Nilimtapel polisi 350 nikiwa kidato cha kwanza
Story yenyewe ipo hivi mimi nilikuwa nasoma shule ambayo lazima nipande magari mawili.
Yaaani moja kutoka home mpaka town na lingine town mapaka shule.
Kwa mnaoijua mwanza ilikuwa natoka igoma mpaka kirumba kabla ya hizi route za siku hiz za kuunganisha.
Bas siku moja moja kama sina nauli wakati wa kurudi(nilikuwa nakula mpaka naishiwa) inabidi nitembee kutoka kirumba mpaka mjini then nikifika mjin nakutana na makondakta wa mtaani wananibeba bure.
Sasa siku hiyo natembea mdogo mdogo nikapita mtaa wa liberty kuna benki ya NBC miaka hiyo alikuwepo askari mmoja nilikuwa namuona kila siku na alikuwa anaogopeka akaniita.
Nikasita kwa kile kiburi cha balehe ila nikasema poa wacha niende.
Kwa sauti ya kibabe akanipa 350/- nimchukulie sigara nakumbuka alinituma embassy
Nikaenda duka ambalo anaweza kuniona nikakosa nikarud kumwambi akasema nenda lile na pale pia alikuwa anaweza kiniona nikakosa.
Nikarudi kumwambia hakuna akaniambia kachukue pale kwenye kona.
Ha ha ha nadhani alijuta sana siki hiyo nilivyopiga kona tu sikuangalia nyuma bahati nzuri nikakutana na gari nikapanda huyoooooo
Sikupita mwaka mzima ile njia