Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Wengi hajui kuhoji watu kwa namna ya kukidhi haja ya wasikilizaji.

Hii inasababishwa na uwezo mdogo wa kufikiri sababu wengi ni feliaz

Kukatiza miziki pale inapochanganya utamu na kuanza kuongea kurudia mashairi ya muziki au kuweka matangazo

Wanachapia bila kujistukia halafu hawaombi radhi wala nini

Kukosekana kwa taarifa za kiuchunguzi badala yake kuokoteza taarifa za viongozi wa serikali na mitandao ambazo nyingine hazijathibitishwa

Kujidai kuongea kiingereza wakati wakiambiwa wasembe kwa mfululizo na kuandika wanapata buyu

Ratiba yangu kusikiliza Redio.
Jtatu - Ijumaa: Saa 12 ASB BBC kupitia RFA
Saa 12:30 Magazeti RFA
Saa 01- 10:30 Kazini
Saa 11 jioni Jahazi Clouds
Saa 03 Usk Sport Clouds
Jmosi: Saa 12 ASB BBC RFA
Saa 12:30 magazeti RFA
Saa 09 mch Terminal cloud
Saa 03usk Sport Clouds
Jpili: Saa 12: 30 Magazeti RFA
Saa 04: Sitosahau RFA
Saa 08: Njiapanda

Pia napendelea vipindi kama Bolingo time ya RFA ilikuwa tamu sana wakati wa Zuberi Msabaha.Pamoja na kile cha jmosi cha Dakote wa Clouds.

Ila Redio punguzeni kurudia rudia miziki kwani kuna akiba ya nyimbo nzuri nyingi kama mchanga wa bahari.
 
kwa ujumla tu radio nyingi kuna wanao tamani kuchekesha na hawawezi na zaidi zaidi naona kuna maa-dj wakutosha ila kwa vipindi hakuna,
ukisikiliza tbc nayo unaweza sema kuna mtu mmoja tu na chama kimoja tu ni kero sana!
 
watangazaji wengi wanakuwa bado wameamka na kidang' a au bado kinakuwa hakijaisha kichwani, sababu watangazaji wengi wa hizi Redio pendwa hawajawahi hata kwenda Congo tu hapo kujifunza weledi wa taaluma hiyo achilia mbali syria, lebanon au hapo Somalia..hawa wanajua kutangaza tu matamasha, ndio maana wanaweza report taarifa ya kuhuzunisha huku nyuma ikigongwa beat ya babalao.
 
mike2k, Matangazo yasiyo na Mpangilio maalum..matangazo yawepo ila kuwe na time range ya kueleweka especially Clouds Fm yani Tangazo likiisha wataeka ata Jingle yao ikiisha the Same tangazo will come again...ata mara mbili mfululizo wanaeza rudia
 
Mijadala isiyokuwa na tija, porojo nyingi (taharifa bila vyanzo maalum), mahojiano yenye uongo mwingi ndani yake (ilimradi kipindi kimalizike).

Sometimes huwa nasikiliza radio katika mahojiano au utoaji wa taharifa fulani mpaka nabaki kucheka tu jinsi tunavyoingizwa chaka na baadhi ya media, huwa nazima radio nasikiliza music.

Mara mia nikae kusoma kitabu cha think and grow rich kuliko kusikiliza redio masaa ishirini na nne.
 
Watangazaji kuchanganya kiswahili na kiingereza kwanini wasitumie lugha moja na kuigana katika utangazaji,kero ya matangazo clouds FM,redio kutokupiga nyimbo za hiphop Mara kwa Mara kama hizi za wabana NOZI.

Inabidi nimpe pongezi Anko Sam,mtangazaji Wa zamani RFA zamani alikuwa anatudondoshea mikwaju ya hiphop bongo katika kipindi cha Weekend fever ilikuwa balaa sidhani kama kulikuwa na redio inagonga hiphop kama RFA kupitia anko sama.
BiG up sana Bro ma raper wengi waliibuliwa ngoma kutoka pande zote za Tanzania bila kubagua.
 
Ase kuna radio Inaitwa Kill Fm. Ipo Kilimanjaro haijasambaa sana. Watangazaji wa ajab ajabu. Kelele kelele mingi. Hasa kuna kipindi kinaendeshwa na chali mmoja wa kiume ila tabia za kike. Radio inakua na kipindi cha mipasho ni redio hiyo kweli. Afu mtangazaji mwanaume

HII NILIISAHAU KUIONGEZA HAPO JUU. HIIMRADIO BHANA HAINA MPANGILIO WA VIPINDI LEO KIPINDI FULANI UTAKISIKIA MDA FULANI KESHO UKIKITAFUTA TENA HAKIPO KABISA.
 
Kwani mumelazimishwa kusikiliza hizo redio?

RADIO HAIKWEPEKI MKUU. HASA SISI WENYE MAGARI SIYO KILA MUDA UNASIKILIZA MUSIC. RADIO KAMA CLOUDS ASILIMIA 90 NI MATANGAZO TU.
 
Ratiba yangu kusikiliza Redio.
Jtatu - Ijumaa: Saa 12 ASB BBC kupitia RFA
Saa 12:30 Magazeti RFA
Saa 01- 10:30 Kazini
Saa 11 jioni Jahazi Clouds
Saa 03 Usk Sport Clouds
Jmosi: Saa 12 ASB BBC RFA
Saa 12:30 magazeti RFA
Saa 09 mch Terminal cloud
Saa 03usk Sport Clouds
Jpili: Saa 12: 30 Magazeti RFA
Saa 04: Sitosahau RFA
Saa 08: Njiapanda

Pia napendelea vipindi kama Bolingo time ya RFA ilikuwa tamu sana wakati wa Zuberi Msabaha.Pamoja na kile cha jmosi cha Dakote wa Clouds.

Ila Redio punguzeni kurudia rudia miziki kwani kuna akiba ya nyimbo nzuri nyingi kama mchanga wa bahari.

RFA WAPO VIZURI UKILINGANISHA NA MEDIA NYINGINE... UKONGWE UNAWABEBA
 
Sikiliza isiyo na matangazo bro

.........Redio na matangazo ni sawa na gari na mafuta mzee.
SAWA SAWA MKUU! tatizo matangazo yanafikia level yanakera kama clouds na hiyo fiesta yaani mpaka watangazaji hawawazi kingine kila sekunde ni fiesta kila dakika ni fiesta. wakikaahapo studio ni fiesta tu. rais alisema kuwa anaiskiliza clouds pale magogoni nadhani anakereka kuliko hata mimi.
 
Vipindi vingi vya redio hasa vile vya mijadala ni TAKATAKA kabisa, hakuna hoja ni makelele na mayowe tuu, watangazaji hawaulizi maswali ya akili yani sijui huko vyuoni wanaenda kufundishwa nini, haya swala lingine ni kuchukua wasanii na kuwafanya watangazaji wa vipindi huo ndo upupu mwingine, mwisho ni hili janga la wanaume kutangaza vipindi vya mipasho kama yule wa radio free asee ni tatizo unaezasema jamaa siyo riziki
 
Back
Top Bottom