Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Mwaka 2015, kwenye uteuzi wa wagombea udiwani na wabunge mambo yalikuwa kama ifuatavyo:
1. udiwani, rufaa zilikuwa 223, nyingi zikiwa za CCM (83) na Chadema (87). Hakuna mgombea wa udiwani wa CCM aliyekatwa, wakati wale wa vyama vingine waliokatwa walikuwa 11, na wengi wao (9) ni Chadema. Walioshinda rufaa walikuwa 39, CCM akiwa mmoja na Chadema 29, na wachache kutoka vyama vingine. Kwa upande wa kupita bila upinzani, wagombea udiwani walikuwa 71, na wote kutokea CCM.
2. Ubunge, rufaa zilikuwa 57, kati ya hizo, nyingi zilikuwa za CCM (11), Chadema (17) and CUF (10). Wote wa CCM hawakuathilika na kukatwa, wakati 2 walikatwa, na 14 kurejeshwa, nusu yao wakiwa wagombea wa Chadema. Ni mgombea mmoja tu wa ubunge kupitia CCM alipita bila upinzani.
Source: NEC
Inaonekana hizo rufaa za CCM zilikuwa ni za kutaka kupita bila upinzani.
Sasa, kwa mwaka huu 2020, mbona kama ukatwaji umezidi kwa wagombea wa vyama mbali na CCM, halafu upitaji bila upinzani umekithiri kwa upande wa CCM? Je, huu ni uroho wa madaraka? Je, haya ndio malengo ya sheria za uchaguzi? Kama ndio, kwa faida ya nani?