Ni jambo la kushangaza kwa Mkurugenzi aliyeiba mabati kuendelea kuwa ofisini hadi muda huu

Kuwa msimamizi wa uchaguzi hakumfanyi kuwa na mandate ya kufanya ubadhirifu wa mali za umma mkuu. Sheria ichukue mkondo wake
Mbona umekomaa na huyo mkurugenzi wakati Kuna gaidi moja lilikwiba 8.9 bilion michango ya wabunge na hakufukuzwa ofisini?
 
Juzi Kati ameyarudisha na ameyagawa kwenye Shule za sekondari na msingi.
 
Mbona umekomaa na huyo mkurugenzi wakati Kuna gaidi moja lilikwiba 8.9 bilion michango ya wabunge na hakufukuzwa ofisini?
Je, kuna ushahidi katika hilo?
Kama upo leta tujadili
 
Msimamizi na muajiri mkuu wa serikali,Raisi,yupo bize anatembeza tumbo,na mimacho ya kulegeza,
Kama watendaji wa Tasac na hazina walipiga milioni 500!kwa kwa kukaa vikao tu,na wakakalipiwa tu,na mpaka leo wapo wanakula bata,sembuse DED aliyeiba tumabati!
 
Juzi Kati ameyarudisha na ameyagawa kwenye Shule za sekondari na msingi.
Kumbe sasahivi wizi umehalalishwa unaiba ukikamatwa unarudisha kesi inaisha?
 
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale na watumishi saba wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa waliodaiwa kuiba mabati 1,172 wameyarejesha wilayani humo.

Hawa ni viongozi ni watumishi wa umma, wamekiri kuiba ni wahujumu uchumi haitoshi tu kuyarudisha bali walitakiwa wafunguliwe mashitaka na wafukuzwe kazi. Kwanini hadi leo DED bado yuko ofisini? Rais anasubiri nini kumfuta kazi mteule wake?

 
Hapo ndo nakumbuka enzi Za Magufuli huyu jamaa angekuwa ameshatumbuliwa, ila huyu mama ni dhaifu sijui kama miradi aliyoacha RIP itakamilika kwa ulegevu huu, wizi umetamalaki kila halmashauri sasa hivi,
 
Leo hii bavicha unashauri Rais kumtumbua mtu?

Si juzi tu hapa mlikuwa mnawatetea kwamba wanaonewa wakitumbuliwa na Magu?
 
Angekuwa mtendaji wa kata sasahivi angekuwa magereza kwa uhujumu uchumi
 
Mama kazidiwa na majukumu ya royal tour, apewe muda...
 
Leo hii bavicha unashauri Rais kumtumbua mtu?

Si juzi tu hapa mlikuwa mnawatetea kwamba wanaonewa wakitumbuliwa na Magu?
Usiwe filimbi, kuna makosa yaliyo wazi kama haya huwezi kuyatetea sio anafukuza mtu kwa tetesi za kutembea na hawala yake.
 
Hivi unajua huo wizi umechunguzwa na kutolewa ripoti na jeshi la polisi?

Kwahiyo unataka kusema jeshi la polisi wameongopa na wanataka kumbambikia DED kesi ya wizi?
Nini msimamo wako kuhusu jeshi la polisi?,unawakubali?
 
Mama kazidiwa na majukumu ya royal tour, apewe muda...
Mama sio lazima afanye kila kitu ndio maana anateua mawaziri ili wamsaidie. Mathalani hili suala la DED lipo chini ya TAMISEMI lakini waziri yupo kimya hata kukemea hajakemea au naye anasubiri maagizo kutoka juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…