Ni kama alivyosema Juliana Shonza, Mbowe must be disposed

Ni kama alivyosema Juliana Shonza, Mbowe must be disposed

Wanaccm wanaoumia kwa uwepo wa mbowe chadema ni wenye nakisi ya akili. Haya walipaswa waseme chadema wenyewe. Au nyiye na nape pamoja na shonza ni chadema. Najua shonza kazimiss akili zake kubwa akiwa chadema yeye Sina shida naye. Huyu nape je nongwa na mbowe inatoka wapi?
Wanachadema wanampenda mbowe jamani. Halafu siwaoni mkimsema lipumba wa cuf cheyo udp, mrema tlp, ambao ni wenye viti wa vyama vyao wa muda mrefu kuliko mbowe. Kwa kutowasema hao ni uthibitisho tosha kuwa shida si mbowe kukaa muda mrefu bali ni kuikamata CCM pabaya.
Mimi na wanaccm wengine Tuliona kukuwa bilkanas mbowe atatoweka na chadema kufa wapi. Funga jela, vunja mguu wapi?
Tuache huu ujinga tujipange kutumikia wananchi kwa Uhuru na amani na utu tutaendelea kuaminika
Sasa hivi wapinzani wanaaminika kwa kuienzi amani kuliko ccm. Mfano CCM kwa miaka mitano imewakataza kufanya siasa kama sheria itakavyo, wametii. Mmekata majina wametii kufuata sheria kukata rufaa. Tunahonga ajira za walimu wako kimya . Amani inatunzwa na wapinzani kuwa wavumilivu. Tuambiane wapenzi wa CCM inatosha uchokozi wa kishamba tuache. Mbona wananchi hutuelewa bila kufanya huu undava wa kishamba.
Kama ww unaona mbowe sio tatizo basi unakosea sana,Iv chama kikuu cha upinzani nchi ambacho kinapata ruzuku pamoja na michango ya wabunge mnayoikata kila mwezi lakini still hakuna hata ofisi za mashinani ili kuwepo na ukuaji wa chama ,Pesa zote wanakula viongozi wa chama alafu mnakuja kushtuka kipindi cha uchaguzi na kusema CCM inawakandamiza mnaakili kweli?
Endeleeni na propaganda na huo uongozi mnaotaka mtasikia kwenye Bomba
 
kutumia anga katika kampeni kwa mgombea wa chadema wakati ccm wakitumia magari ni sababu ya ushindi wa ccm maana anawafikia wananchi wengi hasa wale wa vijijini wenye kiu kuwaona kwa kufanya mikutano isiyo rasmi mingi
 
CHADEMA wakajipange kuanzia ngazi ya mwenyeki hadi mpiga deki maana hawana uelekeo sasa
 
Katika Thread yake ya tarehe 24 February 2016, Ndugu Juliana Shonza aliandika Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! akitaja sababu kadhaa za kwanini anadhani mbowe HAFAI kuwa Kiongozi si kwa chama chake tu bali popote pale Tanzania. Nilitafakari juu ya fikra zake hizo na kwa kweli baada ya Mgogoro wa TBC na CHADEMA ambao msingi wake ulikuwa kukurupuka kwa MBOWE nakubaliana kabisa na Ndugu Shonza kuwa Freeman MUST BE DISPOSED..!

Sifa moja ya Kiongozi bora ni kufanya informed decisions, maamuzi yaliyopitia tafakuru ya kutosha na kupima madhara na faida ya maamuzi hayo, katika kile ambacho kimethibitika kuwa ni kukurupuka, Mbowe aliwafukuza waandishi wa TBC wakiwa Live katika mkutano wao wa ufunguzi Mbagala, katika namna ya kudhalilisha na ambayo ingepelekea kudhuriwa kwa waandishi hao ama mali zao kuharibiwa. Leo amejitokeza hadharani bila aibu anasema alishinikizwa na kupotoshwa wakati anafanya maamuzi hayo, alisema hivi pia siku Lowasa anarudi CCM, kwa Kiongozi wa Juu kabisa wa Chama tena aliyekuwepo madarakani kwa miongo kadhaa kurudia kosa lile lile na kutoa sababu zile zile za kufanya kosa hilo ni UJUHA.

Kilichonifurahisha zaidi ni akili za wafuasi wa CHADEMA, kwa namna wanavyoiponda TBC na kwa namna walivyompongeza Mwenyekiti wao kwa kuwafukuza TBC ni ajabu kwa namna wanavyosifia na kushangilia uamuzi wa kuwaomba msamaha TBC na kuwaomba warushe matangazo yao kwa mara nyingine. Chama kile cha Freeman, kina tatizo kubwa zaidi ya nilivyokuwa nikifikiria awali.,na tatizo hilo linaanzia kwa wafuasi kabla ya Viongozi, kuwa na wafuasi wasio na mwelekeo wasiojua wanataka nini, wanageuzwa kama samaki kikaangoni., ni tatizo na kwasababu hiyo Viongozi wanajua udhaifu wa wanachama wao na wanawajua kwa dhati kabisa kuwa ni watu wasiojielewa, watu wengine wanawaita kwa lile jina baya la Manyumbu, mimi siwezi kuwaita hivyo ila hili la kushangilia matangazo ya TBC kurudishwa limenifikirisha.

Freeman amefikia mwisho wa kufikiri, hana jipya, amekosa mwelekeo, amepoteza jimboni na anapoteza Taifani, amepanic na anaona giza limetanda katika safari yake ya kisiasa. Ni Mbowe amesababisha Chama kukimbiwa na Wabunge, Ni Mbowe ameivuruga Bavicha aliwapangia safu ya uongozi na watu aliowaweka wakamkimbia, ni mbowe ameivuruga Bawacha akamuweka Mdee kwasababu zake binafsi, akagawa ubunge wa Viti maalum kwa upendeleo na matamanio ya nafsi yake, akaendesha Chama kama kijiwe cha wahuni, wale wenye fikra wakamkimbia. Chadema haikubaliki kwa wasomi, haikubaliki na Wazee, haikuwahi kukubalika na wanawake wa nchi hii, haikubaliki kwa Vijana na haikubaliki Kaskazini (hakuna Chadema Arusha, kilimanjaro wala manyara) wala Kusini , haina base Mashariki wala magharibi, Chadema ya leo ni YATIMA.

CHADEMA wamepoteza hamasa katika mikutano yao, wamepoteza mvuto kwa wananchi, wamekosa ajenda na hawana sera. Sio coverage ya TBC, ITV, Clouds TV ama media yeyote ile inaweza kuwasaidia kwasasa. Narudia tena kuwa Kampeni ni maarifa, mipango na akili, CHADEMA WAMEKOSA VYOTE....!!
Punguza uongo
Hadithi za alfu ulela ulela ndio hizi
Aliyekutuma mwambie anawashwa
 
Uongo na ukosefu wa utambuzi wa ukweli wa mambo. CCM leo ina hofia CHADEMA kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya vyama vingi, hili liko wazi sana.
Chadema tuliihofia kipindi cha Lowassa 2015. Sasa hivi hata kampeni zimepooza kwasababu hakuna ushindani kabisa. Lissu mwenyewe hajui kama anagombea urais. Salum Mwalimu ndio kabisa! Hajijui kama ni Mgombea Mwenza au bodigadi wa Lissu!
 
Back
Top Bottom