweni wanakula nini,wanakunywa nini. Kama hawezi vumilia,muache aende anakotaka. Japo hata kwao,utaratibu unatakiwa uwe huo huo,kuna chochote umepata,watumie wazazi wake wamlee.

Mwanamke mwenye malezi na maadili,hawezi kulilia kupewa matumizi yeye,huku anajua hayupo kwake. Overr
 
Tumia akili. Mama ni mama na mama ndio mwenye nyumba hapo kwenu na mahitaji yote ni juu yake sio mkeo. Hivyo ni sahihi kumtumia pesa mama yako. Huyo mkeo kama ana shida nyingine binafsi zaidi ya huduma za hapo kwenu then itakuwa sawa kumtumia pesa yeye kama yeye.
Anatumiwa kiasi kwa matumizi yake,sana sana labda kama akiba itakayolipwa hospitalini. Lakini kwamba anachotumiwa hakitoshi,hapo hamna mke. Anatakiwa awe chini ya uangalizi wa wazazi.
 
Tatizo mkeo ni mchoyo mchoyo, angekua ni mtu poa hata pesa yote unamtumia yeye tu hata kama yupo kwenu.

Sisi kwetu kukiwa na scenario ya namna hiyo pesa yako huwa haihitajiki, mpaka umempeleka kwa maza basi una uhakika maza hawezi shindwa kumtunza huyo binti, hata pesa unaweza kukatazwa kutuma hovyo as if mkeo atashindwa kupata atakacho, labda pesa yako uitunze ije kusaidia itakapotokea dharula au wakati wa kumleleka hospitali.

Ila hiyo familia yako ambayo wanagombania hicho unachopeleka ni tatizo.
Kwa hapo mama aendelee kupokea hizo pesa kama unavyofanya, huyo mkeo anaweza shikwa na uchungu na asitoe hata sent tano mbovu akiamini maza ana pesa, mpe mama pesa.
 
Umekosea kumpelaeka mke kwa wazazi wako. Wanawake wawili hawawezi kuishi pamoja.

Kosa lingine ni kumtumia mama yako hela ili anunue mahitaji ya mke wako. Hiyo ni kumuinyesha dharau mke wako.

La mwisho ila siyo kwa umuhimu, Vijana wenzangu kama bado unajiona uchumi wako haujaeleweka usioe.
Dah La mwisho Ila siyo kwa umuhimu
Vijana wenzangu Kama bado unajiona uchumi wako haujaeleweka usioe.
May God bless you Restless Hustler huo mstari wa mwisho ni mstari ambao kwenye vikao vya wanaume umewekwa mbele kwenye kurasa ya DIBAJI Ila wanatokea wasaliti wachache wanatusaliti yakiwakuta wanakuja kulia na kuomba ushauri ilihali walianza wao usaliti .

Jamani vijana NDOA NI HELA SIO NGONO .

na wewe mleta mada acha Mara moja kutuma hela ya matumizi kwa mama yako mtumie mkeo alafu mama yako mtumie hela ya Mara moja moja ,kuendelea kumpa mama yako hela ya matumizi ni sawa na kuwa wewe haujaoa ,acha hizo
 
Nyie na wake zenu ndio mnazidi kufanya ndoa zionekane ngumu sana..
We mpe za mahutaji yake za chakula mpe mama. Kaka angu alikua anampa ela mkewe hatoi na anaamka anasubiri mama amlishe washenzi wale wamenifanya nihisi namna mama mkwe anavojiskia ... sitaweza kumfanya mama wa watu hivyo wallah! Akinipa ela ya mahitaji yangu ya chakula ampe mama ake jamani wamama wanajiskia vibaya hawasemagi tu
 
Siku ukioa utaelewa. Kwa sasa wakuache kama unavofikilia,pia ni haki.
 
Nyie na wake zenu ndio mnazidi kufanya ndoa zionekane ngumu sana..
We mpe za mahutaji yake za chakula mpe mama. Kaka angu alikua anampa ela mkewe hatoi na anaamka anasubiri mama amlishe washenzi wale wamenifanya nihisi namna mama mkwe anavojiskia ... sitaweza kumfanya mama wa watu hivyo wallah! Akinipa ela ya mahitaji yangu ya chakula ampe mama ake jamani wamama wanajiskia vibaya hawasemagi tu
We kuwa muazi humuogopi mtu. Mama amepokea mzigo si mkwe wala mjamzito.
Mwanamke anaejitambua,hata kwa kile kidogo unachompa,atamkatia mama mkwe kuweka mazingira sawa. Mama mkwe ni mzazi,si mfanyakazi wa mkeo.
Je,huyu isingelikuwa kupinda kwa mwanaume,hata kusalimia haendi.
 
Back
Top Bottom