Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

Namzungumza AMani Karume. Abeid Karume alikua ni muafrika alioa Chotara. Acheni kupotosha historia
Kwani ni kipi nilichopotosha hapo mkuu wangu 'dos.2020? Mimi nimeuliza swali baada ya kutoelewa ulichoandika wewe, halafu sasa unanigeuzia kibao kwamba ninapotosha?

Hawa 'machotara' ndio waarabu wa Oman, au huko Oman kuna waarabu asilia kama zilivyo nchi nyingine za kiarabu? Watu hawataki kulijibu hili swali, sijui kwa nini?
Hebu tusaidie wewe mkuu 'dos.2020, kama unayaelewa vizuri haya mambo.
 
Na haya unayoyaeleza ndio matamu kabisa.

Kumbe awali na awali kabisa, kabla ya ujio wa hawa wakoloni, wote, akiwemo na huyo Mwarabu Sayyed Said, Zanzibar na Pemba zilikuwa ni part and parcel' ya Tanganyika. Sultan hakuwa na tofauti yoyote na hao wakoloni wengine. Mtu utatokaje huko mbali kote, na kwenda kuweka koloni lako mlangoni kwa mtu mwingine!

Zanzibar will forever be part of Tanzania.
 
Hao machotara ni kizazi Cha waarabu wa Oman,washirazi wa Iran na muafrika wa visiwani
 
Kwa nini isiwe part na parcel ya Kenya!?..maana wapemba wakiwa karibu zaidi na mombasa
 
EeeenHeeee!

Nimekuelewa mkuu. Umejitahidi sana, na kwa kweli niseme wazi, nimekuchukulia kuwa ni mtu mwenye subira.

Sasa baada ya yote haya, uamini wangu wa kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania unazidi kuimarika zaidi, kwani najuwa kwamba huyo Sultan na lineage yake yote walikuwa ni walowezi tu waliojikuta wapo hapa na kunyang'anya kisehemu cha nchi na kukifanya kuwa chao.

Najuwa huu ni mjadala mwingine, sikushawishi nao uujibu.
 
Hao machotara ni kizazi Cha waarabu wa Oman,washirazi wa Iran na muafrika wa visiwani
Lakini bado nina swali, pamoja na jibu zuri la mkuu 'mwajuma' alilonipa hapa, ambalo linafanana pia na lako.

Sasa kwa vile nilishamshukuru mkuu 'mwajuma' kwa kunipa elimu ambayo sikuwa nayo, naogopa kumwendea yeye tena moja kwa moja na kumuuliza hili swali jipya lililoniijia akilini sasa hivi. Naona ni bora nilipitishie kwako, kama una jibu, sawa, na pengine hata 'mwajuma' mwenyewe anaweza kulijibu.

Sutan alikuja hapa, na kuitawala Zanzibar, na kuhamishia makao yake kabisa hapa, na kuoa mswahili, na kuzaa, na watoto nao wakaendelea, wanaoa waswahili wanazaa, n.k.

Je, huyu Sultan aliendelea kuwa mtawala wa Oman, bila shaka kutokana na majibu ya 'mwajuma' ni ndio; na ndiyo sababu pakawepo watawala weusi huko Oman.
Sasa huyu wa mwisho aliyetimuliwa wakati wa Mapinduzi, mbona hakurudi nyumbani kuendelea na utawala wake huko? Au wakati huu Oman na Zanzibar walishagawana himaya, kila mtu na yake?
 
Except hawakunyang'anya, Bali walitengeneza, na kushirikiana na waliowakuta, there is a reason kwa nini wazawa walipigana na wareno, wajeruman na mataifa mengine ila walikuwa hawapigani na waarabu.

Waarabu wengi Tanzania wanaishi vijijini Tena unakuta kijiji kimoja Familia mbili ama Tatu, ilikuwa ni rahisi sana kuwapiga, lakini ukienda kwenye hivyo vijiji unakuta wapo respected sana.
 
Kwa nini isiwe part na parcel ya Kenya!?..maana wapemba wakiwa karibu zaidi na mombasa
Kenya walilaza damu zamani. Kwanza pwani yao yote ile ikiwemo na Mombasa ilikuwa utawala wa Sultan. Tungewasikiliza sana waKenya kuhusu Pemba kama wangeichangamkia wakati huo. Visiwa hivi tungevigawana kati yetu.
 
Mkuu, kuna uzi humu humu JF unaosema, waarabu walipokuja Zanzibar, visiwa hivyo havikuwa na binaadam hata mmoja. Iliwalazimu waarabu wakatafute wafanya kazi ng'ambo ya pili, bara, ndipo pakawepo na watu weusi huko visiwani.

Aaah, yaani unasema waarabu wanajuwa kula na kipofu, au siyo!
 
Kenya walilaza damu zamani. Kwanza pwani yao yote ile ikiwemo na Mombasa ilikuwa utawala wa Sultan. Tungewasikiliza sana waKenya kuhusu Pemba kama wangeichangamkia wakati huo. Visiwa hivi tungevigawana kati yetu.
Zanzibar ni pwani yote ya afrika mashariki,mpaka sofala huko
 
Well said
 
Aliyetimuliwa Zanzibar sidhani Kama alikua akitawala Oman pia kipindi anatimuliwa,zilikua dola mbili,ya Oman na zenji
 
WEWE MGESE UMEWAHI KUMSIKIA RARAGASH historia yake huke Zenj?
Acha kutokwa na povu, wewe chogo tu hata ufanye nini. Chuki na roho mbaya ndio hulka yenu.
Who's RARAGASH!
 
Pole.
 
Sijui kama kuna watu walishashuhudia hili, lakini ngoja niliweke hapa, pengine kwa mara ya KWANZA kabisa.

Zanzibar (mji) ni kama kitongoji (suburb) ya Jiji la Dar es Salaam.

Kama ulishawahi kusafiri kwa ndege usiku, toka Zanzibar kuja Dar, ukiangalia taa za Zanzibar mjini ni kama zimeshikana na zile za Dar. Haichukui muda unatua kwenye mji huo huo ulioondokea!
 
Acha kutokwa na povu, wewe chogo tu hata ufanye nini. Chuki na roho mbaya ndio hulka yenu.
Who's RARAGASH!
Ndio taabu yako hujui historia ya kisiwani ,unaniuliza BARAGASH ni nani? Nenda house of Wonders hapo Stone town ukawaulize eti huyu mwarabu alikuwa anaitwa BARAGASH alikuwa ni nani Zanzibar? Bila shaka watakuelimisha halafu urudi useme alikuwa ni nani!
 
Tatizo letu kubwa tumegawanyika,
Wako wanaofikiri kikristo na wako wanaofikiri kiislam. Tunaofikiri kiasili tumebaki wachache sana.

Wanaofikiri kikristo wanaona Umagharibi ni Bora na kutwa kucha wanavutiwa na Kila cha magharibi kama kuvaa, lugha zao, kula kwao, vitu vyao, na kipimo cha kuendelea Ni kuwa kama wamagharibi.

Wanaofikiri kiislam wanaona Uarabu ni ustaarabu, kujua kiarabu ni kuwa jirani na Mungu. Kuvaa kanzu na barghashia ni kilele cha heshma, etc. Wanajisikia kuwa waarabu.

Tunaofikiri kiasili tunawaona wote hayo makundi mawili ni binadamu sawa na binadamu yeyote duniani. Tunaisoma historia katika jicho la mapambano. Tunaona tunahitaji kupambana zaidi ya kulalamika Kila muda. Tunaangalia fursa kokote.

Kwa ufupi. Siku nyingine nitaandika zaidi
 
Well
 
U.A.E , Oman na wote wa dini ile , huu ni muda wao wa kula nchi, kuanzia kuuziwa Loliondo, Ngorongoro, kupewa ubia wa Bandari bila kuchangia chochote, kupewa ujenzi wa bandari kwa masharti ya mlevi tu ambaye anaweza kuyakubali N.K N.K
Kwani wewe ni wa dini hii iliyopewa jina Na wapagani wa Antokia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…