ARVs zimeanza kutolewa 2004 au 2005 sio 2010's
Uko sawa kabisa mkuu!
Pengine sikufafanua zaidi..
Ila uko sawa kabisa ARV zimeanza kutolewaa mwaka 2004 mwezi wa 10 baada ya Tanznia kufikia Waathirika 1.2 Million..
Lakini Naomba kuongezea kidogo..
Kwanza kabisa mwaka huo Huduma za Matunzo (CTC) zilizolaunch dawa ya ARV zilikuwa Chache sana Nafikiri zilikuwa Hospitali za kanda na Hospitali ya Taifa..
Na mwaka 2006 Walishuka mpaka Hospitali za wilaya nazo zikawa zinatoa Huduma ya Matunzo na Tiba(CTC).. na vilikuwa vituo 96 tu Tanznia nzima..
NA report za wagonjwa zilikuwa zikitumwa Hospitali ya Taifa kwa ajili ya kutoa report rasmi ya wagonjwa wote ili kuongeza dawa..
Ilikuwa Vyepesi sana Kuhudumia Wagonjwa wa HIV ambao hawana AIDS kwa sababu kipindi hicho walikuwa hawapewi dawa Mpaka CD4 Ziwe zimeshuka kabisa kama CD4 zilikuwa Hazijashuka Bhasi ilikuwa wanapewa Only Ctx (Septrin/Cotrimoxazole) ili kuzuia magonjwa Nyemelezi..
Na mwaka 2008 Only 13% Ndo walioanzishiwa dawa ya ARV..
Na ilipatikana bahati ya kushuka mpaka vituo vingine vya Chini na Kupatikana vituo 210 tu vinavyotoa huduma ya Tiba na Matunzo..
Na hata Dawa zilizokuwa Zikitolewa zilionekana bado ni chanzo cha kupatikana kwa Drugs Resistance hence drugs failure..
Dawa zilianza kuwa Available Bila shida miakaa ya 2010s na hasa kuanza kutumika kwa Dawa zisizokuwa na burden kwa watu na zenye mauzi machache na Huduma ilikuwa Available na affordable kwa watu wengi..
Mkuu..
Hiki ndo nilichomaanisha