Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Twambombo wakuu!
Mwanaume kulia ni mwiko! Haipendezi mwanaume aliyekomaa kulialia. Hata hivyo lipo jambo moja linaloweza mfanya mwanaume alie kama mtoto mdogo, nalo ni kifo.
Kifo kwa wahusika wafuatao
1. Wazazi au mlezi
Mwanaume anaweza akalia kwa kifo cha mama au baba yake aliyemlea. Zingatia neno "kulea", unaweza ukawa baba au mama mzazi lakini kwa vile hukumlea mtoto basi mtoto asiwe na uchungu na wewe. Kifo kinauma hasa kwa mtu uliyemzoea na kumpenda.
2. Mke
Hii ndio habari nyingine kabisa. Mwanaume anaweza kulia kmtoto pale anapofariki mke aliyekuwa anampenda sana, aliyemzoea, waliofanya mambo mengi. Kinachoumiza zaidi ni kumbukumbu zilizopita. Dooh!
3. Mtoto kipenzi
Mwanaume anaweza kulia ikiwa mtoto wake kipenzi atafariki. Ni kawaida mzazi kupenda watoto wote lakini lazima yupo mtoto mmoja unayempenda zaidi. Mtoto wa baba. Kipenzi cha baba akifa, baba hulia sana. Yakobo alivyoletewa habari ya kifo cha kutungwa cha Yusufu alilia. Daudi alivyosikia kijana wake aitwaye Amnoni ameuawa alilia.
Mtoto kipenzi akifa inaweza mfanya baba akachanganyikiwa. Lakini zaidi ya hapo hakuna kitu kingine kitakachomfanya mwanaume aliyekomaa kulialia kama mjinga tena mbele za watu.
Mwanaume hatoi machozi isipokuwa jasho.
Mwanamke hatoi jasho isipokuwa machozi.
Ingawa kuna mazingira ya dharura kama kutekwa na kupewa mateso makali hii inaweza kumfanya mwanaume pia akalia. Lakini sio kitu kidogo tuu mwanaume mzima unalialia kama mtoto.
Sijui umeibiwa unalia.
Sijui umeachwa na mwanamke unalia kama boya hivi.
Sijui umedhulumiwa kiwanja au mshahara unalia. Unalia nini kama mtoto wa kike, take action.
Ni aibu kwa mwanaume kulialia kijinga jinga hata vitu havieleweki. Wengine tukiona unalia tunakuzaba makofi na mitama. Akili ikukae.
Taikon nipumzike!
Kwa sasa Dar es Salaam.