Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukaapa hutakaa uifanye tena?

Arusha Mererani kwenye machimbo ya Tanzanite.
Wanaume tunapambana sana wakuu.
Uko chini ya ardhi mita mia, , kanjia kenyewe kadogo.
Mara mabomba ya Oksijeni yazime, unaisikia Baruti inafumua huko huko chini mlipo.
Mimi kule sitarudi tena.
Mita mia cha mtoto. Machimbo ya dhahabu mnaenda hata zaidi ya hizo mita
 
Mm nilishtuka baada ya kuona wenzangu wanatoka na mabeseni nkawachana live hii kazi sifanyi nikasepa zangu.

Wakati wa usaili wanakuambia utoe buku mbili kwa ajili ya usaili, Mm nikasema sikujua hilo mana wakati wa maelezo yao sikuambiwa hilo.
Bila.shaka ilikuwa ni magomeni mapipa. Hata Mimi nadhani mwaka 2016, nilijichanganya nikaangukia Kwa Hao Jamaa. Nilikimbia hapohapo ofisini kwao baada ya kugundua KAZI yenyewe ni Kutembeza Vyombo mtaani
.
 
Hivi mtoa mada ushawahi saidia fundi labda???
 
Kazi ya kwenye kiwanda cha nondo idara ya kupokea uji wa moto uliotokana na screpa na kwenda kuweka kwenye mifereji kwa ajili ya hatua za utengenezaji nondo.
Akitegea mtu au akijikwaa mmoja uji ukamwagika kama sio kifo basi kilema cha maisha.
Hii kazi niliifanya siku moja tu na nilimuomba Mungu nimalize salama, sina hamu nayo.
 
Mi nilifanya kazi Kiwanda Cha Mbolea ya chumvi. Picha Linaanza Unabeba Viroba Vya Kilogram 25 Vitatu Unapeleka Juu Kama ghorofa.

Ebwana eeeh! Ile Kazi Nililudi Nyumbani Ata Kunyenyua Kopo La Kuogea Nilishindwa, Toka Hapo Sikurudi Tena. Ile Kazi Kiboko Kwanza Inachubua Mwili Pia Ni Nzito .

Nyie Haya Maisha Kunawatu Wanateseka .
 
Una bahati hukupata short!,Kazi ya kuwa supervisor!Hasa kusimamia watu waliokuzidi umri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ