Ni ipi siri ya Wachaga kuwa kabila lililoyaacha makabila mengine mbali mno kwenye mafanikio?

Ni ipi siri ya Wachaga kuwa kabila lililoyaacha makabila mengine mbali mno kwenye mafanikio?

Endelea kujidanganya! Huko Moshi kuna maajabu gani? Mbona Wachaga tuko nao mtaani ni choka mbaya tu! Wenye mafanikio wapo hasa wale wazee wao wa zamani ila hawa wachaga wa sasa mimi nakukatalia!
Jamii nyingi sana zinafanikiwa katika sekta za biashara kama unavoweza kuona Wakinga,Waha,Wasukuma,Wakurya nk!
Kubaki na idea ya miaka ya 90 mimi natakaa maana unaposema gepu kubwa katika sekta gani? Maana hata vyuoni makabila yote yapo,kwenye biashara makabla mengine pia yanafanya vizuri,Madini , Kilimo kote huko Makabila yote yanafanya vizuri kwa level ya nchi yetu!
Sasa km nyie wengine mmekimbia kwenu na hamtaki kupasikia wala kurudi kwa nini mkasirikie maendeleo ya watu wanaowekeza kwao?
Mkifika Mjini hamtaki kusikia tena habari za huko kwenu simiyu 😁
 
Sasa km nyie wengine mmekimbia kwenu na hamtaki kupasikia wala kurudi kwa nini mkasirikie maendeleo ya watu wanaowekeza kwao?
Mkifika Mjini hamtaki kusikia tena habari za huko kwenu simiyu 😁
Hahaha hakuna mtu aliyekimbia kwao! Mfano Wakinga wanapaendeleza kwao Njombe pia Wasukuma huko kanda ya ziwa kama Kahama,Mwanza na Geita pia Wakurya hawaajapakimbia Tarime ndo maana kuna maendeleo sehemu hizo!
Labda kwa upande wa Waha ndo unaweza kusema hawarudi kwao ila hayo makabila mengine yanarudi kwo kwa sana tu!
Ukitaka kujua nenda Airport au Magufuli Terminal hapo uone watu wanavyosafiri kwenda Mbeya,Mwanza na maeneo mengine!
 
Ila hizi takwimu zenu zitakuja kutuua, Iringa Ni ya pili kwa kipato kikubwa kwa mtu mmoja baada ya Dar, hio Iringa tena inaongoza kwa utapia mlo!!!!!

Kitengo Cha takwimu, kibinafsishwe!!! Wapewe DP World
wanaoongoza kufanya takwimu ni maprofesa!! na maprofesa wengi akili zao wanazijua wenyewe,kama wamedata flani ivi,,ndo manake haukuna taifa ata moja linaongozwa na profesa,,,dunia nzima hamna!!!!!!!!,,,,,,,,ata madikteta wengi ni wale waliosomea sayansi{ata kama hawajafika ngazi ya profesa]..............wao ni wa2 wa princple tu!!!!!...da!!!!! ghafla nimemkumbuka mzee MAGU!!!
 
Licha ya umasikini wetu wa taifa hapakosekani kundi la watu wenye nafuu, hata kwenye ukoo masikini wale wenye magari hutokea koo maskini ila wao kama wao wapo mbali kuzidi wenzao, Tukigusia makabila yenye asili ya hapa kwetu, wachaga wapo mbali mno, yapo makabila yanayofatia ila ni gepu refu mno.

1.Elimu: Hawa watu wamesoma sana na shule zipo huko kwao tangu zamani sana, shule zipo nyingi zimejengwa vizuri hakuna mambo ya wanafunzi kurundikana madarasan ama kukaa chini, walishamaliza haya matatizo tangu zamani. Mwamko huu wa elimu umepelekea kuwepo shule nyingi za kimataifa Moshi na Arusha, matajiri wanapeleka watoto shule hizi hawaoni shida kulipia ada milioni 40, shule hizi ni kama international school of Moshi, Braeburn, Kennedy house, St Constantine, n.k. ni shule zenye mfumo moja duniani na hata matajiri na wanasiasa wa nchi za ulaya husomeshea watoto, kuna comnections nzito na expoosure,.... hapa kwenye elimu wanaokaribia labda wahaya lakini tatizo wahaya wanakomaa kusoma tu Ila mchaga anasoma, anatafuta pesa, hasahau kwao na hata akipata hajigambi wala kuridhika.

Biashara - Ni wakongwe katika hii sekta, biashara ipo ndani ya damu, hata walioishia darasa la saba wanafanya makubwa, wasomi nao maarufu tumeona wakileta makampuni ya ndege, media house, kampuni za kuwachota pesa wazungu waje kutalii, n.k. ukicheki hata soko la hisa DSE watanzania wa asili wapo wachache ila wachaga ndio wengi. sikuhizi naona kuna makabila mengine yamepata mwamko kama wakinga, waha, wasukuma n.k ila kwakweli bado gepu ni refu, wameachwa mbali sana na wachaga.

siasa - Siasa pia ipo ndani ya damu, nikueleze tu ya kwamba hata vyama vingi maarufu vya upinzani vilianzia huko, TLP, NCCR, CHADEMA, n.k.

kuendeleza na kujenga vijijini kwao hawana mpinzani, Ni sehemu yenye vijiji vyenye makazi bora ya nyumba nzuri na za kisasa, wengi wakistaafu hurudi kuishi huku bila shida. maji Safi ya bomba yapo, barabara zipo, hospitali zipo, umeme upo, n.k. Kama ilivyo kwa Moshi kuwa mojawapo ya miji Safi miaka n'a miaka, vijijin pia makazi yamepamgiliwa vizuri kwa usafi wa hali ya juu. nimeona makabila mengine wanajaribu lakini tatizo unakuta hata mtu akijenga kijijini kwao, nyumba nzuri bado inaweza kuwa moja ama zinahesabika kijiji kizima, na hapo kuna shida ya maji inabidi wachimbe kisima, umeme watumie jenereta, barabara mbovu, n.k. Hali hii hupelekea hata waliojenga vijijini wakistaafu wanabaki mjini, ila pia wengi huogopa kujenga ama hata wakijenga wanasita kwenda kuishi vijijini kwasababu ya uchawi, Nina rafiki yangu wa Geita huko wazazi wake walikataa awajengee nyumba ya kisasa kwa kuogopa kuwatia ndugu na majirani zao wivu wasije wakarogwa ama wamroge mtoto wao, mtu anaweza kujenga huko kibishi lakini ni ile ijulikane tu kajenga kwao ila hapendi kukaa huko labda itokee msiba ama dharura.

Kwenye hizi nafasi za Teuzi hawajajaa sana maana hizi nafasi kwa kiasi kikubwa ni Raisi anateua watu wake ila ukija huku kwenye ajira za ofisini wamejaa, mashirika ya uma na kimataifa wapo.

kuridhika kwa wachaga ni ngumu sana, mtu alieridhika mara nyingi huonyesha majigambo, ujivuni, kiburi, sifa, n.k. anaona ndio ashafika, ataanza kuiita laki si pesa hadharani, dharau, sifa za kutaka attention watu wajue ana hela, n.k kwa wachaga mtu anaweza kuwa na pesa kibao ila hizi tabia hawaendekezi.

Ni nadra sana kusikia mambo ya uchawi uchagani kama ilivyo umasaini na ukuryani, simaanishi kwamba haupo kabisaaaa ila ni kwa kiwango kidogo sana, si jambo la kusumbua sana jamii kwamba flani kamtupia jini jirani kisa kapata kazi, kurogana kisa mtu kanunua baiskeli, kutupiana mabusha, malimbwata, kuwanga usiku, n.k. ukisikia mganga mchaga, mmasai au mkurya kimbia, huyo tapeli tu, huku mtu akitaka uchawi afunge safari kwenda kununua kwengine, sehem ya karibu upareni.

Wanaheshimu mila na desturi zao: kifupi wanajua wapi wametoka na wapi wanaenda, wachaga ikifika december kuna mtu asiejua balaa lao ? huwa ni kama waisrael wa nchi mbali mbali wanarudi kwao, Kama ilivyo utamaduni wa kila kabila matambiko hayawezi kukosekana kwa zile koo za kichifu.
..........................
Vyema sana ila Nyerere aliwarudisha nyuma mno sijui atawalipa fidia gani?
 
Moshi bado sana! Maana mji huu ni?mongering lakini bado sana kiukuaji na unazidiwa na Kahama ambayo ni makao makuu ya wilaya!
Ukikatiza Moshi kuelekea Arusha bila kuingia ndani utabaki unajiuliza hivi hiyo moshi ipo wapi? Moshi ni pana mno na ipo zaidi huko milimani. Tembea zaidi uone.
 
Acha uongo mji unajieleza bhana!
ni mji wa kawaida ila kwa vile wapenda sifa Mnasumbuliwa sana!
Ukikatiza Moshi kuelekea Arusha bila kuingia ndani utabaki unajiuliza hivi hiyo moshi ipo wapi? Moshi ni pana mno na ipo zaidi huko milimani. Tembea zaidi uone.
 
ENEO PEKEE WALILOSHINDWA KUFANIKIWA, NI KWENYE NDOA.

NDOA ZAO HAZIDUMU KABISAA.

MAENEO MENGINE WAKO VIZURI
iko hivi,wakati hawa jamaa wakiwa ktk harakati zao za kutafuta utajiri,hawapendi kuumizwa kichwa na m2 yoyote,ndo manake wanapendi kwenda kutafuta pesa mbali na nyumbani kwao,ili kukwepa kero za ndugu{ndugu ni moja ya chanzo kikubwa cha umasikini},,,sasa iko ivi,kama ujuavyo wakati wa uchumba wanawake huwa wanaficha makucha yao,lakini wakishaolewa tu hukunjua makucha yao{sio wote ila ni wengi,na wale ambao wanaficha kucha zao wana tatizo la wivu ambalo nalo ni chanzo cha umasikini,kwani jamaa akirudi usiku kwa ajili ya utafutaji anakutana na maneno},,sasa kinachotokea,jamaa anamprint mkewe chapchap,alaf anamwachia nyumba na vilivyomo anaenda mbali nae na haoi tena,ni kutafuta mikwanja mpaka anakuwa don ndo anakumbuka familia yake na kuirejea,na kipindi chote hicho anatuma mapene kwa famlia yake,ukitaka kujua hilo nenda huko milimani utakuta wanawake kibao wa kichagga wametelekzwa[ni maelekzo wanayofundishwa wakati wa jando,kumbuka jamaa wanatahiriwa wakishabalehe ili somo liingie kichwani,ingawa siku izi hali inabadilika kidogo}
 
Discipline ya maisha kwa wachagga huanzia kwa watoto, malezi juu ya nidhamu pesa, elimu na uvumilivu wakati wa utafutaji huanzia mbali sana, haya malezi huwa na impact kubwa mbele ya safari.

Watoto wa kichagga huwa hawadekezwi kwa kiwango kikubwa, watoto wa kichagga huwa hawaachwi na baba zao, au kutelekezwa hii ina umuhimu sana kwenye ukuaji wao, ndio maana si rahisi sana kukuta mtoto wa kichagga anaranda mtaani.

Jamii nyingine inabd zijifunze kupitia hapo, kitu kingine familia zisiwe na ubinafsi wa maendeleo kwa ndugu zao,

Sababu zipo nyingi, lakini zaidi ya hapo ni asili pia imechangia
 
Wachaga wako kama wahindi, wanaharibu watoto wao, utakuta mmoja dishi limeyumba huwezi kumjua kirahisi...

Huyo ndio anawapa utajiri...

Kingine ni watu wa kafara za damu za wanyama kwa wafu/mizimu...
Total lie, sijawahi ona hii kitu, acha kupambana ukijipa moyo maendeleo yanaletwa na upaka shume bata wahedi
 
Kule mtoto wa mwenzio akifaulu mitihani jamii yote inafurahia,

Mtoto wa jirani akinunua gari au kujenga ni furaha kwa jamii nzima na fahari ya wote,

Lakini njoo huku kwingine uone ni kinyume chake [emoji108]

Tena unakuta hadi ndugu wa tumbo moja wanamroga ndugu yao [emoji24]
Na hata ukirudi nyumbani na chuma yako, unaalika majirani, na jamaa mnakaa pamoja kuria kitochi, sehemu nyingine ukishika pesa huwezi thubutu kurudi hata nyumbani, hayo maendeleo yatakujaje kijijini
 
Back
Top Bottom