kipindi nipo form 6 mimi na wenzangu kama 4 tulikuwa tunafanya project ili tumpelekee mwalimu sasa katika project yetu ilikuwa lazima ufanye tafiti na ukusanye data kisha uandike ripoti umpelekee mwalimu.
sasa bwana tukiwa njiani tunaenda kuwahoji wakulima fulani hivi kuna kichaka fulani hivi tukamkuta mwanafunzi wa kike akiwa amepakatwa na mwanaume kwa kukisia yule mwanaume alikuwa ana miaka 24+,tulivyowapita moyo ulituuma sana huku tukijadili saa tano yote hii asubuhi huyu demu yupo kichochoroni na uniform yani kwao wanajua yupo shule lakini yupo na mwanaume huku wamejificha sasa tulivyomaliza kuwahoji wale wakulima na kuchukua data zetu na kuanza kurudi tukawakuta bado wamekaa wanapiga story ase tukawafungia safari mpaka walipo sasa mtangulizi wetu aliyekuwa mbele alipigiwa simu hivyo akatoa simu akawa anazungumza sasa yule kijana akaogopa na akasimama kama kujitetea huku akitetemeka siye tupo nyuma tena kikauzu hatuongei sasa yule chali yetu aliyopo mbele alivyomaliza kuongeza na simu akamstua mwenzetu mmoja ongea na hao..
yule demu tulimuuliza yupo kidato cha ngapi akatuambia form 1,na huyu mkaka ni nani yako akatujibu mchumba wangu ,mbona saizi saa 5 asubuhi muda ambao ulipaswa kuwa shuleni kusoma lakini upo hapa ,akawa anajingatangata kidole
tukamuambia kuwa na akili kijana umevaa uniform halafu unakaa kichochoroni na mwanaume asubuhi tena hivi hujifikiri wapita njia'' wanawaonaje na mzee wako anajua saizi mwanaye yupo shuleni lakini upo kichochoroni kwelihaki hiyo.
tukamwambia sisi kila moja ana demu hapa lakini hatufanyi ujinga ambao wewe unafanya halafu ukizingatia upo form 1 ,tulipiga sana lecture yule jamaa alituomba msamaha na tulimsema kweli hivi huoni aibu kabisa upo na mwanafunzi mdogo kichochoroni tena kavaa uniform asubuhi tena muda wa masomo.
ase kwa kitendo kile najiona/tunajiona shujaa ,maana moyo ulituuma sana japo tuliwapisha mwanzo lakini tukasema haiwezekani ase yani huyu demu baba yake anajua yupo school halafu yupo kichochoroni kapakatwa haiwezekani.. hapo hapo walisepa na kila mmoja alikwenda njia yake sijui kama walipita denge kukutana sehemu nyingine au la
yule demu sijui matokeo yake ya form 4 atakuwa amepata ngapi ase alikuwa mdogo sana