Ni halali mzazi kumwachisha mtoto shule ili akamhudumie?

Ni halali mzazi kumwachisha mtoto shule ili akamhudumie?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kipindi fulani, nilifuatwa na kijana mmoja aliyekuwa akiishi jirani na nilikokuwa nikifanyia kazi, na kuniomba nimsadie kumtafutia nafasi ya kujifunza masuala ya ufundi kwenye kampuni fulani. Alikuwa bado kijana mdogo, under 18. Aliamua kutafuta hiyo nafasi baada ya kufeli mitihani ya kidato cha pili.

Kwa sababu ya umri wake mdogo, nilimwambia aje na mzazi wake.

Alifanya hivyo. Alikuja na mama yake. Babaye hakuwepo muda huo. Alikuwa akiishi kwingineko.

Baada ya mama yake kukiri kuwa anakubali mwanaye aende kwenye hayo mafunzo, nilionana na meneja wa kampuni husika ( nilikuwa nafahamiana naye) kwa ajili hiyo, na kwa bahati nzuri, akaliridhia ombi husika.

Lakini wakati kijana akijiandaa kwenda kuanza mafunzo, nilipata taarifa kuwa baba yake karejea kutoka alikokuwa. Kwa sababu nilikuwa ninafahamiana naye, nilimpigia simu tuonane. Nilifanya hivyo baada ya kujulishwa kuwa aliporejea kutoka alikokuwa, alianzisha "vurugu" nyumbani kwake kwa kumpiga mkewe n.k. Nilitaka nijue kama ana taarifa kuwa mtoto wake anataka akajifunze masuala ya ufundi.

Nilichobaini ni kuwa hakuwa amependezwa na hilo. Alidai kuwa mkewe na kijana wake hawakuwa wamemshirikisha, hivyo na mimi nikaamua kusitisha huo mchakato.

Lakini nilishangazwa na moja ya hoja zake. Alikuwa akijisifia kuwa yeye aliacha shule akiwa Sekondari, nafikiri "form two", baada ya baba yake kumtaka asitishe masomo akamsaidie kwa sababu alikuwa mgonjwa. Baba yake alienda mpaka shuleni kwao alikokuwa akisoma (shule ya "boarding") na kumwomba mkuu wa shule amruhusu kijana wake kuacha masomo ili akamsaidie shughuli za nyumbani kwa sababu yeye alikuwa mgonjwa na hakuwa na mtu mwingine wa kumsaidia. Japo mkuu wa shule aligoma mwanzoni, lakini kwa kuwa babaye alionesha ung'ang'anizi, mkuu wa shule aliishia kumkubalia.

Kwa mujibu wa masimulizi yake, kabla baba yake hajaaga dunia, alimshukuru na hivyo kumbariki kwa kukubali kwake kuacha masomo ili akamsaidie.

Alinisimulia hayo kunionesha kuwa kwa vile yeye alimtii baba yake, inampasa mwanaye naye kumtii pia. Jambo ambalo alilifanikisha.

Mtoto wake hakuweza kuipata tena hiyo nafasi baada ya kulazimika kusitisha huo mchakato.

Miezi michache baadaye, alinipigia tena simu kuniomba nimtafutie tena huyo mtoto wake kazi. Sikufanikiwa kufanya hivyo japo nilitamani ningeweza kuwasaidia.

Kwangu mimi, sikubaliani na huo mtazamo wa mtoto kuachishwa masomo ili akamsaidie mzazi wake . Hata huko "kwetu" haukubaliki pia.

Vipi huko "kwenu?"
 
Mkuu kuna watu walishafunga ndoa na umaskini ni ngumu kuwatenganisha. Nilitaka niandike uzi kama huu wako ila tofauti yake ni binti aliachishwa kazi ili akamhudumie babu yake mgonjwa kana kwamba ukoo mzima yeye tu ndo anaweza hiyo kazi. Baada ya miezi kadhaa ndo binti anatuma msg ya kutaka tena kazi eti kwa sasa anapatikana. Kuna mwingine aliomba kazi akaulizwa kwanini aliacha kazi aliyokuwa anafanya awali akajibu alienda kuhudumia mgonjwa. Wenye kampuni wakaona atasumbua tena hata akipewa kazi. Maskini wengi ni wajinga na wapumbavu waliokubuhu.
 
Mkuu kuna watu walishafunga ndoa na umaskini ni ngumu kuwatenganisha. Nilitaka niandike uzi kama huu wako ila tofauti yake ni binti aliachishwa kazi ili akamhudumie babu yake mgonjwa kana kwamba ukoo mzima yeye tu ndo anaweza hiyo kazi. Baada ya miezi kadhaa ndo binti anatuma msg ya kutaka tena kazi eti kwa sasa anapatikana. Kuna mwingine aliomba kazi akaulizwa kwanini aliacha kazi aliyokuwa anafanya awali akajibu alienda kuhudumia mgonjwa. Wenye kampuni wakaona atasumbua tena hata akipewa kazi. Maskini wengi ni wajinga na wapumbavu waliokubuhu.
Inasikitisha kwa kweli!

Waafrika wanahitaji ukombozi wa fikra!
 
Tunaweza kudhani tunajua au kufahamu kila kitu lakini wakati mwingine huwa nafikiri kuna vitu viliisha pangwa vitakuwa hivyo hata usipolazimisha au kulazimisha, vitakuwa hivyo hivyo.

Kuna watu wamesoma sana na wanauwezo mkubwa wa akili/ufahamu wa masomo, kwenye maisha ya kwaida wana mafanikio hafifu kuliko hata wale amabao hawajasoma au wenye uwezo hafifu kwenye masomo.

Binafsi, kuna vitu niliisha amua kuviacha na kuacha mambo yafuate mkondo wake. Niliwahi kumlazimisha mtu kwenda shule na kumsaidia ada, na akamaliza chuo. Hatafuti kazi yupo yupo tu, ukimuuliza anakwambia sijapata. Unaangalia ni mtu mzima sasa kaoa na anawatoto, shughuli zake tofauti na alichosomea, licha ya kwamaba zinamuingizia kipato na anaendesha maisha, lakini huwa nadhani angefanya kazi ya elimu yake angekuwa kwenye level nyingine, lakini yeye haamini hivyo.

Hivyo nadhani, ukimuona tajiri jua kaufanyia kazi utajiri wake huo, na kama alirithi basi ndivyo ilivyopangwa iwe.

Na kuna watu ni ma fighter sana lakini hawafanikiwi kwa kiasi kile cha nguvu waziwekazo, na kuna watu wanaishi kimasihara lakini maisha yao yana kwenda utadhani wana ishi heaven, unaona mtu anaishi kwa kupiga deals za ajabu ajabu, lakini ana jumba zuri, gari zuri, mke na famili na maisha yake yako stable, hadi unashangaa. Jaribu wewe kuishi anavyoishi , umalizi hata wiki huna pesa.

Maisha haya ni fumbo, kuna vitu hatuvifahamu, na kuna watu wana bahati, na kuna watu inabidi tutumie nguvu, akili na muda mwingi kutafuta kidogo tukipatacho.

Ishi maisha yako, yao waachie wenyewe.
 
Back
Top Bottom