Ni huduma ipi inayotolewa na Serikali ndani ya Jamii unaifurahia kwa asilimia kubwa?

Ni huduma ipi inayotolewa na Serikali ndani ya Jamii unaifurahia kwa asilimia kubwa?

Mada kama hizi lazima watu waanze matusi.
 
Huduma zinazotolewa na Taasisi,Idara,Mashirika,Wakala na kwingineko.

Mimi binafsi katika utafiti wangu mdogo idara ya maji inajitahidi sana kutuma bili kwa wakati.

Pamoja na watu wengi kulalamikia bili hizo kuwa zinakuwa na bei kubwa ukilinganisha na matumizi lakini wamepiga hatua kubwa.

Vilevile wamejitahidi kuunda Group za WhatsApp kwa ajili ya kupokea kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati.

Vipi kwenye eneo unalotoka huduma zipi zinatolewa vizuri?
Inafikirisha! Idara ya maji wajibu wake mkuu ni kutoa huduma ya maji. Mteja anaridhishwa kwa jinsi Ankara ya malipo inavyomfikia mapema anaona ni huduma!
 
Inafikirisha! Idara ya maji wajibu wake mkuu ni kutoa huduma ya maji. Mteja anaridhishwa kwa jinsi Ankara ya malipo inavyomfikia mapema anaona ni huduma!
Ni huduma mojawapo kwani ni nini?
 
Back
Top Bottom