Ni ipi njia nzuri ya kupunguza uvutaji wa sigara?

Ni ipi njia nzuri ya kupunguza uvutaji wa sigara?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
11,208
Reaction score
20,517
Hallo wakuu, na imani mpo salama kabisa time hii.

Samahani naomba kuuliza kwenye uelewa wa swala hili.

Ni hivi tangu nikiwa advance level nilikuwa napenda sana na kuvutiwa na cigarette, lakini kutokana na mazingira ya school zetu hizi za boarding nikashindwa kufanya nachotaka na ninachopenda.

Basi after maisha ya advance nikaanza life jipya na ambalo nilikuwa na feelings nalo tangu nikiwa kinda.

Moja ni kuvuta sigara.

Kutokana na mazingira ya kibongo bongo kwa mwanamke ukioneka kwa public ya kiswaz unapiga vyombo kama hivyo basi utaitwa majina yote mbaya.

Kwa hiyo nikaamua napiga vyombo kwa home au zile sehemu za starehe lakini zenye watu wanaojilewa na vile nilikuwa Rasi kwa hiyo hakuna hata mutu alikuwa na Time ya kunishangaa, maisha yanaendelea.

Maisha ya kaenda miaka ikaongezeka lakini naona it's too much kwa kweli kwani navuta sigara paketi moja hadi moja na nusu kwa siku, sasa naona kabisa ni hatari kwa afya yangu na nimekuwa addicted kwenye hilo.

Sasa nataka nipunguze hadi nifikishe sigara mbili au tatu kwa siku nifanyeje?

Am sorry
 
Unaweza kuanza kwa kuweka ratiba na muda ya uvutaji, kama ulitumia sigara 20 kwa siku weka mpango wako wa kutovuka sigara kumi kwanza.

Unaweza kupanga muda wa kuwa saa 4 asubuhi, saa 7 mchana, saa 9 alasiri na saa 1 jioni kwa kufanya hivi utajikuta unavuta sigara 8 hadi 10 pekee.

Na pale utapofikisha sigara 5 basi tafuta mama anayenyonyesha akutilie maziwa katika sigara, hali utakayopata utaacha matumizi ya sigara.
 
2366484_downloadfile-3.gif
 
Pole sana hili ni tatizo ambalo unaweza kuliacha lakini lazima ukubaliane kuachana na marafiki wa hovyo.

1. Chagua marafiki wema wasio walevi wa sigara
2. Marafiki walio makini wasiojihusisha na sigara
3. Fanya mazoezi sana kuepuka kuwa na muda wa kutembelea sehemu za ajabu
4. Marafiki wanao mjua Mungu ili upate ushauri kiafya
5. Fanya kazi sana kuwa Bize
6. Tumia muda mwingi kanisani na semina za kidini.
7. Soma biblia sana
 
Pole sana hili ni tatizo ambalo unaweza kuliacha lakini lazima ukubaliane kuachana na marafiki wa hovyo.
1.chagua marafiki wema wasio walevi wa sigara
2.Marafiki walio makini wasiojihusisha na sigara
3.Fanya mazoezi sana kuepuka kuwa na muda wa kutembelea sehemu za ajabu
4.Marafiki wanao mjua Mungu ili upate ushauri kiafya
5.Fanya kazi sana kuwa Bize
6.Tumia muda mwingi kanisani na semina za kidini.
7.Soma biblia sana

You totally missed the point 😷

Hivi Usipovuta sigara na kunywa pombe ndio unakuwa rafiki mwema? Hovyo kabisa.

Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Pole Sana mamie.

Yaani Fegi balaa.

Binafsi ninapigana kuacha. Daah japokuwa ninazijua vyema njia sahihi za kuquit lakini wapi.

Kuna Kipiñdi ninakaa miezi 3 bila ya kuvuta but unfortunately Ninarudia Tena😁😁

Ila nimeweza kupunguza 20 Cigs a day,kuwa 5 kwa Sasa.

Siri ni KUNYWA MAJI KWA WINGI ninappsikia hamu ya kuvuta.

Pia Mazoezi mengi Kama kuruka kamba, push ups, pull ups, squats, planks(normal&side).

Sigara ni tamu mno ila ni mbaya sana kiafya hususani tukija kuwa wazee, COPD, Saratani, CDs etc.

Kuacha kunahitaji COMMITMENT and dedications.

Angalizo:

Kàma hujawahi KUVUTA, PLZ PLZ PLZ DONT DO IT.
 
Kwakweli nina hali kama yako au nimekuzidi!Kuna siku nilisahau kuwa na stock ndani, basi ile nataka kupiga fegi kabla ya kulala si stock imekauka! Daah kucheki maduka ya jirani yamefungwa,nilichoma mafuta kwenda kununua!Sikuweza kuvumilia kupitisha usiku ule bila kuvuta!

Huwa ninaweza kukaa masaa hasa nikiwa busy,ila nikishakula tu lazima kiu inibane sana!Pia nikigusa pombe tu,basi naunga tu moja baada ya nyingine!

Nilianza kuvuta sigara ili nisivute bangi maana kampani yangu walikuwa wanavuta bangi tukiwa sekondari! So tulikuwa tukikaa chimbo wanasokota, walikuwa wanachanganya na tumbaku nusu sigara ya portsman, sasa kile kipisi kilichobaki mimi ndio nilikuwa nazuga nacho! Kuja kushtuka ile nicotin ilishanikaa!Nikaliendeleza mpaka leo miaka zaidi ya 15 imepita!

Nilishajaribu kuacha ila kila nikigusa pombe najikuta nimerejea!

Kwasasa najaribu kuwa busy ili nivute nikishatoka mihangaikoni!Walau natembeza sigara 10-15 kwa siku!
 
Ni YESU tu ambaye anaweza kukutoa kwenye kila aina ya kifungo cha shetani. Uvutaji wa sigara ni kazi ya mapepo kama zilivyo dhambi nyingine. Na kushughulika nayo unahitaji msaada wa yeye aliye na nguvu zaidi. Jina lake ni Yesu Kristo Mwana wa Mungu alye hai.
 
Ni YESU tu ambaye anaweza kukutoa kwenye kila aina ya kifungo cha shetani. Uvutaji wa sigara ni kazi ya mapepo kama zilivyo dhambi nyingine. Na kushughulika nayo unahitaji msaada wa yeye aliye na nguvu zaidi. Jina lake ni Yesu Kristo Mwana wa Mungu alye hai.
Ha ha ha hayaa.

Asante komredi dada mchungaji!
 
Dada mimi zimenitesa, saiz napiga mda wa kinywaji tu na si vinginevyo. Nilichofanya ni kupiga kazi sana, kazi yangu huwezi vuta sigara. Nikichoka baada ya hapo napumzika, kwa kulala au sehemu nzuri. Muda wa saa mbili najichanganya kwenye mvinyo napiga tatu au nne pamoja na tungi zinatosha. Na saiz kinywaji na piga mara chache kwa wiki ata uvutaji, hauniendeshi.
 
Pole Sana mamie...

Yaani Fegi balaa...

Binafsi ninapigana kuacha....daah japokuwa ninazijua vyema njia sahihi za kuquit...lakini wapi....

Kuna Kipiñdi ninakaa miezi 3 bila ya kuvuta but unfortunately Ninarudia Tena😁😁

Ila nimeweza kupunguza 20 Cigs a day,kuwa 5 kwa Sasa....

Siri ni KUNYWA MAJI KWA WINGI ninappsikia hamu ya kuvuta...
Pia Mazoezi mengi Kama kuruka kamba,push ups,pull ups,squats,planks(normal&side).

Sigara ni tamu mno..ila ni mbaya Sana kiafya hususani tukija kuwa wazee,COPD,Saratani,CDs etc.

Kuacha kunahitaji COMMITMENT and dedications.....

Angalizo:

Kàma hujawahi KUVUTA,PLZ PLZ PLZ DONT DO IT.
Hivi mkuu kuna uhusiano kati ya pombe na sigara eeh?
 
Back
Top Bottom