Mi nakumbuka miaka ya 1992/93 pale
hospitali ya meta mkoani mbeya kulikuwa
na pori almaarufu forest.
na kulikuwa na kituo cha mabasi yanayoelekea
mwanjerwa yakitokea mbalizi.
Siku moja tukiwa kwenye basi na mdogo wangu
Binti mmoja aliporwa kitenge alichodai aliagizwa
na mzazi wake akanunue.Wale waporaji wakikimbilia mstuni.
Na pale barabarani walikuwa wanakaa wahuni
ambao walijifanya wasamaria wema kumsaidia
yule dada kuwafukuza waporaji wakatokomea mstuni wakijidai kumsaidia.
Abiria kwenye gari walijitahidi kumuita yule
dada asiwafuate wale wahuni kwani wangemdhuru
yule dada hakutaka kumsikiliza mtu
aliendelea kulia na kuwafuata wale vijana
waliojifanya wanamsaidia.
Mimi roho yangu iliuma sana,nikamwambia mdogo
wangu tushuke ili walau tumsihi yule dada arudi asije akadhurika.
Tulishuka tukaacha lile basi likiendelea na safari.
Pia kuna baba mmoja na kijana mmoja
walishuka kuungana nasi kumnusuru yule dada.
Yule baba tulimuacha kwani tulikuwa tunakimbia mbio.
Tulifanikiwa kumkuta yule dada akiwa peke yake,
lakini akizidi kupiga mbio kuwafuata wale vijana.
tulimsihi arudi ila hakutaka kutusikiliza
akidai mama yake atamuua.Tulizidi kujisikia vibaya
ikabidi tuungane naye kuwasaka.
Kwa bahati tuliwaona kwa mbali msituni bondeni
wameishakuwa kitu kimoja,ila yule mporaji
tulikariri rangi ya nguo yake.
Tuligawanyika ili kuwazunguka,mimi nikapitia
upande wa mbele walikokuwa wanaelekea
na mdogo wangu na yule kijana mwingine waliwaendea kwa nyuma.
Nilifanikiwa kuwawahi kule mbele na nikatunga stori
ya kuwachelewesha ili wenzangu wafike.
Niliwaambia nimepotelewa na ng'ombe wangu
nikawaauliza kama wameishawaona.
Nikiwa nawaelezea stori hiyo,yule dada akajitokeza
kwenye zile barabara za forest kwa mbali wakamuona
wakaamua kutimua mbio,ila wakawawameishaogopa
wakaacha ndala zao ili kujiokoa.
Nilijitahidi kumkamata mmojawapo
akawa ananitishia kunichoma kisu,lakini
akaniponyoka na akanizidi mbio.Kwa bahati
wale wenzangu wakamtia mbaroni yule
mwenye kitenge wakati anajaribu kunikimbia mimi
akapitia kule walikokuwa wanatokea,wakafanikiwa
kumnyanganya kile kitenge.
Wale vibaka walipanic wakidhani lile
pori lilikuwa limejaa watu wanaowatafuta
kumbe tulikuwa watatu na yule binti tu.
Tulifanikiwa kumrudishia yule binti
kitenge chake,na ndala za wale vibaka kama ushahidi
wa yaliyotokea.Kwa kweli tulifurahi
ila nikikumbukaga hii stori huwa najiuliza huo ujasiri
sijui ulitoka wapi ukizingatia hilo eneo miaka hiyo
majambazi yalikuwa yanaua watu.
Nawapongeza wote tulioshirikiana,na hasa
yule kijana mwingine na yule baba
kama nao wapo humu jf nawapa big up sana
kupitia uzi huu.