Uchaguzi 2020 Ni kichwa ngumu na uzalendo tu kwa CCM: Tundu Lissu anatikisa, smart na anapendwa

Na ile mi V8 ya kijani aiache wapi?😂😂
Lissu kala points 3 muhimu kwa kupanda mtumbwi
 
azory je? vip kuhusu ben saanane? na je vip kuhusu wafanyabiashara wakubwa, wanamuziki waliotekwa? vip kuhusu maiti kwenye viroba fukweni? watu walionyang'anywa fedha zao je? maduka ya fedha za kigeni?!!! wakulima waliofilisiwa wakiwemo wa korosho?!!! vitambulisho vya uongo vya wamachinga je? wastaafu wanaosota mitaani bila kulipwa mafao yao je? na je viongozi wa waislam wanaosoteshwa mahabusu miaka nenda miaka rudi? na vip kuhusu walioondolewa kwa vyeti feki kinyume na sheria? unatuambiaje kuhusu watumishi wa umma waliosoteshwa miaka miatano bila kupandishiwa mishahara kinyume na sheria? na vip hao viongoz wa dini waliotuhumiwa kidhuluma kuwa si watanzania kisa tu wamekosoa kisheria? na vip kuhusu kuvunjavunja sheria na taratibu za nchi hovyo hovyo ikiwemo kuwafungia wapinzani wasifanya kazi zao za siasa ilhali wapo kisheria, kuwanyima elimu watoto wa kike waliopata mimba nk nk.....naam yan almradi list ya uovu wa jiwe kwa watanzania ni ndefu sana
 
Vibaya mno, jana nilikuwa nansio hapa ukerewe wanawake na wanaume ni Lissu tu
Unajua kuna vitu jamaa wanavyovifanya vinampa credits nyingi sana Lissu na yeye kwa kulitambua hilo anatumia udhaifu huo huo kula points nyingi zaidi kutoka kwa wananchi.

Sikuona mantiki yoyote ya kumzuia ile siku pale mlandizi, sijaona mantiki , yoyote ya kusingizia kivuko kibovu ziwa Victoria.
Vichwa vinawauma sasa, ngome iliyotegemewa Lissu kaivunja na kaondoka na baraka zote za wanakanda ya maziwa makuu.
 
Kuna dalili zinaonyesha Mahera kawageuka CCM kama ni kweli basi atakuwa kausoma upepo na kaona akiweka Nongwa Mahakama ya The Hague inamuita
mwache ccm wamwingize kwenye msala wa kuchafua uchaguzi aone atakavyoachwa mwenyewe huko the hegi. atatagetiwa yeye kama yeye na si tume vinginevyo awe amejitoa sadaka yeye na familia yake.
 
Mimi huwa nawapenda watu wakweli!! nimefurahi leo umesema ukweli!! sasa badala kuiba kura sibora mkawa wakweli muache wananchi waamue?
Mtoa mada yeye ni CCM na amekiri kwamba wamezidiwa sana na hoja za mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA lakini pia amesema anaamini watashinda kwa njia za kisiasa kabisa zilizoboreshwa. Kazi ipo hapo.
 
tena nashauri siku ya lisu kuingia kufanya kampeni Dar apande mwanapunda ili andiko litimie.
🎶🎶🎙🎙🎧🎤🎤🎸silaha begani hakuna kurudi nyuma Makamanda🎼🎼🎵
🚣‍♂️🚣‍♂️🚣‍♂️🚣‍♂️🚣‍♂️
 
Kuna dalili zinaonyesha Mahera kawageuka CCM kama ni kweli basi atakuwa kausoma upepo na kaona akiweka Nongwa Mahakama ya The Hague inamuita
Nawaonea huruma sana mabosi wote wa vyombo vya Serikali vinavyohusika na mambo ya uchaguzi huu, wamewekwa njia panda .
 
Option ni mbili tu kurudi Chattotown au kwenda the Hague, Huwezi shindana mshindi
 
Yani huyo kiduku lissu apambane anavyojua lakini urais hapati ng'ooo
 
Isipokuwa wanufaikaji wa mfumo wa chama dola,vinginevyo wapenda Haki wote bila kujali vyama vyo wanaenda kumpigia kura Mh.Lissu na watazilinda usiku na mchana zisiibwe.CCM matumbo moto!
Uchaguzi huu,hatudanganyiki kwa Propaganda ya Mabeberu.Tunataka Uhuru,Haki kwa Maendeleo ya wote!Simple.
 
The person is talented; Lissu 2020 hili halina ubishi.

Hili litakiwa funzo kwa viongozi vichwa ngumu
 
Point za Lisu huwezi kuziona unajifanya Mbuni Sababu unajua utarudi kwenu kulima
 
Lissu namkubali sana tena sana lakini ugumu unakuja kwenye kuzuia bao la mkono tu. Je watanzania watakuwa tayari kumuunga mkono kwenye harakati za kulizuia? Mana naona kama itakuwa kama ile ya Mange
Piga Kura linda Kura
 
Fanya uamuzi sahihi,kuwa sehemu ya mabadiliko na kufanya hivyo utakuwa na amani ya kweli ndani ya moyo wako .
 
System imeshapiga tick
NAWAZA Ile mfano wa karatasi ya KUPIGIA KURA SEHEMU ya lissu tayar Ina VEMA SASA KARATAS ZIKIZOBAKIA JE AU ZOTE ZINA VEMA..MTU AKIWEKA VEMA YA PILI SI KURA IMEHARIBIKA?? AU Pythagoras una maanisha KITENGO WAMEMPITISHA LISSU?
 
Mwaka huu sikutegemea kama mnahitajim kupiga kampeni ....lakini mambo yamebadilika ...yaani wananchi wanahasira sana naona....umeona nyomi la kanda ya ziwa bila mabango wala wasanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…