Vigogo wako juu ya serikali awamu hii, wanatamba na kufanya wapendavyo. Na hakuna wa kufanya fyoko.
Hakuna kigogo yeyote wa serikali, hata waliotajwa na CAG kuwa wamefuja mali za umma ambaye ameburuzwa mahakamani hadi leo.
Mama anabakia kusema tu "stupid" lkn hayagusi haya majitu mazito kuliko serikali.
MaDC, maDED, maRC, maRAS, na maRPC wanainamisha vichwa chini wakipishana na gari za wakubwa zikiwa zinafanya yao. Acha kabisa.
Juzi hapa kuna uongozi wa wilaya moja hapa nchini, uliwaita wenyeviti wa serikali za mitaani na watendaji kata na kuwaamuru wayakusanye madubu yote yanayoendeshwa kinyume na utaratibu ktk maeneo yao.
Viongozi hao wa chini kabisa wa serikali wakageuka mbogo na kuanza kung'aka. Wakasema "hamjui madubu haya yanamilikiwa na nani kwa sehemu kubwa nchi hii? Ninyi mnaishi mbinguni kwamba hamuyaoni? Mbona hamuyakamati? Mnataka kutuangushia zigo sisi? Mkutano ukaishia hapo na maagizo yakaishia hapo.
Kama kwenu aliyetoboa ni mwendesha bodaboda kuwa mpole tu . Waache mafisadi watambe awamu hii.