Ni kiasi gani ambacho MTU ukiwa na uhakika wa kuingiza kwa siku unaweza kuhesabika kama wewe ni Tajiri?

Ni kiasi gani ambacho MTU ukiwa na uhakika wa kuingiza kwa siku unaweza kuhesabika kama wewe ni Tajiri?

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
HABARI WAKUU, Nimekuwa nikijiuliza hili swali Mara nyingi sana na majibu nilliyokuja kuyapata hakika MTU anaeitwa Tajiri wanapesa nyingi sana, nimegundua hili zaman katika harakati za kutafta tonge ilikuwa hata kuingiza buku3 kwa siku ilikuwa mbinde sana

Yaani nilikuwa nikikaa naamini kabisa nikipata mchongo ambao walau kwa siku naweza Ku make buku 10 kwa siku nitakuwa nimetoboa, harakat zikaendelea mungu ikafikia hatua nikawa naingiza hata 20 elfu kwa siku ila cha ajabu maisha yakabaki vilevile hakuna lililobadilika maisha yakawa yaleyale tu.

Hapa nikawa nawaza walau ikitokea nikawa na uwezo wa kuingiza 30 kwa siku ndio nitakuwa nishatoboa, harakati zikaendelea kweli mungu si Mshana nikajikuta hiyo pesa inaingia kwa siku tena mda mwingine kwa masaa machache tu ila cha kushangaza maisha yakabaki vilevile yaani hakuna kilichokuja kuwa na unafuu bado nilikuwa najiona wa kiwango cha chini zaidi.

Bado hata pesa ya kulipa kodi ilikuwa inapatikana kwa shida vilevile, bado nikaona walau nikiingiza hata 50 elfu kwa siku hapo sasa nitakuwa ni viwango vingine kabisa kweli bana harakati zimeendelea kusema kweli hadi sasa kwa siku uhakika wa kuingiza 70 elfu hadi 10k na zaidi kwa siku inaingia tena bila kutumia nguvu

Ila ninachoshangaa bado mambo ni tia maji tia maji yaani Mimi sio lolote sio chochote pamoja kuwa naingiza 100k kwa siku ila cha ajabu hata mtaani sionekani wa maana Niko vilevile yaani naonekana bado nipo kwenye kundi la Wagonga ulimbo AKA tia maji tia maji.

Sina heshima sawa na kama nilivyokuwa nikidhania kuwa nikiwa na uhakika wa kuingiza 100K kwa siku nitakuwa na mwonekano kama wao yaani bado wako vilevile, na kwa maisha budget yangu kwa Siku kiwango cha matumizi 30000 hadi 50000 kwa siku na hapo ni Siku ambazo sina galama za ziada kama kuchakata mbususu za michepuko etc, lakini bado sipati heshima wala kuwafikia wale watu ambao mwanzo nilidhani nitawafikia nikiwa na income kiwango flan perday!

Hapa kwa ambae pengine hajafikia kiwango kiwango hicho perday income atajua nazingua ila wadau ambao wanaingiza hiko hili wanalitambua vizuri,

My take ni kwamba vijana tutafte pesa ili tuishi ila utajiri ni mgum sana tena sana!
 
Tajiri ni nani?

Tajiri ni mtu yeyote mwenye uhakika na kesho na kesho kutwa yake.

Tajiri ni mtu yeyote mwenye uhakika na mahitaji yote muhimu ya maishani mwake kuanzia malazi na kila kitu mpk luzuries zake, na bado Chenchi ya kesho ipo pale pale.

Tajiri sio kipato,tajiri sio kiasi cha income Utajiri ni kuweza kupambana na kitu watu wanaita Maisha na ukayatandika Maisha yani una score 5 - 0,

Ila wewe kama daily maisha yanakupga 7-0 watch out,unaweza ingiza 1m per day na usiwe tajiri.
 
Laki yoyote ila uwe na nyumba, gari na biashara kubwa
 
Inaonekana status yako ya maisha inapanda kadri kipato chako kinavyopanda. Ndio maana unakuwa unaendelea kustruggle kwa sababu pesa unayoingiza si kubwa ukilinganisha na maisha yako.

Jifunze kuishi status ya chini ya kipato chako na utapata pesa ya ziada kwa ajili ya akiba na investments.

Nilivyokuwa na miaka 19 nilipiga dili flani nikapata 4 mil mgao wangu net profit. Nikaanza yale ya maneno ya mtaani nikanunua bodaboda ila sikujiinua status kwa kuwa niliona bado pesa ni kidogo. Nilipata hasara ile boda ila kazi zikaendelea kuingia nilikuwa sikosi mil 2 at least kwenye akaunti

Miaka 21 nikaanza kuingiza pesa nyingi takribani 4 kila mwezi. Ghafla nikajikuta nina zaidi ya 25 mil kwenye akaunti sina cha kufanyia. Bata zikaanza. Nilisafiri na kula kama mil 20. Bahati nzuri biashara ilikuwa inaendelea kuingiza so 20 mil nikaendelea kuwa sikosi kwenye akaunti japokuwa by 23 mwishoni nilikuwa nishaingiza zaidi ya mil 100 ambazo nyingi zilikuwa zimepotea juu kwa juu.

Jambo hilo limenifunza. Nikatafuta sehemu nzuri ya kuishi ambayo nikajua sitahama muda wowote soon na kuendelea na kazi. Lifestyle yangu sikuibadilisha zaidi pia.

Nilipoanza kuingiza pesa nyingi zaidi (100 mil plus) nikawa sikimbizani na maisha ya anasa na nikabaki humble. Nashukuru Mungu nimeweza kufanya mazuri sana kwa pesa hizo badala ya kuila na bado akiba na investment nilizoweka ziko vizuri. Mpango ni kuendelea kuishi simple mpaka 35 na hata ikibidi 40 ili niwe na muda wa kutosha kujenga biashara nzuri zitazoingiza kipato cha kizazi hadi kizazi.
 
Maana ya karibu sana ya neno "tajiri" kwa Kingereza ni "trader", mfanya biashara mwenye kuajiri.

Ukifikia kiwango cha kukuingizia pesa huku ukiwa umelala au umeenda mapumziko na pesa hazikati kuingia na kutoka basi elewa kuwa wewe ni mfanya biashara mwenye mafanikio aka tajiri.
 
Ukiweza afford the following

1. To feed your family
2. Bima ya afya na elimu kwa watoto
3. Makazi kwa familia yako (nyumba au uhakika wa kulipa kodi)

Hapo ni tajiri ndugu yangu.
 
Ongeza kipato kisha punguza anasa!! Wakati unapata kipato cha 20k per day ,matumizi yako kwa siku yalikuwaje?
 
Ukiweza afford the following

1. To feed your family
2. Bima ya afya na elimu kwa watoto
3. Makazi kwa familia yako (nyumba au uhakika wa kulipa kodi)

Hapo ni tajiri ndugu yangu.
hivi ninavyo mkuu ila bado naona naishi tia maj maji
 
Inaonekana status yako ya maisha inapanda kadri kipato chako kinavyopanda. Ndio maana unakuwa unaendelea kustruggle kwa sababu pesa unayoingiza si kubwa ukilinganisha na maisha yako.

Jifunze kuishi status ya chini ya kipato chako na utapata pesa ya ziada kwa ajili ya akiba na investments.

Nilivyokuwa na miaka 19 nilipiga dili flani nikapata 4 mil mgao wangu net profit. Nikaanza yale ya maneno ya mtaani nikanunua bodaboda ila sikujiinua status kwa kuwa niliona bado pesa ni kidogo. Nilipata hasara ile boda ila kazi zikaendelea kuingia nilikuwa sikosi mil 2 at least kwenye akaunti

Miaka 21 nikaanza kuingiza pesa nyingi takribani 4 kila mwezi. Ghafla nikajikuta nina zaidi ya 25 mil kwenye akaunti sina cha kufanyia. Bata zikaanza. Nilisafiri na kula kama mil 20. Bahati nzuri biashara ilikuwa inaendelea kuingiza so 20 mil nikaendelea kuwa sikosi kwenye akaunti japokuwa by 23 mwishoni nilikuwa nishaingiza zaidi ya mil 100 ambazo nyingi zilikuwa zimepotea juu kwa juu.

Jambo hilo limenifunza. Nikatafuta sehemu nzuri ya kuishi ambayo nikajua sitahama muda wowote soon na kuendelea na kazi. Lifestyle yangu sikuibadilisha zaidi pia.

Nilipoanza kuingiza pesa nyingi zaidi (100 mil plus) nikawa sikimbizani na maisha ya anasa na nikabaki humble. Nashukuru Mungu nimeweza kufanya mazuri sana kwa pesa hizo badala ya kuila na bado akiba na investment nilizoweka ziko vizuri. Mpango ni kuendelea kuishi simple mpaka 35 na hata ikibidi 40 ili niwe na muda wa kutosha kujenga biashara nzuri zitazoingiza kipato cha kizazi hadi kizazi.
Kumbe humu JF tuna watu wenye maisha haya ya kuingiza 100M+ per month? Nilidhani haya mambo ni nadharia na stories za kusadikika ama fantasies. Hongera sana Mkuu. Siku moja uki-share ulivyoanza na kufikia level hii kibishara hatua kwa hatu utakuwa umetusaidia sana sisi wapambanaji huku chini.
 
Umewekeza nini mkuu? tatizo siyo kupata pesa inawezekana ukapata pesa ukashindwa kuwekeza.
 
HABARI WAKUU, Nimekuwa nikijiuliza hili swali Mara nyingi sana na majibu nilliyokuja kuyapata hakika MTU anaeitwa Tajiri wanapesa nyingi sana, nimegundua hili zaman katika harakati za kutafta tonge ilikuwa hata kuingiza buku3 kwa siku ilikuwa mbinde sana yaani nilikuwa nikikaa naamini kabisa nikipata mchongo ambao walau kwa siku naweza Ku make buku 10 kwa siku nitakuwa nimetoboa, harakat zikaendelea mungu ikafikia hatua nikawa naingiza hata 20 elfu kwa siku ila cha ajabu maisha yakabaki vilevile hakuna lililobadilika maisha yakawa yaleyale tu.

Hapa nikawa nawaza walau ikitokea nikawa na uwezo wa kuingiza 30 kwa siku ndio nitakuwa nishatoboa, harakati zikaendelea kweli mungu si Mshana nikajikuta hiyo pesa inaingia kwa siku tena mda mwingine kwa masaa machache tu ila cha kushangaza maisha yakabaki vilevile yaani hakuna kilichokuja kuwa na unafuu bado nilikuwa najiona wa kiwango cha chini zaidi.

Bado hata pesa ya kulipa kodi ilikuwa inapatikana kwa shida vilevile, bado nikaona walau nikiingiza hata 50 elfu kwa siku hapo sasa nitakuwa ni viwango vingine kabisa kweli bana harakati zimeendelea kusema kweli hadi sasa kwa siku uhakika wa kuingiza 70 elfu hadi 10k na zaidi kwa siku inaingia tena bila kutumia nguvu ila ninachoshangaa bado mambo ni tia maji tia maji yaani Mimi sio lolote sio chochote pamoja kuwa naingiza 100k kwa siku ila cha ajabu hata mtaani sionekani wa maana Niko vilevile yaani naonekana bado nipo kwenye kundi la Wagonga ulimbo AKA tia maji tia maji.

Sina heshima sawa na kama nilivyokuwa nikidhania kuwa nikiwa na uhakika wa kuingiza 100K kwa siku nitakuwa na mwonekano kama wao yaani bado wako vilevile, na kwa maisha budget yangu kwa Siku kiwango cha matumizi 30000 hadi 50000 kwa siku na hapo ni Siku ambazo sina galama za ziada kama kuchakata mbususu za michepuko etc, lakini bado sipati heshima wala kuwafikia wale watu ambao mwanzo nilidhani nitawafikia nikiwa na income kiwango flan perday!

Hapa kwa ambae pengine hajafikia kiwango kiwango hicho perday income atajua nazingua ila wadau ambao wanaingiza hiko hili wanalitambua vizuri,

My take ni kwamba vijana tutafte pesa ili tuishi ila utajiri ni mgum sana tena sana!
Ukiweza kuingiza 1M kwa siku upo pazuri mno.
 
Back
Top Bottom