Ni Jambo gani la ujasiri sana uliwahi kufanya mpaka leo ukikumbuka unafurahia na kujiona mwamba...

Mimi mpaka kesho najiona jasiri mno maana nikikumbuka niliyopitia Nina kila sababu zakujiona jasiri

Iko hivi mwaka 2013 nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho udom nilidisco, hakuna kipindi kigumu ambacho nimewahi pitia kwenye maish yangu kama hiki kiukwel mpaka kesho huwa sijuagi kwanini lile jambo lilitokea

Sina historia ya kufail maisha yangu yote nimekuwa na performance nzuri sana tangu primary school mpaka chuo ila nikiwa first year nilipata sup somo moja, nilicarry ilo somo mana sikupenda nipate kalai hapo ndipo balaa lilipoanza sitokaa nisahahu mana tangu nicarry lile somo matokeo yakitoka kwangu empty fatilia jamaa hawakuwa serious kabisa na maisha yetu wanapiga danadana na Mimi nikaona ah kwasababu huyu ndo mwalimu wa somo na ni HOD atarekebisha mana ndo zilikuwa story zake hizo mwaka wa pili ukakatika fresh matokeo yangu yanapendeza,mwaka wa tatu pia ukakatika matokeo fresh ikumbukwe iyo ndo ilikuwa sup pekee ambayo niliwahi ipata na GPA yangu ilikuwa kubwa mno japo nilikuwa Nina kimeo,

Nikiwa home nasubiri confirm graduation naangalia matokeo bado ikabidi nirudi kwa jamaa namwambia anasema aah mbona fresh nenda nakuwekea matokea ndugu zangu naomba kusema nilichokutana nacho mungu ndo anajua mpaka Leo ninaishi ni kwa neema na upendo wake mana ilifika mahali nilitamani nijiue kabisa sikuwa waza kama itakuja tokea siku nikapata pigo kubwa kama lile nilikata tamaa kabisa nikiangalia rafiki zangu, wazazi wangu nilikuwa nawaza kuanza maisha sasa badala yake nikawaza ntaanzaje upya tumaini likapotea nikadhoofika mwili vidonda vya tumbo,pressure nikawa naumwa kila nikienda Pima naonekana sina tatizo nyumbani hapakukalika kabisa

Mungu ni mwaminifu mama yangu alinitia moyo sana hakuniacha kabisa yeye ndio MTU pekee ambaye aliniami na mpaka kesho ananiamini,simlaumu baba yangu kwa hasira alizokuwa nazo juu yangu kwa sababu naelewa maumivu aliyoyapata gharama alizopoteza Leo nakuja muaibisha kiashi kile hali ilikuwa mbaya wadau, mama yangu alikuwa na Mimi bega kwa bega akaniambia mwanangu wewe ni mshindi inuka usonge mbele nilipata nguvu za ajabu mwaka ule ule nikaapply chuo hatimae Leo nimegraduate nimetimiza ndoto zangu sasa Nina pambana na maisha mtaani kwa nguvu zaidi ya ile niliyoinuka NAyO wakati nimedondoka huu ni ushindi mkubwa kila MTU akikutana na Mimi ananiuliza nimewezaje kwanza wanashangaa lakini nimejifunza ukidondoka unachotakiwa kukifanya ni kuinuka na kusonga mbele usipofanya hivo watakumaliza kabisa kabisa.

Mwisho niseme tu mungu awabariki sana wazazi wangu kwa michango yao bila wao Mimi nisingelifikia Leo ndoto zangu muishi maisha marefu ili mje kula mataunda ya jasho langu.
 
Siku moja tulikua tumetoka kwenye vigodoro usiku wa manane, wenzangu wote walikua wamegonga masanga.
Tulikua tumeongozana na binti mmoja ambaye nae alikua amelewa sana, kufika chobingo fulani jamaa zangu wakamparamia wakawa wanataka kumbaka yule binti.
Nilimwonea huruma na kumsaidia yule binti asidhalilike kwa kufanyiwa ukatili ule.
Nilitupilia mbali urafiki nilio kua nao na wale jamaa na kuwasihi wasimfanye chochote yule dada.
Lakini kitendo hiki kikapelekea wenzangu wanigeuke na kuanza kunishambulia.
Nikawa sina jinsi, moyoni nikajisemea potelea mbali kama urafiki ufe tu lakini habakwi mtu hapa. Ilitokea purukushani moja ya hatari pale, watu waling'oka meno wengine walivuja damu usiku ule.
Nikaondoka na binti wa watu yupo salama salmini, nikamsindikiza kwao Kisha nikarudi ghetto kupoa.
Hii sito isahau na nyingine nyingi.
 
Nilimtongoza madam nikiwa primary school. Aiseeee nilijiona gentleman
Umenikumbusha hata mm niliwahi kumbusu madam wa field mbele ya darasa nilikuwa namtamani, tulibishana na washkaji wakasema nikimbusu napewa buku tano nkamaliza kazi alinishitaki na kesi iliisha ila tulikuja kuwa wapenzi tulipokutana chuo maana kpnd hicho nilikuwa form six
 
Ah kina story moja hivi Nilifanya kufa kupona..dahh sitaki hata kuikumbuka,it was the most painful to me
All in all, never give up..
 
Mimi mpaka kesho najiona jasiri mno maana nikikumbuka niliyopitia Nina kila sababu zakujiona jasiri

Iko hivi mwaka 2013 nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho udom nilidisco, hakuna kipindi kigumu ambacho nimewahi pitia kwenye maish yangu kama hiki kiukwel mpaka kesho huwa sijuagi kwanini lile jambo lilitokea

Sina historia ya kufail maisha yangu yote nimekuwa na performance nzuri sana tangu primary school mpaka chuo ila nikiwa first year nilipata sup somo moja, nilicarry ilo somo mana sikupenda nipate kalai hapo ndipo balaa lilipoanza sitokaa nisahahu mana tangu nicarry lile somo matokeo yakitoka kwangu empty fatilia jamaa hawakuwa serious kabisa na maisha yetu wanapiga danadana na Mimi nikaona ah kwasababu huyu ndo mwalimu wa somo na ni HOD atarekebisha mana ndo zilikuwa story zake hizo mwaka wa pili ukakatika fresh matokeo yangu yanapendeza,mwaka wa tatu pia ukakatika matokeo fresh ikumbukwe iyo ndo ilikuwa sup pekee ambayo niliwahi ipata na GPA yangu ilikuwa kubwa mno japo nilikuwa Nina kimeo,

Nikiwa home nasubiri confirm graduation naangalia matokeo bado ikabidi nirudi kwa jamaa namwambia anasema aah mbona fresh nenda nakuwekea matokea ndugu zangu naomba kusema nilichokutana nacho mungu ndo anajua mpaka Leo ninaishi ni kwa neema na upendo wake mana ilifika mahali nilitamani nijiue kabisa sikuwa waza kama itakuja tokea siku nikapata pigo kubwa kama lile nilikata tamaa kabisa nikiangalia rafiki zangu, wazazi wangu nilikuwa nawaza kuanza maisha sasa badala yake nikawaza ntaanzaje upya tumaini likapotea nikadhoofika mwili vidonda vya tumbo,pressure nikawa naumwa kila nikienda Pima naonekana sina tatizo nyumbani hapakukalika kabisa

Mungu ni mwaminifu mama yangu alinitia moyo sana hakuniacha kabisa yeye ndio MTU pekee ambaye aliniami na mpaka kesho ananiamini,simlaumu baba yangu kwa hasira alizokuwa nazo juu yangu kwa sababu naelewa maumivu aliyoyapata gharama alizopoteza Leo nakuja muaibisha kiashi kile hali ilikuwa mbaya wadau, mama yangu alikuwa na Mimi bega kwa bega akaniambia mwanangu wewe ni mshindi inuka usonge mbele nilipata nguvu za ajabu mwaka ule ule nikaapply chuo hatimae Leo nimegraduate nimetimiza ndoto zangu sasa Nina pambana na maisha mtaani kwa nguvu zaidi ya ile niliyoinuka NAyO wakati nimedondoka huu ni ushindi mkubwa kila MTU akikutana na Mimi ananiuliza nimewezaje kwanza wanashangaa lakini nimejifunza ukidondoka unachotakiwa kukifanya ni kuinuka na kusonga mbele usipofanya hivo watakumaliza kabisa kabisa.

Mwisho niseme tu mungu awabariki sana wazazi wangu kwa michango yao bila wao Mimi nisingelifikia Leo ndoto zangu muishi maisha marefu ili mje kula mataunda ya jasho langu.
Mbona kama nakufahamu...[emoji102]
 
Ndio mkuu mana nikawa mtu kati na aliye umia zaid ni bibi harus huyo ndiyo canceling ilichukua nafas
we zuzu kweli!spelling check hakuna neno canceling labda hicho ni kisukuma
 
Mbona kama nakufahamu...[emoji102]
Yawezekana lakini pia watu wanastory za maisha zinazofanana hivo yangu yaweza pia kuwa inafanana na ya unaemfahamu
 
Nakutania tu... nina mtu wa krb mwenye stry kma yako....
 
Nilijizuia kulia kwenye msiba wa mama yangu hii yote ilikuwa ni njia ya kuonesha walimwengu kuwa sikuumia kwani tangu anaanza kuugua mengi yalisemwa hasa mambo ya ushirikina kuhusu ugonjwa wake ila niliwachekea wote pale msibani ila kila nikikumbuka huwa natokwa na machozi sana.

"Usitake wanadamu wajue ulivyoumia hata kama watakufanyia mabaya wewe cheka nao"
 
Mi nakumbuka miaka ya 1992/93 pale
hospitali ya meta mkoani mbeya kulikuwa
na pori almaarufu forest.
na kulikuwa na kituo cha mabasi yanayoelekea
mwanjerwa yakitokea mbalizi.

Siku moja tukiwa kwenye basi na mdogo wangu
Binti mmoja aliporwa kitenge alichodai aliagizwa
na mzazi wake akanunue.Wale waporaji wakikimbilia mstuni.
Na pale barabarani walikuwa wanakaa wahuni
ambao walijifanya wasamaria wema kumsaidia
yule dada kuwafukuza waporaji wakatokomea mstuni wakijidai kumsaidia.

Abiria kwenye gari walijitahidi kumuita yule
dada asiwafuate wale wahuni kwani wangemdhuru
yule dada hakutaka kumsikiliza mtu
aliendelea kulia na kuwafuata wale vijana
waliojifanya wanamsaidia.

Mimi roho yangu iliuma sana,nikamwambia mdogo
wangu tushuke ili walau tumsihi yule dada arudi asije akadhurika.
Tulishuka tukaacha lile basi likiendelea na safari.
Pia kuna baba mmoja na kijana mmoja
walishuka kuungana nasi kumnusuru yule dada.
Yule baba tulimuacha kwani tulikuwa tunakimbia mbio.

Tulifanikiwa kumkuta yule dada akiwa peke yake,
lakini akizidi kupiga mbio kuwafuata wale vijana.
tulimsihi arudi ila hakutaka kutusikiliza
akidai mama yake atamuua.Tulizidi kujisikia vibaya
ikabidi tuungane naye kuwasaka.

Kwa bahati tuliwaona kwa mbali msituni bondeni
wameishakuwa kitu kimoja,ila yule mporaji
tulikariri rangi ya nguo yake.
Tuligawanyika ili kuwazunguka,mimi nikapitia
upande wa mbele walikokuwa wanaelekea
na mdogo wangu na yule kijana mwingine waliwaendea kwa nyuma.

Nilifanikiwa kuwawahi kule mbele na nikatunga stori
ya kuwachelewesha ili wenzangu wafike.
Niliwaambia nimepotelewa na ng'ombe wangu
nikawaauliza kama wameishawaona.
Nikiwa nawaelezea stori hiyo,yule dada akajitokeza
kwenye zile barabara za forest kwa mbali wakamuona
wakaamua kutimua mbio,ila wakawawameishaogopa
wakaacha ndala zao ili kujiokoa.

Nilijitahidi kumkamata mmojawapo
akawa ananitishia kunichoma kisu,lakini
akaniponyoka na akanizidi mbio.Kwa bahati
wale wenzangu wakamtia mbaroni yule
mwenye kitenge wakati anajaribu kunikimbia mimi
akapitia kule walikokuwa wanatokea,wakafanikiwa
kumnyanganya kile kitenge.

Wale vibaka walipanic wakidhani lile
pori lilikuwa limejaa watu wanaowatafuta
kumbe tulikuwa watatu na yule binti tu.
Tulifanikiwa kumrudishia yule binti
kitenge chake,na ndala za wale vibaka kama ushahidi
wa yaliyotokea.Kwa kweli tulifurahi
ila nikikumbukaga hii stori huwa najiuliza huo ujasiri
sijui ulitoka wapi ukizingatia hilo eneo miaka hiyo
majambazi yalikuwa yanaua watu.

Nawapongeza wote tulioshirikiana,na hasa
yule kijana mwingine na yule baba
kama nao wapo humu jf nawapa big up sana
kupitia uzi huu.
 
Niliwapatanisha baba na shangazi waliokuwa maadui kwa takriban miaka zaidi ya kumi..

Wakubwa zangu woote (Watoto wa shangazi) hawakuthubutu hata kujaribu kulitatua Tatizo kwakuogopa lawama.

Kwa uwezo wa Mungu nilifanikiwa.
 
nyie bwana kitenge sh ngapi si mngemchangia tu dada hela akanunue kingine? acheni ubahili
 
Back
Top Bottom