Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

Toa pascal njaa. Hana anachojua. Mtu yeyote ambaye na F ya hesabu ni zero brain
Usimwonee Mkuu. Kusoma sheria huhitaji kufaulu hesabu. Wanasheria wengi wazuri sana walipata F ya hesabu O-Level, kama vile mainjinia wengi wazuri sana walipata F ya English O-level. You cant excel in everything. Messi hawezi kucheza basketball.
 
Hakuna engineer ambaye anaweza pata F ya English. Sema si maengineer Huwa tunafaulu vyote ingekuwa unaruhusiwa kuchukua masomo yote A level basi sisi tungechukua vyote. Ila Hawa ngwini Huwa hawana alternative nyingine mana sayansi ni zero hawawezi kabisa
 
Labda kweli. Lakini amini nakuambia, lawyers hawahitaji Mathematics ukiwaambia wanahitaji watakuambia that argument is null and void ab-initio!
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania)

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki raisi wa Tanzania mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha raisi anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama raisi anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa uraisi ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama raisi katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi raisi anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa raisi alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa raisi madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha raisi aondolewe madarakani?
Ebu kapitiepitie Sheria ya Mwaka 1992 Na. 20 ib. 8 na Sheria ya Mwaka 1995 Na. 12 ib. 4 halafu urudi tujadili.
 
Kwa ufahamu wangu, kuvunja katiba ni jambo linaloweza kufanya Rais aweze kuondolewa madaraka yake na bunge
 
Kwa katiba iliyopo sasa raisi kamithilishwa mungu, anachokisema ni sheria, kila analofanya ni sahihi, hakosei. Na hata ikionekana kakosea kabisa hapaswi kuhukumiwa.
 
Mkuu mie sio mwanasheria sijui hata hizo sheria nitazipata wapi. Tuwekee hapa
Wewe umeuliza kama Kuna Sheria yoyote ya kumwajibisha Rais wa JMT nami nimekupa hizo Sheria. Shida yako nini? Unaweza kuanzisha uzi JF, lakini kutafuta Sheria mtandaoni ukasoma huwezi? Pumbavu!!!
 
Wana JF nitafutieni Pascal Mayalla, Tundu Lissu nk waje huku watuongoze
Lissu mwenyewe kamiminiwa marisasi kila siku anabweka tuu makonda makonda, hakuna chochote anachofanya. Hapa hawezi kusaidia chochote.
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania)

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki raisi wa Tanzania mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha raisi anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama raisi anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa uraisi ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama raisi katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi raisi anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa raisi alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa raisi madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha raisi aondolewe madarakani?
Kwa mujibu wa katiba YETU pendwa Rais hatoshitakiwa kwa kosa lolote lile alilolitenda akiwa madarakani ama pia BAADA ya kustaafu MAJUKUMU ya urais.kama sijasahau.
 
Kwa mujibu wa katiba YETU pendwa Rais hatoshitakiwa kwa kosa lolote lile alilolitenda akiwa madarakani ama pia BAADA ya kustaafu MAJUKUMU ya urais.kama sijasahau.
Tuseme Raisi akiamua kuwauzia Kenya Mlima Kilimanjaro hakuna lolote tunaweza kufanya?
 
Wewe umeuliza kama Kuna Sheria yoyote ya kumwajibisha Rais wa JMT nami nimekupa hizo Sheria. Shida yako nini? Unaweza kuanzisha uzi JF, lakini kutafuta Sheria mtandaoni ukasoma huwezi? Pumbavu!!!
Sawa nakubali. Nimeitafuta nikaipata;

46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
inadaiwa kwamba Rais-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa
yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya
namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya
wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

Ila sasa nimegundua tatizo, kwamba ni kupitia Bunge tu ndio Raisi anaweza kuwajibishwa kwa kuvunja Katiba. Sasa ukiwa na Bunge kama hili tulilo nalo, ambapo karibu viti vyote viko CCM, Raisi anaweza kuivunja Katiba anavyotaka na msifanye chochote, kwa kuwa sio raisi wabunge wa CCM wakajenga hoja kumuondoa raisi kutoka CCM.

Hivyo basi, kimsingi, Katiba haijaweka mwanya wa kumwondoa madarakani raisi ambaye kwa makusudi anavunja Katiba. Kimsingi Katiba inasema kesi ya nyani itapelekwa kwa nyani. Very silly.
 
Tuiulize katiba.
Nimeona kwamba Katiba ina mapungufu sana. Ina fanya assumption kwamba unaweza kuwa na Bunge ambalo lina Raisi ambaye anatoka cahama ambacho hakina majority bungeni.

Suala la kumuwajibisha raisi anaekiuka matiba lilipasa liwekwe kwenye mhimili wa mahakama, sio bunge ambapo ni obvious wabunge wa chama anachotoka raisi watakuwa wengi na hawatakubali kumwondoa raisi wao
 
Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania).

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki Rais wa Tanzania Mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ili kuelewa suala lililopo labda tuchukue extreme case. Kwa mfano Raisi anaamua kuwauzia Kenya Mlima Kilimanjaro, hakuna tunaloweza kufanya itabidi tusubiri hadi uchaguzi ili tumtoe kwa kura?

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha Rais anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama Rais anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa Urais ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama Rais katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi Rais anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa Rais alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa Rais madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha Rais aondolewe madarakani?
Angalau umefanya homework. Ila kiukweli kwa Katiba JMT ni Bunge la JMT ndilo linaloweza kumuondoa Rais wa JMT madarakani (Impeachment). Na karibia nchi nyingi duniani ambacho ni Jamhuri zina utaratibu huo mfano Kenya, Afrika Kusini na Marekani kutaja chache.
 
Back
Top Bottom