Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

Ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa endapo Rais atavunja Katiba kwa kukusudia au kutokukusudia?

Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, kwamba ikiwa iko wazi na dhahiri kabisa kwamba raisi wa Tanzania anaekuwa madarakani, anaamua kwa makusudi na huku akijua hilo, au kwa kushauriwa vibaya, au kwa kutoelewa, anavunja Katiba ya Tanzania (yaani kufanya uamuzi au kuchukua hatua inayoenda kinyume na Katiba ya Tanzania).

Nauliza hivi kwa sababu ninaelewa kwamba huwezi kumshitaki Rais wa Tanzania Mahakamani, iwe yupo madarakani au amemaliza muda wake.

Ili kuelewa suala lililopo labda tuchukue extreme case. Kwa mfano Raisi anaamua kuwauzia Kenya Mlima Kilimanjaro, hakuna tunaloweza kufanya itabidi tusubiri hadi uchaguzi ili tumtoe kwa kura?

Ningeomba wale wenye ufahamu mzuri wa sheria au Katiba ya Tanzania wasaidie kujibu maswali haya hapa chini;
  1. Je, Tanzania tuna utaratibu wowote wa kisheria wa kumwajibisha Rais anaetenda kinyume na Katiba ya nchi kwa makusudi au kwa kutojua akiwa bado madarakani?
  2. Je chama chake kinawezaje kumwajibisha ikiwa raisi ndio anakuwa pia mwenyekiti wa chama chake?
  3. Je kama Rais anavunja katiba kimakusudi bado tunalazimika kusubiri hadi uchaguzi mkuu ili wananchi ndio waamue?
  4. Na je, ni halali chama cha siasa kuteua mtu kuwa mgombea wa Urais ikiwa kuna uthibitisho kwamba akiwa madarakani kama Rais katika awamu inayoisha alikuwa akivunja katiba?
  5. Je unaweza kumwekea pingamizi Rais anaemaliza awamu moja kugombea tena kwa sababu kuna uthibitisho kwamba akiwa Rais alivunja Katiba na hivyo hastahili kugombea uraisi kwa awamu nyingine?
  6. Je kuna uhalali wa kumwondoa Rais madarakani kwa nguvu (yaani mapinduzi) badala ya kungojea uchaguzi mwingine ikiwa anathibitika kuvunja Katiba mara kwa mara na chama chake hakina namna ya kumwajibisha, au hakuna utaratibu wa kidemokrasia unaowezesha Rais aondolewe madarakani?
Hao wananchi wanaijua katiba na maana ya katiba? Watanzania hata haki zao za msingi hawazitaki japo zipo na wanazijua, ndiyo sababu tunasema usimtetee mtanzania utaumbuka atakapokukana.
 
Katiba ya Tanzania sijawahi kuiona , ajabu ni kuwa tukiwa shule ya msingi somo la siasa Miaka ya 80 tulifundishwa katiba ya ccm na karibu kila mwanafunzi alikuwa nayo .
 
Back
Top Bottom