Uchaguzi 2020 Ni Kanda ya Ziwa ila maji tunapata kwa masaa na unataka tukupigie kura tena?

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwamba "Yesu wa LUGOLA" apigiwe kura na mabombadier na mastiglers goji
 
Wewe acha kutuchota akili hapa, Avatar yako inaonyesha unamhusudu Huyo unayemponda, Halafu unajifanya Bwege ili usikilizie siyo.
Iyo avata itazame kwa jicho la tatu ndyo utaelewa kwanini ipo apo.
 
Bukoba yenyew mji haunaga stendi Zaid ya kichochoro cha matope na soko kuu la mabati.

Watu wa Bukoba walishachoka Bora hata iddi Amin angeichukua sasa bukoba ingekuwa jiji sawa na kampala
 
Too Sad yaani Buhongwa tunaamka tunaona Ziwa huyoooo.Eti halafu kuna shida ya maji. Stupid policies.Halafu kutwa kunyooshea vidole mabeberu. Hivi mabeberu wanazuia msijenge mabomba na kuwa na huduma ya maji yasiyokatika katika ?

Hakuna kitu kinanikera na kunitia hasira kama kumekuwa na wawakilishi miaka na nenda rudi huko bungeni lakini maeneo mengi ya kanda ya ziwa hawana maji safi na salama ya kunywa. Maeneo ya kanda ya ziwa yote yalitakiwa yawe na maji safi na salama ya kunywa, maana chanzo cha maji kimewazunguka halafu wanaishi kwa shida shida. Na sasa hivi watapita tena kuwaomba kura halafu watawapa? Kweli akili zao zinafikiria vizuri? Kuna huduma za msingi kulingana na upatikanaji wake katika maeneo husika haitakiwi kuwa shida upatikanaji wake. Kwa kanda ya Ziwa upatikanaji wa MAJI, MAJI, MAJI, MAJI ,katika vijiji vyake vyote ni muhimu sana. Kuna mikoa mengine wanamito tu lakini maji karibia mkoa mzima yanapatikana.
 
Unaongea mara moja kwa wiki, nakaa Buswelu manispaa ya Ilemela na sijapata maji ya bomba zaidi ya miezi mitatu.

Siwezi kuwapa kura CCM hata nikiwa mgonjwa wa akili
 
Wasiofika Mwanza wanaweza kushangaa km labda tunasingizia......
Sasa chato wanakubalije kujengewa uwanja wa kimataifa wa ndege hata maji kwao ni shida?

Watz bana ni watu wa ajabu sana
 
QUOTE="LadyRed, post: 36327345, member: 358507"]
Hahahah eti mandege
[/QUOTE]
Tangu 2015 Hadi Sasa mkoa wa Mara na wilaya zake serikali haikufika huko,mkoa wa kagera na wilaya zake serikali haikufika huko.Leo wanaotarajia kwenda huko kuomba Kura za ubunge ,uraia na udiwani. Kura kwa kipindi hiki zitatolewa Kama wajumbe walivyotoa Kura za maoni" nipe nikupe,hakuna Kura za bure October"
 
Unaongea mara moja kwa wiki, nakaa Buswelu manispaa ya Ilemela na sijapata maji ya bomba zaidi ya miezi mitatu.

Siwezi kuwapa kura CCM hata nikiwa mgonjwa wa akili
Buswelu ipo within 30 km from lake victoria north, west na est imezungukwa na ziwa victoria
 
Mimi niko kata ya Kishili, naingia mwezi wa nne sasa bomba la maji la nyumbani halijatoa maji. Vyoo vya ndani bila huduma ya maji kweli!!! MWAUWASA wamenitumia bill ya July na ninashangaa kwa huduma ipi? Kipindi Corona inaanza March sisi huku tulikuwa na shida na maji ya kunawa. Kweli ulimwengu wa kati Afrika ni shiiiiidaaaa!!!
 
Kesho nakuja halo chadema kuangalia ndondo LA mashujaa vs Kishiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…