Ni ipi Hoteli nzuri Morogoro?

Hoteli nzuri pale ni nyumbani kwa mjumbe wa mtaa, ukifika Moro mtafute mjumbe akupe hifadhi ya siku kadhaa.
 
Ni yale madude flani inayoelekea zamani enzi zake yalikua fresh lakini siku hizi zimechuja.

Na mimi ndio nachojaribu kukwepa hicho. Kwavile sijafika moro mda kama miaka mi3-4 nna wasiwasi hoteli zilizokua nzuri enzi hizo zinaweza zisiwe nzuri kwa sasa. Ila nilichogundua moro hapajajengwa hoteli mpya kwa miaka ya karibuni so itabidi nikapambane na hizo hizo au nishuke kwenye loji.
 
Tafuta lodge tu, maana kwa kiasi hicho hauwezi kulala Kingsway, Flomi au Morena.
 
acha dhereu nyoko hahahaha, japo umeongea ukweli.
 
Tax palace, top life Kuna hotel karibu mpya kabisa
 
Mbwembwe zote ukute unalala peke yako na gebe zako za kutaka hotel Kubwaaaaa!
Daaah mkuu hivi kweli ningekua nalala peke yangu ningehangaika kuja mpaka huku kutafuta chumba? Mimi mbona chumba cha 15,000 tu nalala fresh kabisa?πŸ˜„
 
GM, QUEENS, KIBO PEAK, STARPACK HOTEL (ingawa vyumba vina socket moja tu iliyopo nyuma ya kabati, lakini ni mpya)
 
Kuna hoteli moja nilika siku mbili nimeisahau jina ila njia panda ya msamvu kuelekea mjini unanyooka na hiyo barabara mpaka njia panda ya pili unachukua mchepuko wa kulia kutoka hapo njia panda ya pili ni kama mita 200, ni ghorofa na pasafi na pana parking...vyumba 40 mpaka 80000 daraja unalotaka...nilikaa cha 55000, sijutii...nimesahau jina lake ila ni barabarani tu...
Na msamvu boda boda ni buku...panaweza kuwa kama kilometa mbili au tatu mpaka msamvu...
 
Nawashukuru kwa msaada wenu wakuu. Kuna loji nimepata chumba kina sebule yenye sofa set, bedroom na veranda kwa nje, full AC, dstv, simu, maji moto na room service kwa Tsh 40,000. Mliokua mnanitisha kwendeni zenu huko hamuijui Moro nyie..πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…