Ni halali kutuma pesa za matumizi kwa mama wakati mke wangu yupo kwake?

Siku ukioa utaelewa. Kwa sasa wakuache kama unavofikilia,pia ni haki.
Ndugu yangu nioe Mara ngapi mkuu ? Nilioa nikaachika na soon nitamuoa tena Nyamwi255 Ila nasisitiza kuwa hakuna pesa hakuna ndoa NI kujongea kwenye mkondo wa ngono .

Sio kuwa ukioa basi itaanza kushushiwa hela ya matumizi lazima ndoa iyumbe na inyambulike ,hivyo vijana NDOA bila hela ni ugomvi wa nafsi Kaka
 
Umekosea kumpelaeka mke kwa wazazi wako. Wanawake wawili hawawezi kuishi pamoja.

Kosa lingine ni kumtumia mama yako hela ili anunue mahitaji ya mke wako. Hiyo ni kumuinyesha dharau mke wako.

La mwisho ila siyo kwa umuhimu, Vijana wenzangu kama bado unajiona uchumi wako haujaeleweka usioe.
Uchumi wa Afrika hautabiriki unaweza kulala tajiri na kuamka masikini
 
Mkuu huo ni uchanga katika ndoa! Fahamu katika ndoa Mme na Mke wanamilki cho chote pamoja hata kama Mme ndiye anatafuta.
Mama au Baba hawana sehemu kabisa katika mali au fedha ya Mme na Mke!
Wazazi wanapewa msaada tu.
Kwa hiyo hapo Mme anatakiwa kumtumia fedha mkewe kwa ajili ya matumizi yake binafsi anapokuwa mjamzito siyo Mama.
Pili katika ndoa,Mme na Mke lazima waaaminiane siyo kuchungana au kutuhumiana.
Bila kuzingatia hayo ndoa kama kama hizo huwa hazidumu.
Unalolisema ni kweli wawapo kwao. Sasa,leo hawapo kwao,na walipo,ni kama wamehifadhiwa. Watajipangiaje maisha ya kila siku na hawapo kwao?
 
Ndugu yangu nioe Mara ngapi mkuu ? Nilioa nikaachika na soon nitamuoa tena Nyamwi255 Ila nasisitiza kuwa hakuna pesa hakuna ndoa NI kujongea kwenye mkondo wa ngono .

Sio kuwa ukioa basi itaanza kushushiwa hela ya matumizi lazima ndoa iyumbe na inyambulike ,hivyo vijana NDOA bila hela ni ugomvi wa nafsi Kaka
Nakupata mkuu,ila na mi nakuomba kitu kimoja. Usijumlishe,twende kwenye mada husika hapa. Jama kapata kikazi mbali,na akaona kuacha familia nyuma ni ngumu. Pengine mpaka akauze vitu,ni apate hata kodi na kusafilisha vitu vya kuanzia. Na mke kamuacha mwa mda,pengine anataka akimleta awe yupo vizuri(kwa plans zake). Sasa,inaonekana mwanamke halidhiki na kile anachopewa. Huwezi mleta mtu kwangu na aanze kunipangia maisha. Haiwezekani. Kwa uswahili wetu,lazima mwenye mji ajione ana mamlaka fulani. Kwa mila zetu,lazima mwanamke atambue yupo ugenini. Mama anatumiwa zaidi ya mara moja,kwa sababu yeye ndo amempokea mgeni,hakika na kwake si mama mambo shwari,anaungwa mkono. Kwa anayejiweza,hata hiyo pesa isingekuwa inatumwa. Unless kutokuwa vizuri kwa jamaa ndo kuwe tatizo.
 
Hapo ni kweli Kaka Kuna namna nahisi mwanamke anakosea pia maana Sasa nimekuelewa wewe yawezekana sikumpata vyema mleta mada ,Ila kwa hapo sioni Kama kumpa hela mwanamke na ilihali alishamzoesha mama yake kutuma hela ya matumizi Kama italeta afya Ila kwa hapo inabidi jamaa atumie hekima sana kumueleza mkewe aelewe vyema .
 
Ndugu yangu nioe Mara ngapi mkuu ? Nilioa nikaachika na soon nitamuoa tena Nyamwi255 Ila nasisitiza kuwa hakuna pesa hakuna ndoa NI kujongea kwenye mkondo wa ngono .

Sio kuwa ukioa basi itaanza kushushiwa hela ya matumizi lazima ndoa iyumbe na inyambulike ,hivyo vijana NDOA bila hela ni ugomvi wa nafsi Kaka
Upo serious utanioa ...nambie nianze kufanya vioja niachike🥰🥰😅
 
1.Huna uchumi wa kuwa mume ulimharibia maisha binti
2.Huna ukomavu wa kutosha kuwa mume,bado hujui nafasi ya mama na mke ,hela ya mume hushikwa na mke sio mama yako.kimsingi mama alipaswa kuna namna amuone mkwewe sio mzigo kwa kuona anatoa matumizi
3.Muache binti aende kwao ,mja mzito anaamri nyingi anazopaswa kumpa mlezi wake hawezi kuwa huru kumtuma tuma mkwewe ,umefanya usenge sana ku** ww kumpeleka kwa mama yako ,mzazi unamrudisha kwa mama yake kisha unamtumia matumizi yeye ,kule atakuwa huru maana ni kwao ,pata picha ww ukiambiwa ukakae mwezi kwa wakwe zako utajisikiaje ukitaka uchemshiwe maji ya moto utamtuma mkwe???
 
Ungempeleka kwao maana hata kama kuna njaa huko anajua kwao
Ila umebugi sana kumpeleka kwenu
Ila kama bado unajiandaa itabidi umruhusu aende kwao
Huko utakuwa na piece of mind
Utamtumia yeye na huku ukimtumia mama yako
Mama ni Mama tu na ana nafasi kubwa
Usiwachonganishe
 
Mimi ni kijana bado natafuta kwa ajili ya familia yangu hivi karibuni nilihamishwa kazi na kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu nyumbani akiwa mjamzito.

Kutokana na ukata wa maisha ili tubidi kuuza baadhi ya vitu ambavyo ilikuwa gharama kuhamisha na nikampeleka mke wangu nyumbani kwetu wakati akisubiri kujifungua

Kabla na baada ya mke kujifungua huwa natuma pesa za matumizi madogo madogo ya nyumbani kupitia namba ya simu ya mama yangu jambo ambalo linamkera sana mke wangu licha ya kwamba na yeye huwa namtumia pesa za vocha na vitu vidogo vidogo

Mke wangu hataki kukaa nyumbani anatishia kurudi kwao na mimi bado sijarudi kwenye mstari bado sijawa na maisha ya kumleta mke wangu huku nilipo

Naombeni ushauri wenu wana jujwaa

Mwambie Mkeo Afanye kile anachoona yeye NI Sahihi.

Yeye NI mtu mzima
 
Mke wako hana busara na ni mchoyo hapo anaona mama anafaidi sana, hapo sio kwake ni kwa mama yako....
For as long as mama yako ana nguvu na ndiye anafanya manunuzi ya hapo nyumbani mtumie mama na mke endelea kumtumia za matumizi binafsi.

Usitishike kirahisi, akilalamika we msikilize usitie neno, akisema anaenda kwao mwambie nenda ila nenda kwa nauli yako na utajitunza mwenyewe ukifika huko.

Ifike hatua wanaume mjue nafasi zenu, ukiwa mnyonge kwa vitu vya kijinga utanyanyasika tu. Huyo mke hana hoja, unless hali vizuri na hapewi huduma za msingi za uzazi ambazo unaweza tafuta binti wa kazi amsaidie
 
Mtumie mkeo mama mpe tu hela kidogo ya mahitaji yake.

Mwelezee mama yako sasa asijisimbue sana mahitaji yote atafanya mkwe wake.

All in all ni kasheshe
Huu sio utaratibu, huo sio mji wake,
Mimi kama mama wa vijana wa kiume wa kutosha ukija kwangu utafata sheria zangu, utanipangia nikija kwenye mji wako
 
1.Huna uchumi wa kuwa mume ulimharibia maisha binti
2.Huna ukomavu wa kutosha kuwa mume,bado hujui nafasi ya mama na mke ,hela ya mume hushikwa na mke sio mama yako.kimsingi mama alipaswa kuna namna amuone mkwewe sio mzigo kwa kuona anatoa matumizi
3.Muache binti aende kwao ,mja mzito anaamri nyingi anazopaswa kumpa mlezi wake hawezi kuwa huru kumtuma tuma mkwewe ,umefanya usenge sana ku** ww kumpeleka kwa mama yako ,mzazi unamrudisha kwa mama yake kisha unamtumia matumizi yeye ,kule atakuwa huru maana ni kwao ,pata picha ww ukiambiwa ukakae mwezi kwa wakwe zako utajisikiaje ukitaka uchemshiwe maji ya moto utamtuma mkwe???
Muwe mnaacha ujuaji na maneno makali ya kijinga, mpaka anampeleka ukweni walikubaliana haikuwa lazima, kufika huko ndo anabadilisha gia angani kwa sababu za kijinga.
Angekua na shida toka mwanzo angeenda kwao
 
Back
Top Bottom