Mtambachuo
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 2,919
- 5,558
Rekebisha kichwa cha Uzi wako,hawajawaacha kwa mbali kama ulivyoandika kwa sababu hakuna official figures zozote zinazoonyesha orodha za utajiri wa makabila mbalimbali isipokuwa huwa tunabuni tu,nikiandika hivi sijadharau juhudi za wachaga katika kuchakalika kukuza uchumi wao,wako vizuri sana,ila tu ni hicho kichwa cha Uzi umekiandika ili kupata wasomaji wengi yaani "click bait".
Namwona shirima na macha
Soko la hisa siyo kiashiria pekee cha Kujua kwamba kabila gani limewaacha mbali makabila mengine kiutajiri au kiuchumi,ukizingatia kua DSE Bado ni soko changa sana,Wala hata hisa zake huwa hazijawahi kupanda bei kiasi cha watu kuuziana hisa yaani hapo watu wamestick wanasuburia gawiwo la mwisho wa mwaka😁,yaani Bado sana.Hakuna haja ya figure mzee mambo kwa ushahidi si yanaonekana tunapozunguka huko Muleba, Shinyanga, Kyela na kwingineko. Wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani.
Pia angalia list ya matajiri wa soko la hisa la Dar es Salaam utuambie ukiachana na hao Waasia ni kabila gani lina ongoza
Soko la hisa siyo kiashiria pekee cha Kujua kwamba kabila gani limewaacha mbali makabila mengine kiutajiri au kiuchumi,ukizingatia kua DSE Bado ni soko changa sana,Wala hata hisa zake huwa hazijawahi kupanda bei kiasi cha watu kuuziana hisa yaani hapo watu wamestick wanasuburia gawiwo la mwisho wa mwaka😁,yaani Bado sana.
Kuna makabila Yana utajiri mkubwa hapa Tanzania ila hayajionyeshi,nadhani kwa sababu wanamiliki biashara ambazo hazina umaarufu,ila utawagundua utajiri wao siku wanapoamua kumleta bibi harusi wao kwenye harusi kwa kutumia helicopter 🚁.
Sijadharau soko la hisa ila nimesema hicho siyo kigezo cha kupimia uchumi wa watanzania.
Sidhani kama uwekezaji wa soko la hisa la Dar ni kigezo kikubwa.Ni kigezo moja wapo. Huo ni uwekezaji.
We kibwengo km ni mchaga acha kudanganya wasiwajua, uchagani kuna umaskini mkali sana, shule zilijengwa na wamisionari, tofauti ya wachaga na makabila mengine ni sifa za kupenda sifa za kijinga. Wachaga wanaomiliki hasa mali km mali ni wachache sana, wana mali gani? Hawana ardhi, hawafugi, hawavui samaki wengi ni vibiashra vidogo vidogo tu.Licha ya umasikini wetu wa taifa hapakosekani kundi la watu wenye nafuu, hata kwenye ukoo masikini wale wenye magari hutokea koo maskini ila wao kama wao wapo mbali kuzidi wenzao, Tukigusia makabila yenye asili ya hapa kwetu, wachaga wapo mbali mno, yapo makabila yanayofatia ila ni gepu refu mno.
1.Elimu: Hawa watu wamesoma sana na shule zipo huko kwao tangu zamani sana, shule zipo nyingi zimejengwa vizuri hakuna mambo ya wanafunzi kurundikana madarasan ama kukaa chini, walishamaliza haya matatizo tangu zamani. Mwamko huu wa elimu umepelekea kuwepo shule nyingi za kimataifa Moshi na Arusha, matajiri wanapeleka watoto shule hizi hawaoni shida kulipia ada milioni 40, shule hizi ni kama international school of Moshi, Braeburn, Kennedy house, St Constantine, n.k. ni shule zenye mfumo moja duniani na hata matajiri na wanasiasa wa nchi za ulaya husomeshea watoto, kuna comnections nzito na expoosure,.... hapa kwenye elimu wanaokaribia labda wahaya lakini tatizo wahaya wanakomaa kusoma tu Ila mchaga anasoma, anatafuta pesa, hasahau kwao na hata akipata hajigambi wala kuridhika.
Biashara - Ni wakongwe katika hii sekta, biashara ipo ndani ya damu, hata walioishia darasa la saba wanafanya makubwa, wasomi nao maarufu tumeona wakileta makampuni ya ndege, media house, kampuni za kuwachota pesa wazungu waje kutalii, n.k. ukicheki hata soko la hisa DSE watanzania wa asili wapo wachache ila wachaga ndio wengi. sikuhizi naona kuna makabila mengine yamepata mwamko kama wakinga, waha, wasukuma n.k ila kwakweli bado gepu ni refu, wameachwa mbali sana na wachaga.
siasa - Siasa pia ipo ndani ya damu, nikueleze tu ya kwamba hata vyama vingi maarufu vya upinzani vilianzia huko, TLP, NCCR, CHADEMA, n.k.
kuendeleza na kujenga vijijini kwao hawana mpinzani, Ni sehemu yenye vijiji vyenye makazi bora ya nyumba nzuri na za kisasa, wengi wakistaafu hurudi kuishi huku bila shida. maji Safi ya bomba yapo, barabara zipo, hospitali zipo, umeme upo, n.k. Kama ilivyo kwa Moshi kuwa mojawapo ya miji Safi miaka n'a miaka, vijijin pia makazi yamepamgiliwa vizuri kwa usafi wa hali ya juu. nimeona makabila mengine wanajaribu lakini tatizo unakuta hata mtu akijenga kijijini kwao, nyumba nzuri bado inaweza kuwa moja ama zinahesabika kijiji kizima, na hapo kuna shida ya maji inabidi wachimbe kisima, umeme watumie jenereta, barabara mbovu, n.k. Hali hii hupelekea hata waliojenga vijijini wakistaafu wanabaki mjini, ila pia wengi huogopa kujenga ama hata wakijenga wanasita kwenda kuishi vijijini kwasababu ya uchawi, Nina rafiki yangu wa Geita huko wazazi wake walikataa awajengee nyumba ya kisasa kwa kuogopa kuwatia ndugu na majirani zao wivu wasije wakarogwa ama wamroge mtoto wao, mtu anaweza kujenga huko kibishi lakini ni ile ijulikane tu kajenga kwao ila hapendi kukaa huko labda itokee msiba ama dharura.
Kwenye hizi nafasi za Teuzi hawajajaa sana maana hizi nafasi kwa kiasi kikubwa ni Raisi anateua watu wake ila ukija huku kwenye ajira za ofisini wamejaa, mashirika ya uma na kimataifa wapo.
kuridhika kwa wachaga ni ngumu sana, mtu alieridhika mara nyingi huonyesha majigambo, ujivuni, kiburi, sifa, n.k. anaona ndio ashafika, ataanza kuiita laki si pesa hadharani, dharau, sifa za kutaka attention watu wajue ana hela, n.k kwa wachaga mtu anaweza kuwa na pesa kibao ila hizi tabia hawaendekezi.
Ni nadra sana kusikia mambo ya uchawi uchagani kama ilivyo umasaini na ukuryani, simaanishi kwamba haupo kabisaaaa ila ni kwa kiwango kidogo sana, si jambo la kusumbua sana jamii kwamba flani kamtupia jini jirani kisa kapata kazi, kurogana kisa mtu kanunua baiskeli, kutupiana mabusha, malimbwata, kuwanga usiku, n.k. ukisikia mganga mchaga, mmasai au mkurya kimbia, huyo tapeli tu, huku mtu akitaka uchawi afunge safari kwenda kununua kwengine, sehem ya karibu upareni.
Wanaheshimu mila na desturi zao: kifupi wanajua wapi wametoka na wapi wanaenda, wachaga ikifika december kuna mtu asiejua balaa lao ? huwa ni kama waisrael wa nchi mbali mbali wanarudi kwao, Kama ilivyo utamaduni wa kila kabila matambiko hayawezi kukosekana kwa zile koo za kichifu.
..........................
Hawa Jamaa ndio mana walipata Sana Platform ya kuwa Kwenye Vyombo vya Usalama especially teethSehemu yenye shule nyingi Tanzania ni Iringa
Sidhani kama uwekezaji wa soko la hisa la Dar ni kigezo kikubwa.
Generation pia inachange sana miaka ya nyuma tulikuwa hatuwasikii Wakinga Wasukuma na Waha kwenye biashara na Uwekezaji lakini saizi ni jamii zinazofanya vizuri sana pia.
Kuna jamii zimewekeza kwenye kilimo,madini na ufugaji uwekezaji ambao si rahisi kuuona maana uko maeneo ya vijijini mashambni.
We kibwengo km ni mchaga acha kudanganya wasiwajua, uchagani kuna umaskini mkali sana, shule zilijengwa na wamisionari, tofauti ya wachaga na makabila mengine ni sifa za kupenda sifa za kijinga. Wachaga wanaomiliki hasa mali km mali ni wachache sana, wana mali gani? Hawana ardhi, hawafugi, hawavui samaki wengi ni vibiashra vidogo vidogo tu.
Kuna makabila yana mali wametulia tu hawana visifa vya kijinga. Tulieni acheni ukabila, wachaga kwao ni maskini ndiyo maana wamekimbia kwao na kuishi km wahamiaji. Km wachaga ni matajiri Moshi leo ingekuwa jiji tena kubwa, ila imedumaa kwani uchagani hakuna mali, purchasing capacity ya wachaga ni ndogo sana ndio maana wamekimbia kwao.
Hawa Jamaa ndio mana walipata Sana Platform ya kuwa Kwenye Vyombo vya Usalama especially teeth
Usijidanganye kaka dunia hii haijasimqma na hakuna kusema Kabila fulani litaongoza miaka yote.Jamaa wewe unaonakana una stress katafute matibabu. Na punguza chuki kwa Wachagga. Kama hayo makabila mengine yangekuwa na mali si tungeziona.
Usijidanganye kaka dunia hii haijasimqma na hakuna kusema Kabila fulani litaongoza miaka yote.
Ukijaribu kutizama hata historia inakwambia Uingereza ilitawala nchi mbalimbali ila saizi inapambana na nchi kama South Korea,China au Singapore.
Hao Wachaga tuambie hapa wana miliki nini ambacho Mkinga, Msukuma,Mhaya na makabila mengine wapambanaji hana kwa sasa?
Je sekta ipi Mchaga ameishika? Je ni biashara? Kilimo?, Ufugaji? Madini? Tekinolojia?
Kama hakuna kitu hapo juu anaongoza basi ni kuwa wanafanya biashara za kawaida tu kama jamii zingine.
Way back ni kweli maduka mengi walikuwa wao na Wahindi jambo ambalo halipo kwa sasa na majira hameshabadilika kutokana na elimu na Tekinolojia tuliyopo.
Hizo ni story tu, kama ni kutawala wakoloni basi kuna sehemu walienda mapema kabla ya uchagani.siri iko hapa,
wajerumani walitawala maeneo ya kilimanjaro mapema sana kuanzia 1885, hivyo wachaga walikua ni moja kati ya makabila ya kwanza kabisa kuchangamana na watu weupe tanzania bara....
shughuli la kiuchumi na ile elimu ya kikoloni kwa wale wachaga wa tabaka la juu ndo ikapelekea wao kujanjaruka haraka kuliko makabila mengine....