Kama kichwa kinavyoelezea hapo juu, kuna kampuni moja binafsi imenitapeli kiasi cha pesa. Sasa naomba kujua nawezaje kufungua kesi na kuishtaki ili niweze kupata haki yangu.
Pesa yenyewe ninayowadai ni kidogo (250,000) ndio maana nasita kwenda kushtaki kwa kuhofia kuwa kunaweza kuwa na gharama kubwa zaidi kuliko kile kiwango ninachodai.