Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Ni jambo gani linakukera kwenye Redio za Tanzania?

Mnapata wapi muda wa kuwasikiliza hao vilaza.. Mi nasikiliza muziki tu wakianza porojo zao nahama station maana hamna kipya watakachoniambia..

Kwa sasa nasikiliza sana Choice Fm maana hawa ni pini tu mwendo mmoja!!
Radio ina vitu vitatu muhimu,( habari,elimu,burudani) kimoja kikizidi basi shida ishaanza
 
CMG wanakuambia wao ndio redio ya kwanza kuwafanya watangazaji wake kuwa huru studioni, mtangazaji anaweza hata kujamba live on air[emoji39][emoji39][emoji39]. Hawa wengine nao wakaiga, sasa hivi uki-tune redio utasikiliza mabishano(sio mijadala), utasikiliza ujuaji(kila mtu ni anajua) na hakuna anayemsikiliza mwenzake. Nikiwa kwenye gari nasikiliza redio, otherwise sisikilizi.
 
Yule jamaa mwanzon nlijua, James delicious
Ase kuna radio Inaitwa Kill Fm. Ipo Kilimanjaro haijasambaa sana. Watangazaji wa ajab ajabu. Kelele kelele mingi. Hasa kuna kipindi kinaendeshwa na chali mmoja wa kiume ila tabia za kike. Radio inakua na kipindi cha mipasho ni redio hiyo kweli. Afu mtangazaji mwanaume
 
KERO YANGU TBC NI TAARIFA YA HABARI DAKIKA TANO MMESHAMALIZA.RADIO YA KANISA INATANGAZA HABARI NYINGI ZILIZOTAFITIWA KWA DAKIKA KUMI NINYI MNASHINDWA NINI.NDIO MAANA RAISI AKITUKANA WATU NAMKUBALI.HATA MAFANIKIO HAMTANGAZI? WALE WEZI WA PESA ZA UMMA JE WANA NAFASI TENA AWAMU HII?
 
Mnapata wapi muda wa kuwasikiliza hao vilaza.. Mi nasikiliza muziki tu wakianza porojo zao nahama station maana hamna kipya watakachoniambia..

Kwa sasa nasikiliza sana Choice Fm maana hawa ni pini tu mwendo mmoja!!
Vipi kuna ma DJ's wakali wanaopiga ngoma na mikito heavy? Bro!!
 
Ase kuna radio Inaitwa Kill Fm. Ipo Kilimanjaro haijasambaa sana. Watangazaji wa ajab ajabu. Kelele kelele mingi. Hasa kuna kipindi kinaendeshwa na chali mmoja wa kiume ila tabia za kike. Radio inakua na kipindi cha mipasho ni redio hiyo kweli. Afu mtangazaji mwanaume
Hahahaaaa jamaa juzi kati tukawa tunabishana nasema ni mwanamke kumbe ni dume anaitwa Arnold Moshi .. #Itakuasioridhikiyule
 
Achaneno nazo siku hizi radio station ni nyingi chagua inayokufaa tu kama wanazingua
 
baada ya tangazo fulani la bidhaa kuisha utasikia mtangazaji anasema "hata me natumia hayo maji yakoo bariiida sana"
"unasikia bwana kitenge hizo karanga ninatafuna sana kabla sijaja hapa kipindini"

"kifurushi hicho ni bomba saana yaani hata ile laini ya mtandao mwngne nishaiacha ..ninkuperuzi tu"

NB NDUGU HAWA WATU NI WANABOA KILA TANGAZO UNAKUTA YEYE TU ANATUMIA ila sijawahi sikia baada ya tangazo la condom kuwa kuna mtangazaji huwa anaongea lolote
 
SAWA SAWA MKUU! tatizo matangazo yanafikia level yanakera kama clouds na hiyo fiesta yaani mpaka watangazaji hawawazi kingine kila sekunde ni fiesta kila dakika ni fiesta. wakikaahapo studio ni fiesta tu. rais alisema kuwa anaiskiliza clouds pale magogoni nadhani anakereka kuliko hata mimi.

Wakiacha kurusha matangazo mtasaidia kulipa na matangazo na gharama nyingine za uendeshaji?

..........Tatizo letu wabongo tunalalamika mno, kila siku, kila mtu analalamika.
Wewe umelazimishwa kupitia na ku comment huu uzi??
Sijalazimishwa ndio maana silalamiki.

.........sasa wewe redio zote hizi bado mnalialia.
 
Waandishi wa habari wananjaa sana. Yaani ni ombaomba hatari hadi naboreka yaani
 
Ku interview watu ambao ni irreverent kwenye maswala ya kitaaalamu.
 
Binafsi nachukuia pale wametoka kucheza matangazo kama 15 hivi, mengine mara mbili mbili; halafu watangazaji wakirudi on air wanazungumzia hayo hayo matangazo kama promotion hivi.
Hata kama ni profit maximization, sasa redio unakuta 80% ni matangazo. RADIO ZIMEKUWA BILLBOARDS sasa hivi.
Na pale wakiongea, utafikiri wako kwenye personal podcasts zao.

Mwisho wa siku kunakuwa hakuna point ya redio. Hakuna utakachojua. Kwa sababu hata mada yenyewe unakuta wameichukua instagram halafu inafanyiwa discussion kwa ZOGO.

Mwisho, radio zote sasa ni Clouds Fm.
Clouds Fm ilianzishwa kwa ajili ya bongo flava na vijana wadogo. Sasa kwa sababu ya uzuri wa soko hilo, basi kila mtu anaenda huko. Ukiwa mtu wa kufuatilia facts and civilized discussions, unakosa pa kujichimbia.

Sometimes unajisikia tu upate mijadala ya hoja kama kipima joto ya ijumaa ITV, lakini hupati... halafu unakuta mkoa wako una redio kama 40 hivi, halafu hakuna hata Moja yenye watu wasio na mihemko bali hoja.
Yaani sasa hivi ikishafika saa 3 asubuhi hakuna kipindi cha maana.

Anyways, labda my time is up!
 
Back
Top Bottom