Ni Jambo gani la ujasiri sana uliwahi kufanya mpaka leo ukikumbuka unafurahia na kujiona mwamba...

Ni Jambo gani la ujasiri sana uliwahi kufanya mpaka leo ukikumbuka unafurahia na kujiona mwamba...

nyie bwana kitenge sh ngapi si mngemchangia tu dada hela akanunue kingine? acheni ubahili
Asante nadhani hujui maana ya pori,unamchangiaje mtu anunue kitenge porini?
ila kwa akili ya haraka haraka unaweza ukaona ni rahisi.Yule dada alikuwa
hasikii la mtu ila kitenge enzi hizo vilikuwa vinatoka malawi.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mimi mpaka kesho najiona jasiri mno maana nikikumbuka niliyopitia Nina kila sababu zakujiona jasiri

Iko hivi mwaka 2013 nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho udom nilidisco, hakuna kipindi kigumu ambacho nimewahi pitia kwenye maish yangu kama hiki kiukwel mpaka kesho huwa sijuagi kwanini lile jambo lilitokea

Sina historia ya kufail maisha yangu yote nimekuwa na performance nzuri sana tangu primary school mpaka chuo ila nikiwa first year nilipata sup somo moja, nilicarry ilo somo mana sikupenda nipate kalai hapo ndipo balaa lilipoanza sitokaa nisahahu mana tangu nicarry lile somo matokeo yakitoka kwangu empty fatilia jamaa hawakuwa serious kabisa na maisha yetu wanapiga danadana na Mimi nikaona ah kwasababu huyu ndo mwalimu wa somo na ni HOD atarekebisha mana ndo zilikuwa story zake hizo mwaka wa pili ukakatika fresh matokeo yangu yanapendeza,mwaka wa tatu pia ukakatika matokeo fresh ikumbukwe iyo ndo ilikuwa sup pekee ambayo niliwahi ipata na GPA yangu ilikuwa kubwa mno japo nilikuwa Nina kimeo,

Nikiwa home nasubiri confirm graduation naangalia matokeo bado ikabidi nirudi kwa jamaa namwambia anasema aah mbona fresh nenda nakuwekea matokea ndugu zangu naomba kusema nilichokutana nacho mungu ndo anajua mpaka Leo ninaishi ni kwa neema na upendo wake mana ilifika mahali nilitamani nijiue kabisa sikuwa waza kama itakuja tokea siku nikapata pigo kubwa kama lile nilikata tamaa kabisa nikiangalia rafiki zangu, wazazi wangu nilikuwa nawaza kuanza maisha sasa badala yake nikawaza ntaanzaje upya tumaini likapotea nikadhoofika mwili vidonda vya tumbo,pressure nikawa naumwa kila nikienda Pima naonekana sina tatizo nyumbani hapakukalika kabisa

Mungu ni mwaminifu mama yangu alinitia moyo sana hakuniacha kabisa yeye ndio MTU pekee ambaye aliniami na mpaka kesho ananiamini,simlaumu baba yangu kwa hasira alizokuwa nazo juu yangu kwa sababu naelewa maumivu aliyoyapata gharama alizopoteza Leo nakuja muaibisha kiashi kile hali ilikuwa mbaya wadau, mama yangu alikuwa na Mimi bega kwa bega akaniambia mwanangu wewe ni mshindi inuka usonge mbele nilipata nguvu za ajabu mwaka ule ule nikaapply chuo hatimae Leo nimegraduate nimetimiza ndoto zangu sasa Nina pambana na maisha mtaani kwa nguvu zaidi ya ile niliyoinuka NAyO wakati nimedondoka huu ni ushindi mkubwa kila MTU akikutana na Mimi ananiuliza nimewezaje kwanza wanashangaa lakini nimejifunza ukidondoka unachotakiwa kukifanya ni kuinuka na kusonga mbele usipofanya hivo watakumaliza kabisa kabisa.

Mwisho niseme tu mungu awabariki sana wazazi wangu kwa michango yao bila wao Mimi nisingelifikia Leo ndoto zangu muishi maisha marefu ili mje kula mataunda ya jasho langu.
Pole sana mkuu,nilidhani umedisco kwa kushinda makuti,kumbe ni uzembe wa walimu
 
Nilipokua mdogo nilikua nafuga Sungura,sasa kuna wale Paka vimburu walikua wanakuja usiku na kuwala watoto wa Sungura kila siku,

Nikawa naamka usiku ili kuwawinda hao Paka, kwa hasira nikamkuta Paka anawanyemelea watoto wa Sungura,basi nilichukua Jembe kimya kimya na kumkata kichwa yule Paka! Nilikata vichwa kama Paka wanne hivi,na Sungura wangu wakawa wanazaliana na kuishi kwa amani,

Lakini mpaka leo hii hua nikikumbuka siamini kabisa,na kujiuliza hivi ule ujasiri wa kumkata Paka kichwa kwa jembe niliutoa wapi?
 
nakumbuka siku moja nimekunywa magrants yangu yakutosha,kichwani kila mtu namuona kama mwanangu wa mwisho.

tumetoka zetu tarime msibani pembeni kuna jembe langu linapiga mashine balaa tuko na prado.
kufika maeneo ya bunda tukapigwa tochi na wazee wenye mamlaka ya mwendo kasi.

ile tuu kutusimamisha mimi nikashuka nikaenda zangu vichakani kulimwaga siunajua tena mtu ukiwa tungi inavyokuwaga ... narudi nakutana na yule mshikaji wangu ambaye ni dereva wana bembelezana na trafik .
mimi nikaingia nika kaa kwenye siti yangu siti za nyuma kuna washikaji wawili wamevaa miwani black mimi niko pembeni ya dereva .

nikaingia nikijifanya ndio bosi wao namuuliza dereva " kijana kwa kunanini hapa?" yule dereva naye akajiongeza "bosi mwendokasi"

nikamchimba mkwara "afande unatujua sisi ni wakina nani?...wewe upo kazini na sisi tupo kazini naomba utuache tusije tukaharibiana kazi" dah afande kusikia vile na ukizingatia ilikuwa ni kipindi cha JK (pumzika msoga baba tunakukumbuka kweli kweli) maana ingekuwa ni kipindi cha mjomba magu nadhani bado tungekuwa ata butimba .

afande kusikia vile alituomba msamaha kwa kutupotezea muda basi kwenye gari kila mtu "grants oyeee."
 
kipindi nipo form 6 mimi na wenzangu kama 4 tulikuwa tunafanya project ili tumpelekee mwalimu sasa katika project yetu ilikuwa lazima ufanye tafiti na ukusanye data kisha uandike ripoti umpelekee mwalimu.

sasa bwana tukiwa njiani tunaenda kuwahoji wakulima fulani hivi kuna kichaka fulani hivi tukamkuta mwanafunzi wa kike akiwa amepakatwa na mwanaume kwa kukisia yule mwanaume alikuwa ana miaka 24+,tulivyowapita moyo ulituuma sana huku tukijadili saa tano yote hii asubuhi huyu demu yupo kichochoroni na uniform yani kwao wanajua yupo shule lakini yupo na mwanaume huku wamejificha sasa tulivyomaliza kuwahoji wale wakulima na kuchukua data zetu na kuanza kurudi tukawakuta bado wamekaa wanapiga story ase tukawafungia safari mpaka walipo sasa mtangulizi wetu aliyekuwa mbele alipigiwa simu hivyo akatoa simu akawa anazungumza sasa yule kijana akaogopa na akasimama kama kujitetea huku akitetemeka siye tupo nyuma tena kikauzu hatuongei sasa yule chali yetu aliyopo mbele alivyomaliza kuongeza na simu akamstua mwenzetu mmoja ongea na hao..

yule demu tulimuuliza yupo kidato cha ngapi akatuambia form 1,na huyu mkaka ni nani yako akatujibu mchumba wangu ,mbona saizi saa 5 asubuhi muda ambao ulipaswa kuwa shuleni kusoma lakini upo hapa ,akawa anajingatangata kidole

tukamuambia kuwa na akili kijana umevaa uniform halafu unakaa kichochoroni na mwanaume asubuhi tena hivi hujifikiri wapita njia'' wanawaonaje na mzee wako anajua saizi mwanaye yupo shuleni lakini upo kichochoroni kwelihaki hiyo.

tukamwambia sisi kila moja ana demu hapa lakini hatufanyi ujinga ambao wewe unafanya halafu ukizingatia upo form 1 ,tulipiga sana lecture yule jamaa alituomba msamaha na tulimsema kweli hivi huoni aibu kabisa upo na mwanafunzi mdogo kichochoroni tena kavaa uniform asubuhi tena muda wa masomo.

ase kwa kitendo kile najiona/tunajiona shujaa ,maana moyo ulituuma sana japo tuliwapisha mwanzo lakini tukasema haiwezekani ase yani huyu demu baba yake anajua yupo school halafu yupo kichochoroni kapakatwa haiwezekani.. hapo hapo walisepa na kila mmoja alikwenda njia yake sijui kama walipita denge kukutana sehemu nyingine au la

yule demu sijui matokeo yake ya form 4 atakuwa amepata ngapi ase alikuwa mdogo sana
 
Pole sana mkuu,nilidhani umedisco kwa kushinda makuti,kumbe ni uzembe wa walimu
Asante kiongozi na hilo ndo jambo ambalo lilikuwa linaniumiza sana sikuwahi ijua bata ilikuwa Mimi na shule shule na mimi, ila baadae ilibidi nibadilishe tu mfumo nimesoma kwa raha sana niliporudi tena chuo mana nilijipa muda wa kuhave funny pia ilikupunguza msongo wa mawazo na mambo yakaenda vizuri sana,
 
Back
Top Bottom