Ni hatari sana kwa nchi kutegemea ushauri wa Legal Officer (Hamza Johari), na kuiingiza nchi kwenye mkataba

Majungu katika ubora wake. Watanzania tumezoeshwa kupata kingi kwa kazi ndogo.

Tumezoeshwa riziki ya wizi kuwa sehemu ya riziki halali, wapo wapigaji wengi wa kimfumo waliojikuta wakipoteza riziki zao haramu tangu Hamza alipoteuliwa kuwa mkurugenzi wa TCAA miaka karibu nane iliyopita.

Wameshazoea ma-CEO wapigaji wanaoingilika kirahisi wakaja kugonga mwamba kwa aina ya utendaji wa Hamza.

Hayati JPM alimkubali sana namna anavyofanya kazi, alikuwa ni mtu wake wa karibu kwa sababu JPM alikuwa mpenda haki na mzalendo wa kweli wa Tanzania.

SSH ameingia madarakani yakaanza majungu wakidhani kuwa watarudia kupata zile riziki zao haramu kwa njia zao za panya, wakaanza majungu tena yale makubwa lakin Rais SSH anapita mule mule alimopita hayati na bado riziki zao zinaendelea kufungwa.

Haya majungu ya huu uzi ni sehemu tu ya chuki nyepesi dhidi ya Hamza Johari. Legal Officer alionyesha uwezo kwa hayati JPM akawa akimpa kazi nzito na nyeti na sio ajabu akawa kwenye team ya wanasheria walioipambania Tanzania huko Dubai ili ipate mkataba mnono wa pesa nyingi.

Cha kujiuliza inakuwaje Legal Officer tena mkurugenzi wa mamlaka ya anga anaongoza team ya wanasheria wa sekta ya bandari?.

Ukijiuliza kwa kina hilo swali utaupata ukweli kwamba tunayo elimu ya kubabaisha, tunao wababaishaji wengi wenye kushika nafasi nyeti na ndio wanaotuchelewesha kimaendeleo.

Nchi zinazotuzunguka kama Kenya, Uganda, Malawi na Msumbiji hazina haki ya kusimama na Tanzania kwa aina ya utajiri tuliojaliwa na Mungu. Lakini bado tunalo tatizo la weak manpower. Tuna uongozi mwingi dhaifu.
 
yaani wenyewe wanadanganya watu kuwa ni makubaliano ya awali, dah vitu havina hata backup ya sheria?, dah hapo ndio nachoka kabisa
 
yaani wenyewe wanadanganya watu kuwa ni makubaliano ya awali, dah vitu havina hata backup ya sheria?, dah hapo ndio nachoka kabisa
Now vina backup ya sheria ambayo ni azimio LA bunge tunachosubiri na kupitisha marekebisho September ya sheria zote kwa mujibu wa mkataba
 
Huyo naye bure tu mbona Pascal Mayalla ni wakili

Mkurugenzi unakuwa bush lawyer kweli?
 
is he a professional lawyer?, is he a member of professional? ni hilo tu mkuu, kama hakidhi hivyo sio professional lawyer
 
is he a professional lawyer?, is he a member of professional? ni hilo tu mkuu, kama hakidhi hivyo sio professional lawyer
Huwezi kuwa mkurugenzi mkuu wa TCAA yaani anga zima la Tanzania liwe chini yako halafu usiwe professional kwenye kazi yako!. Mikataba mingi ameingia kwa niaba ya serikali huu wa bandari ni maarufu kwa sababu ya unyeti wake.
 
Tatizo la mada hii ni lile lile la watanzania la miaka yote. Kudharau taaluma za watu haswa wale wasiowajua vizuri.

Tunachukulia poa sana elimu za watu na huu ni ushahidi wa sisi wenyewe kuwa na elimu za kubabaisha hivyo tunadhani kila mtu na yeye ni mbabaishaji tu.
 
TLS wanasemaje kuhusu uanachama wake na Chama Cha mawakili wa Tanganyika zungumzia suala hili au kwa kuwa amewekwa na Mamlaka za juu ya uteuzi.?
Ili kuepusha maswali na kuleta heshima ya taaluma husika,vigezo na masharti ya Tasnia yazingatiwe wakati wa kufanya uteuzi.
 
shida sheria ni professional, na wote wanasheria wanajulikana na wako regulated? sasa kama hujui kaa kimya
 
TLS wanasemaje kuhusu uanachama wake na Chama Cha mawakili wa Tanganyika au kwa sababu amewekwa na Mamlaka za uteuzi.? Ili kuepusha maswali mengi, na kuleta heshima ya taaluma husika,vigezo na masharti ya Tasnia yazingatiwe wakati wa kufanya uteuzi.
Rais JPM alimuamini tangu miaka ile ya ukaguzi wa vyeti. Ni msomi mahiri mimi ninamfahamu, tulikuwa wote Ukraine ile ya miaka ya tisini mpaka elfu mbili mwanzoni.
 
shida sheria ni professional, na wote wanasheria wanajulikana na wako regulated? sasa kama hujui kaa kimya
Profession ipi kwa mujibu wako wewe?. Alikuwa mwanasheria wa kampuni binafsi kabla hajachukuliwa mamlaka ya anga upande wa haki za wasafiri na baadae akaomba nafasi ya ukurugenzi akaipata enzi za JK.

Wakaweka kwenye makabati recommendations za JK na alipokuja JPM akamuona na kumchukua.

Profession yake anaitetea vyema ndio maana sekta ya anga kwa sasa imesimama kuliko wakati mwingine wowote huko nyuma. Huyo ni sehemu ya viongozi wa taasisi ya kidunia ya sekta ya anga ICAO akiwa ni kiongozi wa bara la afrika.

Unaongelea professionalism ipi labda?, huko kote afanye tu kazi bila ya kujua anafanya nini!

Unarudi kule kule kwenye kutazama haiba binafsi ya mtu badala ya kutazama substance nzima ya kile anachokifanya kwa maslahi ya Tanzania nzima. Tunaibiwa na wezi wanakuja kisomi kwa kutafuta watetezi wao humu jukwaani.

Mleta mada tuliza kichwa chako.
 
Rais JPM alimuamini tangu miaka ile ya ukaguzi wa vyeti. Ni msomi mahiri mimi ninamfahamu, tulikuwa wote Ukraine ile ya miaka ya tisini mpaka elfu mbili mwanzoni.

Achana na JPM. Na isiwe kigezo cha yeye kupendwa na mwendazake basi ndo akizi vigezo. Swali anavyovigezo vya kua mwanasheria wa serikali. Na weka ushaidi. Mwenzio kaweka hadi website kuangalia kama HJ yupo
 
Shida akili ikimekwisha shikiliwa na mwarabu, hebu soma kilicho andikwa MEMKWA nini? usikurupuke kujibu soma kwanza, ndio ujibu hoja, ndio maana mnaelezwa mkabata nehi mnang'ang'ania DP ataleta ajira
Ulichomaanisha kwenye huo uharo wako juu hapo ni kwamba huyo asiye mwanasheria kashauri mkataba, meaning tumeamini mtu asiye mwanasheria..ndo nikakuuliza ikiwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali haikuhusika tukategemea huyo mshauri...au hujui ulichoandika!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…