Ni katika eneo gani tumefanya vizuri sana kama nchi?

Kwakweli tunafanikiwa kwa speed nzuri kabisa kurudi kule kabla ya Wakoloni kuja.
 
Amani na utulivu ni tunu kubwa sana kwetu ni vile tumeshindwa kuzitumia kutuletea maendeleo yaliyotukuka.

Tungekuwa smart,wenye uchungu na nchi yetu kwa rasilimali tunazomiliki ilitakiwa tuwe ktk top 10 ya nchi zenye maendeleo sana Africa.
 
Umbea
 

Kwenye UCHAWA tupo the best , tumefanya vizuri sana
 
Kwenye sekta ya dini. Kila baada mitaa miwili lazima ukute kanisa. Lakini kwingine kote ni uozo mtupu
 
Tumefanya vizuri sana sana kwenye kumsifu mama Samia.
 
Kwenye sekta ya dini. Kila baada mitaa miwili lazima ukute kanisa. Lakini kwingine kote ni uozo mtupu
Kuwepo kwa Utitiri mkubwa wa nyumba za ibada ni dalili na Uthibitisho mojawapo kwamba kwenye hiyo nchi kuna janga kubwa sana la kushindwa na kuanguka kabisa kwa mifumo yote ya kiutawala wa nchi (the total failure of all the Government Machinery), pamoja na kushindwa na kuanguka kabisa kwa mfumo wa Elimu katika nchi husika. Watu baada ya kushindwa kupanga na/au kuendesha maisha yao kwa kutumia akili na Elimu zao vizuri badala yake sasa wanategemea bahati nasibu, 'kudra za Mungu' na Miujiza.
 
Tumefanikiwa kuingiza siasa hata kwenye mambo ya kitaalaamu
 
Ni kweli mkuu hata ukifanya tafiti maeneo yenye wakaaji wengi walioshiba itikadi ya dini ndio yenye kiwango kikubwa cha ujinga na umasikini, unakuta waamuni wamefanya harambee ya kujenga kanisa mpaka wamefanikiwa halafu siku ya ibada wanaenda hapo kanisani kumuomba Mungu awawezeshe watoto wao kupata ajira wakati izo pesa walizotumia kujenga kanisa wangeanzisha kiwanda au mradi wa uzalishaji zingepatikana ajira nyingi tu.
 
Hivi kweli rais au mpambe wake anaona haya majibu? Majibu yanafikirisha sana. Wote waliopo jamii forum wana sifa ya kuwa wabunge na ndiyo safari ya kufika cheo cha uwaziri na vyeo vinginevyo serikalini.

Kwa muktadha huo, nachukulia haya ni maoni ya wasomi.

Kwa maana hiyo wanasikitishwa na spidi au mipango yetu katika maendeleo.
 
China wanatafuta ukubwa, kupitia manufacturing industries, wanahakikisha wanaweza kutngeneza chochote duniani,
India kwenye technologies nk,
America, ulaya, military and technology industries, Afrika haijulikani tunatafuta ukubwa katika nini! Labda, kukata mauno insta, kuteua na kupangua, na ziara za hovyo!unasikia eti waziri Afika eneo lenye mafuriko, unakuta wnaenda maofisa kibao wa wizarani wamevaa suti wanaenda kuona mafuriko yalivyotokea! Sio, mafundi, wala ma engineer, eneo lenye maafa wanaenda kufanya nini?
 
Nikusahihishe kidogo mkuu. Ethiopia si nchi ya Kiarabu, ni kama sisi Tanzania tuko kundi moja hata kama shirika lake la ndege lina fanya vizuri.
 
Nikusahihishe kidogo mkuu. Ethiopia si nchi ya Kiarabu, ni kama sisi Tanzania tuko kundi moja hata kama shirika lake la ndege lina fanya vizuri.
Najua mkuu. Hata Botswana siyo nchi ya waarabu. Tanzania tumefanya vizuri wapi?
 
Tatizo hata hao wenye mawazo ya kujenga wakilambishwa asali wanabadilika case study nzuri ni Hamphrey Polepole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…