Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukaapa hutakaa uifanye tena?

Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukaapa hutakaa uifanye tena?

Nikiwa chuo mwaka wa tatu nilipata nafasi ya kwenda kwenye interview Marketing agency flani hapa Dar. Walikuwa wanataka Social Media Manager unfortunately nikakosa ile nafasi. Wiki iliyofuata boss akaniita na kuniambia nimekosa ile nafasi lakini kuna nafasi ya Sales. Nikasema sawa nitaifanya.

Kazi ya sales ni unazunguka kutafuta wateja wa kufanya nao kazi. Mwanzo niliona ni rahisi ila kiukweli niliteseka kuzunguka na hili jua la Dar na nilkuwa natumia gharama nyingi kuliko hata mshahara ninaopokea nilifanya miezi miwili nikaacha kwasababu ilikuwa ni mateso tu.

Sijui mtu anilipe mshahara wa shing ngapi ndo nipate moyo wa kufanya kazi ya sales tena
Alafu waajiti bwana wahuni sana sasa mtu wa sales humpi hela ya vocha hela ya kuzunguka hao wateja atawafikiaje ili sales ziongezeke?
 
Hivi mtoa mada ushawahi saidia fundi labda???
Saidia fundi ni kazi nayo ya kusema ngumu?. Hujafanya kazi ngumu basi.
Kazi ya kwenye kiwanda cha nondo idara ya kupokea uji wa moto uliotokana na screpa na kwenda kuweka kwenye mifereji kwa ajili ya hatua za utengenezaji nondo.
Akitegea mtu au akijikwaa mmoja uji ukamwagika kama sio kifo basi kilema cha maisha.
Hii kazi niliifanya siku moja tu na nilimuomba Mungu nimalize salama, sina hamu nayo.
Binafsi hii kazi niliitoroka na hela yangu niliwaachia sikutaka hata kuidai Ile sio kazi ya kufanya kwa mtu mwenye utimamu wa akili.
 
Katika idara ambazo watu hutakiwa kulipwa vizuri ni idara ya sales. Imagine mtu anapambana kuiingizia kampuni mamillion ya fedha ili shughuli zote ziende kwa ufasaha halafu mtu huyo wanamlipa laki na nusu mpaka laki 3!

Sehemu pekee ambapo watu wa Sales and Marketing wanalipwa vyema ni kwenye baadhi ya makampuni ya benki,teknolojia ya mawasiliano na kampuni za bia na sigara tu. Kampuni nyingi ni wababaishaji yani sales person anakuwa kama punda tu.
 
Binafsi hii kazi niliitoroka na hela yangu niliwaachia sikutaka hata kuidai Ile sio kazi ya kufanya kwa mtu mwenye utimamu wa akakili.
Hapo kwenye "Utimamu wa akili" umenichekesha sana mkuu.
Nilikuwa sijawahi kuona chuma kinakuwa uji ndio nilishuhudia siku hiyo, ule mvuke wake kipindi kinu kinamwaga uji kwenye mtungi ili mbebe ni balaa.
 
Katika kipindi fulani nimefulia niko nauhitaji wa pesa sana,kuna mtu akawa anatafuta mtu wa kumpa mafunzo mbwa wake wa kizungu.,American bulldog aliyekuwa cross kidogo,umri ni alikuwa kafika miezi mi 5 hivi likubwa lishakuwa. Nikamwambia usijali boss hata mimi naweza kufundisha mbwa.

Boss akakubali nikamuomba siku mbili hivi nijiandae- huo muda nikawa nautumia kuangalia video youtube mbali mbali za wafundisha mbwa,hatua kwa hatua nikajua huyu mbwa atakuwa kama wa polisi! Vitu vya kuanza navyo nikanunua fresh- siku ya kwanza nikafika,mbwa anatisha sema najikaza! Anabweka ananifuata nataka kukimbia sema napiga moyo konde,kulikuwa na dada mwenyeji naye anamuogopa balaa,mzee mwenye mbwa kaniacha hapo nipambane.
Siku ya kwanza ikaenda fresh,sababu sikutumia muda sana. Siku imefuata yule mbwa nikamfunga sehemu moja baada ya kuona ananisumbua kukimbia kimbia na hatuelewani kwa chochote,yule mbwa alikuwa mkali balaa! Alikuwa ananisubiri nimsogelee tu animalize! Kuona hivyo nikawasha zangu pikipiki kimya kimya nikasepa-sikuwahi kurudi na wala sikutaka tena kuskia hiyo kazi
 
Katika idara ambazo watu hutakiwa kulipwa vizuri ni idara ya sales. Imagine mtu anapambana kuiingizia kampuni mamillion ya fedha ili shughuli zote ziende kwa ufasaha halafu mtu huyo wanamlipa laki na nusu mpaka laki 3!

Sehemu pekee ambapo watu wa Sales and Marketing wanalipwa vyema ni kwenye baadhi ya makampuni ya benki,teknolojia ya mawasiliano na kampuni za bia na sigara tu. Kampuni nyingi ni wababaishaji yani sales person anakuwa kama punda tu.
Oya ukweli mchungu makampuni ambayo sale anapiga hela ni TCC/TBL.
 
Back
Top Bottom