Ni ipi sababu ya Rais Samia kuwa karibu sana na kuipa uzito Nchi ya Oman?

Namzungumza AMani Karume. Abeid Karume alikua ni muafrika alioa Chotara. Acheni kupotosha historia
Kwani ni kipi nilichopotosha hapo mkuu wangu 'dos.2020? Mimi nimeuliza swali baada ya kutoelewa ulichoandika wewe, halafu sasa unanigeuzia kibao kwamba ninapotosha?

Hawa 'machotara' ndio waarabu wa Oman, au huko Oman kuna waarabu asilia kama zilivyo nchi nyingine za kiarabu? Watu hawataki kulijibu hili swali, sijui kwa nini?
Hebu tusaidie wewe mkuu 'dos.2020, kama unayaelewa vizuri haya mambo.
 
Zanzibar, haijawahi kuwa koloni la Oman au koloni la yeyote, bali mwaka 1732, Sultan Sayyed Said wa Oman, aliihamishia the Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar.

Wakati wa Mkutano wa Berlin kuigawa Africa, Zanzibar haikugawia, iliachwa kwa Sultan of Zanzibar. Hivyo Zanzibar has never been colonized.
P
Na haya unayoyaeleza ndio matamu kabisa.

Kumbe awali na awali kabisa, kabla ya ujio wa hawa wakoloni, wote, akiwemo na huyo Mwarabu Sayyed Said, Zanzibar na Pemba zilikuwa ni part and parcel' ya Tanganyika. Sultan hakuwa na tofauti yoyote na hao wakoloni wengine. Mtu utatokaje huko mbali kote, na kwenda kuweka koloni lako mlangoni kwa mtu mwingine!

Zanzibar will forever be part of Tanzania.
 
Hao machotara ni kizazi Cha waarabu wa Oman,washirazi wa Iran na muafrika wa visiwani
 
Kwa nini isiwe part na parcel ya Kenya!?..maana wapemba wakiwa karibu zaidi na mombasa
 
Mkuu sijui wapi unashindwa kuelewa.

Mwarabu katoka oman kaja Tanzania, kazaa na Mtanzania, mwanae nae kazaa na Mtanzania, mjukuu kazaa na Mtanzania etc hapa damu imechanganyika wee mpaka wanakua weusi, ila ukoo na asili bado ni ya oman, wajukuu na Vitukuu wanarudi oman hali ya kuwa ni weusi na wanapokelewa, na sababu wengine ni lineage ya usultani wanapewa pia Chance ya kuwa watawala. Sijui hapa nimeeleweka?
EeeenHeeee!

Nimekuelewa mkuu. Umejitahidi sana, na kwa kweli niseme wazi, nimekuchukulia kuwa ni mtu mwenye subira.

Sasa baada ya yote haya, uamini wangu wa kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania unazidi kuimarika zaidi, kwani najuwa kwamba huyo Sultan na lineage yake yote walikuwa ni walowezi tu waliojikuta wapo hapa na kunyang'anya kisehemu cha nchi na kukifanya kuwa chao.

Najuwa huu ni mjadala mwingine, sikushawishi nao uujibu.
 
Hao machotara ni kizazi Cha waarabu wa Oman,washirazi wa Iran na muafrika wa visiwani
Lakini bado nina swali, pamoja na jibu zuri la mkuu 'mwajuma' alilonipa hapa, ambalo linafanana pia na lako.

Sasa kwa vile nilishamshukuru mkuu 'mwajuma' kwa kunipa elimu ambayo sikuwa nayo, naogopa kumwendea yeye tena moja kwa moja na kumuuliza hili swali jipya lililoniijia akilini sasa hivi. Naona ni bora nilipitishie kwako, kama una jibu, sawa, na pengine hata 'mwajuma' mwenyewe anaweza kulijibu.

Sutan alikuja hapa, na kuitawala Zanzibar, na kuhamishia makao yake kabisa hapa, na kuoa mswahili, na kuzaa, na watoto nao wakaendelea, wanaoa waswahili wanazaa, n.k.

Je, huyu Sultan aliendelea kuwa mtawala wa Oman, bila shaka kutokana na majibu ya 'mwajuma' ni ndio; na ndiyo sababu pakawepo watawala weusi huko Oman.
Sasa huyu wa mwisho aliyetimuliwa wakati wa Mapinduzi, mbona hakurudi nyumbani kuendelea na utawala wake huko? Au wakati huu Oman na Zanzibar walishagawana himaya, kila mtu na yake?
 
EeeenHeeee!

Nimekuelewa mkuu. Umejitahidi sana, na kwa kweli niseme wazi, nimekuchukulia kuwa ni mtu mwenye subira.

Sasa baada ya yote haya, uamini wangu wa kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania unazidi kuimarika zaidi, kwani najuwa kwamba huyo Sultan na lineage yake yote walikuwa ni walowezi tu waliojikuta wapo hapa na kunyang'anya kisehemu cha nchi na kukifanya kuwa chao.

Najuwa huu ni mjadala mwingine, sikushawishi nao uujibu.
Except hawakunyang'anya, Bali walitengeneza, na kushirikiana na waliowakuta, there is a reason kwa nini wazawa walipigana na wareno, wajeruman na mataifa mengine ila walikuwa hawapigani na waarabu.

Waarabu wengi Tanzania wanaishi vijijini Tena unakuta kijiji kimoja Familia mbili ama Tatu, ilikuwa ni rahisi sana kuwapiga, lakini ukienda kwenye hivyo vijiji unakuta wapo respected sana.
 
Kwa nini isiwe part na parcel ya Kenya!?..maana wapemba wakiwa karibu zaidi na mombasa
Kenya walilaza damu zamani. Kwanza pwani yao yote ile ikiwemo na Mombasa ilikuwa utawala wa Sultan. Tungewasikiliza sana waKenya kuhusu Pemba kama wangeichangamkia wakati huo. Visiwa hivi tungevigawana kati yetu.
 
Except hawakunyang'anya, Bali walitengeneza, na kushirikiana na waliowakuta, there is a reason kwa nini wazawa walipigana na wareno, wajeruman na mataifa mengine ila walikuwa hawapigani na waarabu.

Waarabu wengi Tanzania wanaishi vijijini Tena unakuta kijiji kimoja Familia mbili ama Tatu, ilikuwa ni rahisi sana kuwapiga, lakini ukienda kwenye hivyo vijiji unakuta wapo respected sana.
Mkuu, kuna uzi humu humu JF unaosema, waarabu walipokuja Zanzibar, visiwa hivyo havikuwa na binaadam hata mmoja. Iliwalazimu waarabu wakatafute wafanya kazi ng'ambo ya pili, bara, ndipo pakawepo na watu weusi huko visiwani.

Aaah, yaani unasema waarabu wanajuwa kula na kipofu, au siyo!
 
Kenya walilaza damu zamani. Kwanza pwani yao yote ile ikiwemo na Mombasa ilikuwa utawala wa Sultan. Tungewasikiliza sana waKenya kuhusu Pemba kama wangeichangamkia wakati huo. Visiwa hivi tungevigawana kati yetu.
Zanzibar ni pwani yote ya afrika mashariki,mpaka sofala huko
 
Zanzibar, haijawahi kuwa koloni la Oman au koloni la yeyote, bali mwaka 1732, Sultan Sayyed Said wa Oman, aliihamishia the Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar.

Wakati wa Mkutano wa Berlin kuigawa Africa, Zanzibar haikugawia, iliachwa kwa Sultan of Zanzibar. Hivyo Zanzibar has never been colonized.
P
Well said
 
Lakini bado nina swali, pamoja na jibu zuri la mkuu 'mwajuma' alilonipa hapa, ambalo linafanana pia na lako.

Sasa kwa vile nilishamshukuru mkuu 'mwajuma' kwa kunipa elimu ambayo sikuwa nayo, naogopa kumwendea yeye tena moja kwa moja na kumuuliza hili swali jipya lililoniijia akilini sasa hivi. Naona ni bora nilipitishie kwako, kama una jibu, sawa, na pengine hata 'mwajuma' mwenyewe anaweza kulijibu.

Sutan alikuja hapa, na kuitawala Zanzibar, na kuhamishia makao yake kabisa hapa, na kuoa mswahili, na kuzaa, na watoto nao wakaendelea, wanaoa waswahili wanazaa, n.k.

Je, huyu Sultan aliendelea kuwa mtawala wa Oman, bila shaka kutokana na majibu ya 'mwajuma' ni ndio; na ndiyo sababu pakawepo watawala weusi huko Oman.
Sasa huyu wa mwisho aliyetimuliwa wakati wa Mapinduzi, mbona hakurudi nyumbani kuendelea na utawala wake huko? Au wakati huu Oman na Zanzibar walishagawana himaya, kila mtu na yake?
Aliyetimuliwa Zanzibar sidhani Kama alikua akitawala Oman pia kipindi anatimuliwa,zilikua dola mbili,ya Oman na zenji
 
WEWE MGESE UMEWAHI KUMSIKIA RARAGASH historia yake huke Zenj?
Acha kutokwa na povu, wewe chogo tu hata ufanye nini. Chuki na roho mbaya ndio hulka yenu.
Who's RARAGASH!
 
Sio kweli, usiwadanganye watu. Oman haina undugu wala asili ya Zanzibar. Walikuwa watawala tu walioitawala Unguja na Pemba ( Wakoloni ) kama watawala wengine. Watu wa Unguja na Pemba walienda Oman kufanya kazi wakaloea wakabaki huko na sasa wanajiita Waarabu wa Oman kumbe ni Waunguja na wa Wapemba na hawana asili za Ki Arabu Kabisa!

Asili ya wa Unguja na wa Pemba ni " MIJIKENDA" na SIO WAARABU! acheni kujikweza kutafuta naswaba nyiingi.....

Na hao wanaojiita wa Oman wanawasaidia ndugu zao sio wa Oman ila ni hao Waunguja na Wapemba waliolowea / walioshi huko hao ndio ndugu zao waliowaacha huko visiwani.

Kwa taarifa zenu tu Waarabu Wenyewe Oman huwaita "ZINJIBARI" wanawajua hao ni Wazanzibari kutoka Zanzibar na sio Waarabu.

Acheni kuwadanganya watu!

Mkataa kwao..............

Sent from my P00C using JamiiForums mobile app
Pole.
 
Zanzibar, haijawahi kuwa koloni la Oman au koloni la yeyote, bali mwaka 1732, Sultan Sayyed Said wa Oman, aliihamishia the Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar.

Wakati wa Mkutano wa Berlin kuigawa Africa, Zanzibar haikugawia, iliachwa kwa Sultan of Zanzibar. Hivyo Zanzibar has never been colonized.
P
Sijui kama kuna watu walishashuhudia hili, lakini ngoja niliweke hapa, pengine kwa mara ya KWANZA kabisa.

Zanzibar (mji) ni kama kitongoji (suburb) ya Jiji la Dar es Salaam.

Kama ulishawahi kusafiri kwa ndege usiku, toka Zanzibar kuja Dar, ukiangalia taa za Zanzibar mjini ni kama zimeshikana na zile za Dar. Haichukui muda unatua kwenye mji huo huo ulioondokea!
 
Acha kutokwa na povu, wewe chogo tu hata ufanye nini. Chuki na roho mbaya ndio hulka yenu.
Who's RARAGASH!
Ndio taabu yako hujui historia ya kisiwani ,unaniuliza BARAGASH ni nani? Nenda house of Wonders hapo Stone town ukawaulize eti huyu mwarabu alikuwa anaitwa BARAGASH alikuwa ni nani Zanzibar? Bila shaka watakuelimisha halafu urudi useme alikuwa ni nani!
 
Yaani wabongo bhana.... mbona kutwa tukiisifia USA, UK na nchi nyingi za Ulaya ambazo zilikuwa ni Wakoloni wetu na hatuoni shida????

Haya makengeza mpaka kwenye kufikiri yatatulemaza akili zetu....

Leo hii huwezi kuta familia hapa Tanzania zenye mchanganyiko wa damu kati ya wazawa na Wajerumani au Waingereza meaning walituchukulia kama watumwa na daraja la pili kwao... lakini kwa upande wa Oman ni tofauti meaning wanawaona Zanzibar kama sehemu ya ndugu zao....

KUNA UBAYA GANI WAKISHIRIKI KUWEKEZA HUMU NA KUIMARISHA MASHIRIKIANO YA KIUCHUMI?

TUACHE KUFIKIRI KINYUMENYUME JAMANI...

Oman yenye watu chini ya 10M wanaweza kweli to Overdue the Country of more than 60M? Tutakuwa mazombi siyo bure.
Tatizo letu kubwa tumegawanyika,
Wako wanaofikiri kikristo na wako wanaofikiri kiislam. Tunaofikiri kiasili tumebaki wachache sana.

Wanaofikiri kikristo wanaona Umagharibi ni Bora na kutwa kucha wanavutiwa na Kila cha magharibi kama kuvaa, lugha zao, kula kwao, vitu vyao, na kipimo cha kuendelea Ni kuwa kama wamagharibi.

Wanaofikiri kiislam wanaona Uarabu ni ustaarabu, kujua kiarabu ni kuwa jirani na Mungu. Kuvaa kanzu na barghashia ni kilele cha heshma, etc. Wanajisikia kuwa waarabu.

Tunaofikiri kiasili tunawaona wote hayo makundi mawili ni binadamu sawa na binadamu yeyote duniani. Tunaisoma historia katika jicho la mapambano. Tunaona tunahitaji kupambana zaidi ya kulalamika Kila muda. Tunaangalia fursa kokote.

Kwa ufupi. Siku nyingine nitaandika zaidi
 
Well
 
U.A.E , Oman na wote wa dini ile , huu ni muda wao wa kula nchi, kuanzia kuuziwa Loliondo, Ngorongoro, kupewa ubia wa Bandari bila kuchangia chochote, kupewa ujenzi wa bandari kwa masharti ya mlevi tu ambaye anaweza kuyakubali N.K N.K
Kwani wewe ni wa dini hii iliyopewa jina Na wapagani wa Antokia?
 
Back
Top Bottom