Kwa kweli, bado tuna matatizo lukuki nchi hii. Hapa leo watu wa Mza wameanza kucharuka lakini kila mtu akiamka maeneo yake akianza kutoa kero zake ni nyingi mno mpaka mtashangaa sasa hawa wanaopitaga na kutuaminisha tunaelekea kumaliza matatizo yetu hii awamu ya tano wanatokeaga wapi huko kwao ambapo pako sawa kila kitu?
Shida ni moja, kusema tu ukweli nchi hii wewe tayari unaonekana ni mbaya. Wabunge wetu sio kwamba hawasemi au hawapendi kutaka kutuongelea matatizo yetu ila mfumo unawaminya. Nakupa mfano, kwenye bunge hili hili lililomaliza muda wake Mh Kitwanga mbunge wa Misungwi alisemea jimbo lake na maeneo jirani ya Nyamagana na Magu kuhusiana na shida za maji. Aliongelea kwa uchungu mkubwa sana hata akadiriki kutaka kushika shilingi bajeti ya wizara hiyo lakini kiongozi wa bunge alimtishia kwa kumwambia kuwa asipokubali kupitisha bajeti ile basi hata yeye ataanguka kisiasa, hebu imagine mtanzania kwa style kama hiyo tutapata suluhu ya matatizo yetu bungeni kupitia wawakilishi wetu? Mfumo wetu ni mbovu sana.
Tuanze kwa kuikataa CCM maana wao ndio chanzo cha kuendelea na matatizo haya tuliyonayo watanzania. Mimi tangu mwaka 2000 nilipopata uelewa mzuri niliikataa CCM.