Hii ni muhimu zaidi kwetu wenye vipato vya kawaida.
Sio jambo la aibu hata kidogo wala sio urijali wala ujanja kwenda date bila kumpanga mapema kuhusana na bajeti. Ukishindwa kujipanga jiandae kupata aibu, kuharibu bajeti yako, n.k.
Kumjuza bajeti yako itakusaidia mapema kujua kama yupo nje ya ligi / level zako, nidhamu yake kwenye pesa, n.k.
Unaenda date bila plan yoyote, mfukoni una kilo ukajitutumia ita cover kila kitu, Kufika huko trailer inaanza anaagiza kinywaji ghali cha elf 70, kijasho kinakutoka bado hajaagiza msosi, Date ishaharibika kwasababu akili yote ipo kwenye bili.
Unaenda date bila plan yoyote, unamkuta kafika na kamati yake ya watu wawili, hawajaagiza chochote wanakusubiri wewe usimamie kila kitu, dakika 2 hazijaisha wameanza kuagiza mbuzi choma, savannah, lobsters, n.k. yani hadi vingine wanaweka kwenye pochi, ki laki 1 na nusu ulichobeba kinapigwa mtama ndani ya dakika chache sana.