Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

David Harvey

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2014
Posts
2,894
Reaction score
6,020
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito, nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni, nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
 
Pole sana
 
Mkuu mkuu usikufuru kama hauoni umuhimu wa mzazi potezea na sio kuanza kumuombea kifo kisa mtu uliyekutana nae ukubwani. Mzazi ana umuhimu wake na mke,mume ana umuhimu wake pia. Jambo usilolijua au kulifahamu asilimia kubwa ya wanawake wapo tayari kumpoteza Mume na sio mtoto au mzazi wazazi wake.

Pole kwa msiba
 
Pole sana Mkuu, kama una nafasi ya kubadilisha mazingira fanya hivyo nyumba kodisha. Inaweza kukusaidia kuanza upya sasa hivi ni ngumu sababu nyumba ni ile ile, ndugu ni wale wale na wapo pale pale, marafiki ni wale wale. So kila utachofanya taswira ya mwenzio lazima ije, badili mazingira ukiweza!!

NB: Wanao ndiyo wanaona umuhimu wa mzazi ila wewe unaona umuhimu wa mke. Huoni umuhimu wa wazazi sababu ulishajitegemea
 
Make unaweza kuoa mwingine,Mama utampata wapi?
 
Jikaze Mkuu inauma mazoea yanaletaga shida ila jikaze kiume hukuzaliwa nae huyo kumbuka wanao ndiyo ndugu zako wa damu kabisa ana kwao huyo, Ile kauli ya mkae mwili mmoja ni scam!
 
Pole kwa majonzi Kiongozi.

Mke/Mume mkitofautiana mnaweza kuachana na ukapata mwingine.

Vipi unaweza kupata mbadala wa Mama/Baba Mzazi akifariki?

Kuna wenzio tunatembea na maumivu ya kuwapoteza wote kwa pamoja au mmoja wao na hadi sasa tumekosa mbadala wao 😭
 
Mchumba wangu alipata miscarriage, aliumia sana. Ajabu akaniambia ni bora angenipoteza mimi! I was perplexed! Since then I learned mke siyo ndugu yako. They're too selfish.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…