Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea wa Urais CHADEMA 2015? Lipi lilikuwa kosa la Dkt. Slaa?

Pamoja na Kuhamia CHADEMA Lowasa Bado aliendelea kuwa na ulinzi wa TISS

Thibitisha kuwa gharama za hoteli alilipiwa na ccm
- Hapa namzungumzia Dr. Slaa sio Lowassa, sasa uniambie kwanini Dr. Slaa apewe ulinzi na TISS? yeye ni nani?

- Sijui unataka uthibitisho upi tena, nimekwambia mwenzie waliehongwa nae alikwenda kula bata Rwanda, yeye kwa ubahili wake akaamua kujibanza hapa bongo, sijui huelewi kitu gani!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sababu kuu zilikuwa tatu ambazo chadema ndio wakaamua hivyo

Ya kwanza walisema ni zamu ya mtu wa kaskazini kutoa uraisi .Lowasa na Slaa vigezo hivyo vyote waliweza

Cha pili Chadema walitaka mgombea awe na pesa za kutosha za kuendesha kampeni nchi nzima Lowasa alikuwa nazo Slaa hakuwa nazo Lowasa kipengele hicho akamshinda Slaa .Lowasa alimwaga pesa sio utani nchi nzima Kwa wagombea wa chadema wote na Kwa ajili ya kampeni

Kipengele Cha tatu Chadema walitaka mgombea awe Mlutheri kuwa wakatoliki wameshashika ni zamu ya walutheri dini Ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutoa Raisi .Lowasa Mlutheri wakati Slaa mkatoliki .Lowasa akashinda Slaa akatupiliwa mbali

Hivyo vigezo vitatu Slaa alizidiwa kimarks na Lowasa.Akapigwa chini na umaarufu wake wote
 
Kama unaamini wapinzani waliomkataa Lowasa walihongwa na CCM weka ushaidi wa wazi.
Kama unaamini bila ushahidi wa wazi Kwa nini unapata ugumu kuamini kuwa LOWASA aliwahongo CHADEMA ili wamkubali na wampitishe katika dakika za lala salama kuwa mgombea wa chama chao.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Chama kikubwa kama CHADEMA hakiwezi kuchukua mtu aliyekataliwa na CCM waliomlea na kuwa mgombea wao wa kiti cha urais. Kibaya zaidi Viongozi zaidi ya watano wa kamati kuu ya CDM akiwemo M/kiti na katibu mkuu wakati huo walikuwa wamemtuhumu LOWASA kwa wizi na ufisadi waz wazi
Kipi kiliwafanya CDM wampitishe LOWASA KUWA mgombea wa kiti cha urais 2015?
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nimekupa mfano kuthibitisha kile ninachokwambia kumhusu Dr. Slaa, kaba alihongwa hiyo pesa akaitumia kukaa hoteli na TISS wakampa ulinzi, hili mbona lipo clear kabisa...

Sasa wewe unayetaka kutuaminisha wapinzani walihongwa kumpitisha Lowassa ndio utupe ushahidi, kwasababu mimi ninajua Lowassa alipitishwa na vikao halali vya chama.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ni ipi hasa ilikuwa sababu ya kusimamishwa EL?
EL alidanganywa na nabii wa Nigeria kwamba yeye ndiye rais wa awamu ya 5.

Alitoa sadaka kwa nabii yule kisha akaja kama kumhonga Mbowe agombee kwa tiketi ya CDM, wapenda mageuzi pia hasa walokole (ondoa wasukuma na wagogo) tuliingizwa mkenge na huo unabii tukala sadaka ya Ngoyayi ila EL hakuchaguliwa kwa sababu aliutafuta urais kwa njia ya rushwa.

Sasa sintasahau huo ujinga.
 
Unapoandika chama kikubwa kama Chadema hakiwezi kumkataa mtu aliyekataliwa na CCM hayo kwangu ni mawazo yako, sitakiwi kuyapinga.

Lakini kuna sababu za kisheria, zenye mantiki kabisa zinazokizuia Chadema kutompokea yeyote anayetaka kujiunga nao, wakati wowote, bila kujali itikadi, rangi, dini, jinsia, au vyovyote vingine.

Are you there?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Tukio la sumu ilikuwa baada ya ripoti kusomwa na ilikua 2011.

Miaka 3 mbele, kiufupi hakuna genge lililoifilisi Tanzania kama hilo, maana story yao haikuanzia hapo bali kwa Dr .Omari Ally Juma ikaja kwa Salim na wengineo hakuna ambaye hakukumbana na mkono wa hili genge kwa namna yake pale alipotaka kulizibia upenyo kimaslahi.

Ila mwisho lilikuja kupishana na kusambaratika ndio kilichotokea maana kisasi lazima kingetokea mtolewa sadaka angeshika nchi maana aliahidi kumleta hata yule gavana tuliyedanganywa alikufa.

Inasikitisha sitaki hata kukumbuka hili genge lilivyoivuruga nchi kwa kigezo wao ndio watoto wa mjini.
 
Sasa wewe unayetaka kutuaminisha wapinzani walihongwa kumpitisha Lowassa
Ushahidi gani sasa unaoutaka?

Ile sadaka aliyoitoa kule Lagos unadhani ilikuwa sadaka kama ya matonya?

EL alimhonga nabii ili tangazo la nabii litangazwe madhabahuni ili liwalainishe walokole lia lia na ndivyo ilivyofanyika.

Slaa akifanywa tu kuwa mbuzi wa kafara.
 
Kwa sababu viongozi wa chadema walimtuhumu lowasa kwa wizi.

Kwa mantiki hiyo chama kina watu wengi wazuri lakini kwa nini kiliamua kumchukua mgombea mwenye tuhuma na kuwaacha wanachama wengi wasafi na wanayoijua na kuipigania itikadi ya CDM?
 
Mimi nasema umjiuliza maswali ya kipumbavu sana aisee.

Kwani wewe ukiulizwa maswali haya utajibuje, kwamba;

1. kitu gani hasa kiliifanya CCM kumsimamisha John P. Magufuli 2015?

2. Je, ni kwa sababu CCM ilikosa mgombea mzuri zaidi yake?

3. Aliletwa Kwa maslahi ya chama au watu wachache?

## Na hayo mengine yote yageuze yawe ya huko kwenu CCM na mgombea wenu..

## Na majibu utakayoyapata ndiyo hayohayo yatakuwa majibu ya maswali yako yote juu ya CHADEMA na Edward Lowassa 2015...!!

Pole sana..
 
Taja kiasi alicholipiwa Dr. Slaa Hotelini na list ya jina la mlipaji. Tutajie pia majina ya walizi wa TISS NA namba za vitambulisho vyao. Huo ndo aina ya ushaidi unaotakiwa

Ndugu yangu jielimishe kujua aina mbalimbali za ushaidi unavyotakiwa uwe itakusaidia kujenga hoja
 
Ni uongoo huu uongo😂😂😚
 
Wewe ni kilaza
 
Hii nayo nyingine tena, so Lowassa alienda Nigeria kujisafisha na tuhuma dhidi yake badala ya kujisafisha mwenyewe?

Ok nimekupata!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kwa sababu viongozi wa chadema walimtuhumu lowasa kwa wizi.

Kwa mantiki hiyo chama kina watu wengi wazuri lakini kwa nini kiliamua kumchukua mgombea mwenye tuhuma na kuwaacha wanachama wengi wasafi na wanayoijua na kuipigania itikadi ya CDM?
Sasa hao watu wengi wazuri si ndio walikutana kwa pamoja wakaamua kulipitisha jina la Lowassa?

Sioni shida, wewe unawataka wao, wao wakamtaka Lowassa, inakubidi ukubali maamuzi yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…