Ni ipi Hoteli nzuri Morogoro?

Ni ipi Hoteli nzuri Morogoro?

Hoteli nzuri pale ni nyumbani kwa mjumbe wa mtaa, ukifika Moro mtafute mjumbe akupe hifadhi ya siku kadhaa.
 
Ni yale madude flani inayoelekea zamani enzi zake yalikua fresh lakini siku hizi zimechuja.

Na mimi ndio nachojaribu kukwepa hicho. Kwavile sijafika moro mda kama miaka mi3-4 nna wasiwasi hoteli zilizokua nzuri enzi hizo zinaweza zisiwe nzuri kwa sasa. Ila nilichogundua moro hapajajengwa hoteli mpya kwa miaka ya karibuni so itabidi nikapambane na hizo hizo au nishuke kwenye loji.
 
Tafuta lodge tu, maana kwa kiasi hicho hauwezi kulala Kingsway, Flomi au Morena.
 
Mkuu yani na mimi ndio kinachonishangaza. Moro nalipaje laki mji hauna kivutio chochote? Hakuna bahari, hakuna mbuga ya maana, hakuna mlima? 😄😄😄 Ila nadhani labda kwavile hoteli zipo chache ndio maana wanajipangia bei wanavyotaka.

Mfano nilikua naiangalia moja jina sitaji ambayo ilitaka kubomolewa kipindi cha nyuma. Mtandaoni wanaonekana wanachaji 232,000!
  • hoteli ipo katikati ya mji, karibu na highway means makelele vurugu kama zote ukitoka tu getini unakutana na bodaboda, mama ntilie wanauza vitumbua nk
  • hoteli haina hata garden useme jioni utatoka upumzike
  • hoteli haina swimming pool
  • hoteli haina hata gym tu achilia mbali huduma zingine jacuzzi, sauna nk tusiende huko

Sasa hiyo 200k nalipia nini hasa, kitanda?? Hapo ukute hata dstv wamejiunga kifurushi cha 9000😀. Na mtu kabisa anakuja kujisifu eti nimelala hoteli nzuri. Mzee umepigwa! 😄😄 pale sanasana labda wangechaji 40,000 ningewafikiria 🤣🤣
acha dhereu nyoko hahahaha, japo umeongea ukweli.
 
Nategemea kwenda Morogoro kwa shughuli za kiofisi. Naomba anaejua hoteli nzuri isiwe mbali sana na Msamvu anijuze. Napendelea hoteli mpya mpya kwani ndio hua zinakua bado safi, vyoo havijagandia ukurutu, na magodoro hayajawa chapati.

Kwavile nina muda kidogo sijafika Moro, naomba msaada kwa aliefika siku za karibuni. Bajeti 50,000 - 60,000 kwahiyo sitafuti vi loji vya uchochoroni. Natanguliza shukrani.
Tax palace, top life Kuna hotel karibu mpya kabisa
 
Mbwembwe zote ukute unalala peke yako na gebe zako za kutaka hotel Kubwaaaaa!
Daaah mkuu hivi kweli ningekua nalala peke yangu ningehangaika kuja mpaka huku kutafuta chumba? Mimi mbona chumba cha 15,000 tu nalala fresh kabisa?😄
 
GM, QUEENS, KIBO PEAK, STARPACK HOTEL (ingawa vyumba vina socket moja tu iliyopo nyuma ya kabati, lakini ni mpya)
 
Nategemea kwenda Morogoro kwa shughuli za kiofisi. Naomba anaejua hoteli nzuri isiwe mbali sana na Msamvu anijuze. Napendelea hoteli mpya mpya kwani ndio hua zinakua bado safi, vyoo havijagandia ukurutu, na magodoro hayajawa chapati.

Kwavile nina muda kidogo sijafika Moro, naomba msaada kwa aliefika siku za karibuni. Bajeti 50,000 - 60,000 kwahiyo sitafuti vi loji vya uchochoroni. Natanguliza shukrani.
Kuna hoteli moja nilika siku mbili nimeisahau jina ila njia panda ya msamvu kuelekea mjini unanyooka na hiyo barabara mpaka njia panda ya pili unachukua mchepuko wa kulia kutoka hapo njia panda ya pili ni kama mita 200, ni ghorofa na pasafi na pana parking...vyumba 40 mpaka 80000 daraja unalotaka...nilikaa cha 55000, sijutii...nimesahau jina lake ila ni barabarani tu...
Na msamvu boda boda ni buku...panaweza kuwa kama kilometa mbili au tatu mpaka msamvu...
 
Nawashukuru kwa msaada wenu wakuu. Kuna loji nimepata chumba kina sebule yenye sofa set, bedroom na veranda kwa nje, full AC, dstv, simu, maji moto na room service kwa Tsh 40,000. Mliokua mnanitisha kwendeni zenu huko hamuijui Moro nyie..😆😆
 
Back
Top Bottom