Ni kama alivyosema Juliana Shonza, Mbowe must be disposed

Nandio alosababisha kupoteza wabunge na madiwani
 
Acha selfdefend nenda kwenye kujibu hoja
 
Tatizo kubwa ninalo liona kwa mbowe ni kukaribisha na kuwapa nafasi kubwa watu wasiostahili amekubali watu Kama Lema, Lisu, Heche kuwa sehemu ya maamuzi hilo ndilo linalomtesa kwa sasa. Hawa ni watu wa amsha amsha hawastahili kutoa majibu ya maswali magumu na ya haraka. Ni mara elfu mia kukubali Ushauri wa mnyika, Prof J au Mchungaji msigwa kuliko hao wanaharakati wale karama yao ni ujasiri na kuhamasisha wakiwa mstari wa mbele huku nyuma wenye akili wakiwa nyuma kuwapa ramani ya vita. Anyway wasipojitazama namuona strategist Zitto akiwapiga chini
 
Nimbinafsi na mbaguzi
 
Jambo la kwel ni lakwel tu hata kam kaongea mtoto mdogo
 
Sasa kati ya hao wagombea nani anaweza kumsaidia mwananchi kupata milo mitatu zaidi ya JPM?
Akili hizi Tunatofautiana sn. Kwan JPM anaanza sahivi kuongoza, mika mitano ikiyopita kwann hakuwasaidia. Subirin kwenye sanduku la kura, mtaona Nani ana mvuto
 
Tukio la chadema kuwafukuza TBC kwenye mkutano wao wakiwa wanarusha matangazo yao live ni dhahiri kua walificha aibu ya kukosa wafuasi kwenye mikutano yao na kuwadanganya watanzania kua wanakubalika kumbe ukweli wanaujua wenyewe.
 
Uchambuzi mzuri uliojaa hoja ya msingi, CHADEMA mjitafakari.
 
Wekeni pia na ya Dr slaa yaliyowahi kuandikwa na Juliana musiishie kwa Mbowe peke yake.
 
Hakuna anaeumia ila mnaelekezwa kwani yote yaliyosemwa ni kweli na hakuna la uongo
Mbowe hana jipya na CDM inakufa kifo kibaya mnoo
Wanaccm wanaoumia kwa uwepo wa mbowe chadema ni wenye nakisi ya akili. Haya walipaswa waseme chadema wenyewe. Au nyiye na nape pamoja na shonza ni chadema. Najua shonza kazimiss akili zake kubwa akiwa chadema yeye Sina shida naye. Huyu nape je nongwa na mbowe inatoka wapi?
Wanachadema wanampenda mbowe jamani. Halafu siwaoni mkimsema lipumba wa cuf cheyo udp, mrema tlp, ambao ni wenye viti wa vyama vyao wa muda mrefu kuliko mbowe. Kwa kutowasema hao ni uthibitisho tosha kuwa shida si mbowe kukaa muda mrefu bali ni kuikamata CCM pabaya.
Mimi na wanaccm wengine Tuliona kukuwa bilkanas mbowe atatoweka na chadema kufa wapi. Funga jela, vunja mguu wapi?
Tuache huu ujinga tujipange kutumikia wananchi kwa Uhuru na amani na utu tutaendelea kuaminika
Sasa hivi wapinzani wanaaminika kwa kuienzi amani kuliko ccm. Mfano CCM kwa miaka mitano imewakataza kufanya siasa kama sheria itakavyo, wametii. Mmekata majina wametii kufuata sheria kukata rufaa. Tunahonga ajira za walimu wako kimya . Amani inatunzwa na wapinzani kuwa wavumilivu. Tuambiane wapenzi wa CCM inatosha uchokozi wa kishamba tuache. Mbona wananchi hutuelewa bila kufanya huu undava wa kishamba.
 
Hivi kama mbowe hakuchukua uamuzi wa kuwaondoa TBC pale Mbagala kuu, Unafikiri TBC wangejua kama kuna mahali hawapo sawa katika kazi zao?
 
Nimekuelewa vizuri, hongera sana kwa thread hii. Ujumbe umewafikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…