Ni kama watangazaji wa vipindi maarufu kwenye haya maredio wamebadilishwa!

vipaji ndio kila kitu mjuba
Kipaji ni added advantage lakini lazima upate elimu ya taaluma husika.
Hata ujue sheria kwa kiwango gani huwezi kuwa Wakili bila kusoma haiwezekani.
Hata ujue kutibu kwa kipaji huwezi kusajiriwa kama Daktari na haujasoma haiwezekani.
Sasa uandishi wa habari ilibaki fani isiyo na uthibiti ikaonekana ukishakua mashuhuri tu unapewa kipindi wewe mwanahabari tayari.
 
Watu tunachosahau ni kuwa diploma utaplipata vipi hauna cheti cha 4M4 ?

Ukiona MTU hana Diploma ujue tatizo cheti cha 4M4

Hapa tanzia Elimu ya chuo ni rahis Ila mchawi form four kukipata kile cheti
Muhusika angeweza kureseat kupata D nne inawezekana kabisa.
Kwasababu utaratibu huu uliletwa mwaka 2016 ni miaka 9 sasa imepita. Kama mtu kapewa miaka 9 kupata Diploma hata kama alikua lasaba angeweza kusoma mpaka kufikia Diploma hata bachelor.
Labda wahusika hawakua na nia ya kusoma au hawana mpango na hiyo kazi ya uandishi wa habari wanafanya kama kazi ya ziada ila wana shughuli zingine.
 
why nisifanye kazi ambayo najua A B C zake? Siwezi nikaacha kutatua tatizo eti kwa kuwa sijasoma. Nimejuaje hizo code kama sijasoma? Basi bodi i appreciate na kunipa ithibati kwa kuwa naweza kufanya kazi vema. Mbona kuna wengine wanatunukiwa doctorate za heshima wakati hawajaenda chuoni kuzisomea?
 
Wameachwa toka mwaka 2016, ni miaka 9 sasa imepita hata mtu wa lasaba angekua kamaliza hiyo Diploma kitambo.
Labda hawapendi shule au hawapendi kuwa wanahabari.
hawakupaswa kuondoka au kuondolewa wangeachwa wamalizikie kama walimu wa elimu za chini wanavyomalizika wenyewe kwa kustaafu licha ya kuwa nao walitakiwa kujiendeleza kielimu lakini kuna wengine hawakujiendeleza mpaka wakastaafu utumishi wao na wengine wenye elimu za juu wakaingia kazini
 
Kwa mitazamo hii ya kielimu ikiwemo kukua kwa sayansi na teknolojia kuna sababu ya kuwa na multiple education, elimu rasmi na isiyo rasmi ili tu kuweza kujikimu kimaisha pale unapokosa kuajiriwa basi option zipo za kujiajiri kuliko kwenda kufedheheka kwenye ajira za wengine kwa kuambiwa huna cheti, huna elimu na upuuzi mwingine wa kutiwa umasikini wa kujitakia
 
Hao ndio watangazaji wakubwa? Yaani mtu mzima una switch vipindi hivyo na station hizo kweli?
 
Kwani hao hawawezi kupewa crush program wakaendelea na ajira zao?mbona wenzetu duniani watangazaji wanakuwa na degree zingine kama sheria halafu wanapewa mafunzo maalumu ya uandishi wa habari na utangazaji
 
Ithibati ndugu.
 
Wameachwa toka mwaka 2016, ni miaka 9 sasa imepita hata mtu wa lasaba angekua kamaliza hiyo Diploma kitambo.
Labda hawapendi shule au hawapendi kuwa wanahabari.
We mtu kama zembwela atakubali ku resit au kufanya QT?
 
Wengine umri umeenda , umrudishe jitu zima Leo akasome mfecane war siyo rahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…