Ni kazi gani uliwahi kuifanya ukaapa hutakaa uifanye tena?

Alafu waajiti bwana wahuni sana sasa mtu wa sales humpi hela ya vocha hela ya kuzunguka hao wateja atawafikiaje ili sales ziongezeke?
 
Hivi mtoa mada ushawahi saidia fundi labda???
Saidia fundi ni kazi nayo ya kusema ngumu?. Hujafanya kazi ngumu basi.
Binafsi hii kazi niliitoroka na hela yangu niliwaachia sikutaka hata kuidai Ile sio kazi ya kufanya kwa mtu mwenye utimamu wa akili.
 
Katika idara ambazo watu hutakiwa kulipwa vizuri ni idara ya sales. Imagine mtu anapambana kuiingizia kampuni mamillion ya fedha ili shughuli zote ziende kwa ufasaha halafu mtu huyo wanamlipa laki na nusu mpaka laki 3!

Sehemu pekee ambapo watu wa Sales and Marketing wanalipwa vyema ni kwenye baadhi ya makampuni ya benki,teknolojia ya mawasiliano na kampuni za bia na sigara tu. Kampuni nyingi ni wababaishaji yani sales person anakuwa kama punda tu.
 
Binafsi hii kazi niliitoroka na hela yangu niliwaachia sikutaka hata kuidai Ile sio kazi ya kufanya kwa mtu mwenye utimamu wa akakili.
Hapo kwenye "Utimamu wa akili" umenichekesha sana mkuu.
Nilikuwa sijawahi kuona chuma kinakuwa uji ndio nilishuhudia siku hiyo, ule mvuke wake kipindi kinu kinamwaga uji kwenye mtungi ili mbebe ni balaa.
 
Katika kipindi fulani nimefulia niko nauhitaji wa pesa sana,kuna mtu akawa anatafuta mtu wa kumpa mafunzo mbwa wake wa kizungu.,American bulldog aliyekuwa cross kidogo,umri ni alikuwa kafika miezi mi 5 hivi likubwa lishakuwa. Nikamwambia usijali boss hata mimi naweza kufundisha mbwa.

Boss akakubali nikamuomba siku mbili hivi nijiandae- huo muda nikawa nautumia kuangalia video youtube mbali mbali za wafundisha mbwa,hatua kwa hatua nikajua huyu mbwa atakuwa kama wa polisi! Vitu vya kuanza navyo nikanunua fresh- siku ya kwanza nikafika,mbwa anatisha sema najikaza! Anabweka ananifuata nataka kukimbia sema napiga moyo konde,kulikuwa na dada mwenyeji naye anamuogopa balaa,mzee mwenye mbwa kaniacha hapo nipambane.
Siku ya kwanza ikaenda fresh,sababu sikutumia muda sana. Siku imefuata yule mbwa nikamfunga sehemu moja baada ya kuona ananisumbua kukimbia kimbia na hatuelewani kwa chochote,yule mbwa alikuwa mkali balaa! Alikuwa ananisubiri nimsogelee tu animalize! Kuona hivyo nikawasha zangu pikipiki kimya kimya nikasepa-sikuwahi kurudi na wala sikutaka tena kuskia hiyo kazi
 
Oya ukweli mchungu makampuni ambayo sale anapiga hela ni TCC/TBL.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…