Ni ipi kozi yenye ajira kati ya Business Administration na Accountancy?

Chale david

Member
Joined
Jun 12, 2023
Posts
51
Reaction score
27
Naombe msaada kujuzwa kozi nzuri kati ya Bussness Administration na Accountancy ipi yenye ajira zaidi?
 
Zote zina ajira, mchawi Connection.. ukishasoma Accounts hakikisha una CPA, au angalau Masters!

Hiyo Business Administration ukipiga na Masters yake itakuwa mali sana!
 
Nooooo,halikisha ukisoma business courses cha kwanza fikiria kujiajiri tu mengine yaje km alternative.
Kwahiyo mtu anasome accounts au BBA ili ajiajiri???... Kuna haja ya kukagua ninayebishana nae!... Nakutakia jioni njema!
 
Kwahiyo mtu anasome accounts au BBA ili ajiajiri???... Kuna haja ya kukagua ninayebishana nae!... Nakutakia jioni njema!
Sio wote wanaosoma ni maskini kuna wanaosoma wasimamie mali za familia kuna wanaosoma wanapewa mitaji kuanzisha biashara au miradi ya familia,kuna watuwanasubiriwa wamalize wapewe kazi endelea kuamini hivyo hivyo
 
Una elimu gan??... Yani Kwa jinsi ulivyojibu unaonekana Kabisa huna elimu... Ndo maana unakatisha watu tamaa
😅😅😅Jamaa amekuambia ukweli na hualisia wa Ulimwengu juu ya Elimu... Tumia akili kutafakari utamuelewa ila ukitumia hayo makaratasi yako unayoita Elimu hutomuelewa
 
Sio wote wanaosoma ni maskini kuna wanaosoma wasimamie mali za familia kuna wanaosoma wanapewa mitaji kuanzisha biashara au miradi ya familia,kuna watuwanasubiriwa wamalize wapewe kazi endelea kuamini hivyo hivyo
Ushataja mtaji tayari... Yani baada ya kugraduate ni familia ngapi zitaafford kukupa wewe mtaji... 0.001% Tusiongopeane hapa ... Hii ni Tanzania almost 80% mpka 90% ni watoto wa wakulima(Kipato cha chini) Na tunasoma tuajiriwe kisha tuzikomboe familia zetu!!... Hii mitazamo ya kujiajiri ni nadharia za uongo... Na hata ikitokea mtu amejiajiri basi lazma afanye kazi walau miaka mitano mpka kumi kisha ndo aamue kufanya Mambo yake mfano kilimo,biashara au Kampuni binafsi mfano nzuri ni Fred Vunjabei... Aligraduate na BBA... akaajiriwa serikalini baada ya Muda(Alipopata mtaji) akaamua kuacha na kufungua biashara zake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…