Ni ipi njia nzuri ya kuishi na mwanamke anayeonesha dalili zakutaka kumtawala mwanaume wake?

Ni ipi njia nzuri ya kuishi na mwanamke anayeonesha dalili zakutaka kumtawala mwanaume wake?

Hakuna kitu inaitwa bahati duniani, hata bahati nasibu watu wanashinda kwa sababu walichukua hatua ya kununua tiketi!

Sasa wewe labda katika maisha yako unavutiwa na wanawake wabishi wabishi, wajeuri jeuri, na baadye unakuja kuchukizwa na hizo tabia. Haiwezekani wote wawe wanaficha makucha yao hadi muoane. Mwanamke mjeuri utamgundua tu, au watu wengine watakuambia pale moto usiguse!
Unaongea kutokana na ubishi, ujuaji na mihemko vimekujaa!

Haya umeshinda! We ndo unajua zaidi na wewe ndo upo sahihi na wewe ndo umeshida 🙌👍
 
Ongea kwa vitenso na sio maneno mkuu. Acha kumlalamikia kabisa kila anachofanya we mtazame na una respond kana kwamba hujui nini kafanya.
 
Ndugu zangu wana Jf Salaam sana.

Ndugu zangu kweli mimi nilikua mkereketwa wa chama cha wanaokataa ndoa ila mwisho wa siku niliona huwezi kuwa rijali na ukakataa kuishi na mwanamke . Nilikusanya akili zangu na kuamua kuoa sasa leo hii nipo hapa kuomba ushauri wa namna nzuri ya kuishi na mwanamke anayeonyesha kila dalili ya kutaka kumtawala mwanaume.

Mimi nimeoa ila kipindi cha uchumba mke wangu alikua ananisikiliza sana na alikua nikimuongoza anafata kwa usahihi yale yote niliyokua na mwelekeza na alinionyesha tabia njema mpaka nikavutiwa kumuoa

Sasa Kilichokuja kutokea ni baada ya kumuoa ndiyo ameanza kunionyesha mabadiliko mara kwa mara.

1: MKE WANGU, Amekua akinionyesha kwa maongezi na vitendo vyake kwamba ana kila dalili ya kutaka kunitawala mimi mume wake , hata kupitia mazungumzo yake na lawama zake unaona kabisa hapa anatak kunitawala.

2: MKE WANGU, Amekua akinitaka mimi mume wake nifate kila utaratibu wa maisha anaosema yeye jambo ambalo linaashiria kabisa anataka mimi mume wake nikae kwenye mfumo jike wake na siyo yeye kukaa kwenye taratibu zangu

3: MKE WANGU, amekua akiishi na mimi kama mtu mwenye machale machale mguu nje mguu ndani na mara nyingi tukipishana kauli amekua akiniambia kama simtaki au nimemchoka ni mwambie aondoke.

4: MKE WANGU, amekua akiongea kauli ambazo zinakua na amri amri ndani yake mfano, nataka , naenda, nipe, niletee, kama hutaki niambie au fanya.

5: MKE WANGU , amekua akijifanya yeye ni mweye misimamo mikali hata kama haina maana yeyote ile, aking'ang'ania jambo ameling'ang'ania hasa.

6: Mbali na yote hayo hata akiongea ujinga , akikosea au akinijia juu anataka mimi ndo nishuke nianze kumbembeleza na kumwelekeza kwa upole. na siyo yeye kushuka kama ilivyo desturi ya mwanamke awe mnyenyekevu na mtiifu kwa mumewe.

Nb.

Ndugu zangu mimi kwa upande wangu kaa mwanaume kuhusu majukumu mengine kweli mke wangu anajitahidi ila kuhusu hayo hapo juu nimeweka msimamo kwamba sipoteyari kwa namna yeyote ile kukubaliana na mambo yake na kila mara na mwambia mwanaume ndiye nguzo, msimamizi na kiongozi wa mwanamke.


SASA NIPO HAPA NAOMBENI NAMNA NZURI YA KUISHI NA MKE WANGU MWENYE KILA DALILI YA KUTAKA KUNITAWALA NA KUTAKA MIMI NDIYE NIWE NA MSIKILIZA YEYE NA MWENYE KUJISHUSHA KWAKE MAANA MIMI SIPO TEYARI KABISA KUKUBALIANA NA MAMBO YAKE.

"" MSINISHAURI NI ACHANE NAE MAANA KWA STYLE HII NIMESHA WAACHA WENGI SANA"

ASANTEN:;-
Ukicheka na kima utavuna ushuzi
 
Loading failed ukweli mchungu ni kuwa, 'mwanamke hatoacha kukupima maisha yako yote' hivyo kamwe usilegeze kamba, tena kama ndiyo 'wenzangu na Mimi' ushasema, hili kabila kuna namna tupo bold naturally tu, yaani ukiwa dhaifu hakuna rangi utaacha kuona..!!

Kuwa mkali, kuwa na misimamo, hakikisha sana usiyumbishwe, ukikubali kuwa chini kwenye moja amini nakuambia umefungua mlango kuletewa ujeuri kwenye lingine..!! Hakuna mwanamke anapenda mwanaume dhaifu, laini laini, analegeza legeza, tunapenda wanaume wenye AMRI, na Ile MANHOOD hasa..!! kama wewe ni wa zile za 'babe babe' kwenye kila situation shauri yako,

Mwanamke wako akizingua unatakiwa uwashe moto hasa mzee, ukimuangalia jicho moja anaomba samahani, nyie endeleeni na mapenzi ya Kikorea..!!

Nashukuru sana hakika nitazidi kukaza kamba sana na kuzingatia haya yote, kuliko nimlegezee hakika bora ndoa isambaratike
 
Huyo kama akiwa anakuletea zile za kama hautaki sema ,Wewe muulze kwani ww unatakaje!? Sjui nataka uje nyumbani sshv kama upo busy mwambie kwa sasa nko busy ila baadae kdgo nitakuwa home akianza kama kufoka muulze huko kufoka kwako unamaanisha nn yani! Unatakaje sasa, Niamini atakuwa anatulza mshono.
Shukrani nitazingatia mkuu
 
Sasa jitahidi kumkwepa..
Rudi nyumbani kulala tu, pia jitahidi sana ktk Chakula usile peke ako, akipakua na yeye ale hicho hicho.

Pia jitahidi wakati wa kulala usilale kama Ng'ombe, jitahidi ukae mkao.

Pia usiwe mtu wa maneno meengi, timiza wajibu wako kama Mume hasa wa kuacha kodi ya meza na kulipa bills.

Ukirudi hakikisha unarudi na zawadi.. muachie kisha oga vzr kula msosi.. lala.

Pia tafuta faraja nje ya Ndoa.. (Jiongeze) tafuta mtu wa kukupa furaha na amani ya moyo.. si lazima awe MPENZI.
Leta namba ya simu
 
Mchango mzuri sana kiongozi, ila tafadhali rekebisha hapo mwisho chini... Sio atafute mtu wa kumpa faraja, bali atafute kitu cha kumpa faraja, amani na raha. Usimshauri mwenzako kutoka nje ya ndoa yake ingawaje hana sababu ya msingi wala hajaligundua na kulithibitisha hilo kwa mwenza wake. Otherwise anatafuta mabalaa, mamikosi, magonjwa na malaana.

Ahsante!
Ahsante.. ndio maana nikasema si LAZIMA awe Mpenzi..

Inaweza ikawa washkaji zake.. Mama ake, Baba, Dada etc..

Faraja inakuja kwa njia nyingi, mfano mimi Faraja yangu ni kuona watu wangu wa karibu wakifurahia Maisha.
 
Back
Top Bottom