Ni hatari sana kulala na mtungi wa gesi ndani.

Zenji hapa mkuu
Sasa mbona unakuwa kama ndumila kuwili namana ww huijui bongo? Bongo siyo ya kufananisha na bukoba na unaposikia daslamu usifikr utakuta majumba kama dubai, unaposikia daslamu ujue n jiji na watu wake wakulungwa wa jiji!
 
Ges ya mama ,post
 
Sasa Mtungi WA gas Tu mmestuka hivyo,Vile Mkisema mnakinukisha na hamtaki Amani,itakuwaje?
 
Mtu amepanga chumba kimoja uswahilini halafu ajengee mtungi nje na hakuna hata uzio!!

Sasa hivi mita za maji zinaibwa,ile earthrod ya copper wanachimba wanabeba hlf muwaongezee na mitungi.

NB:Sijawahj kushawishika kabisa na matumizi ya gesi kwangu bora gharama za umeme tu.
 
Gas nyingi hasa mitungi mikubwa ina sehem yq kufunga na kufungua.

Hakikisha baada ya matumizi unafunga kwenye kichwa cha mtungi.

Hakikisha ile PIPE ni ngumu na sio zile za bei rahisi.

Hakikisha connection ya mtungi ipo tight pia na pale kwenye Jiko pako tight..

Epuka kujikunja kwa Pipe, kuhamisha hamisha mtungi bila sababu za msingi.. weka sehem moja fanya fittings tulia.

Kabla ya kuwasha hakikisha hakuna harufu yoyote ya gesi.. ( ki kawaida gesi ya kupikia haina HARUFU, ila wataalam waliweka substance ya kuifanya INUKE kwa sababu za kiusalama zaidi..)

Binafsi ninayo GESI ndani na wala sihofii.

Mwisho, CONTROLLER wa Gesi au Jiko la Gesi awe ni mmoja au wawili wa kujielewa.. sio amekuja mgeni au watoto unawaachia wachezee jiko la gesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…