Ni kipi kianze kati ya Katiba Mpya au Kuitoa CCM Madarakani?

Kwa akili za baadhi ya watu unaona kabisa ilivyo ngumu hawa jamaa kutoka madarakani, nchi yenye watu zaidi ya 60 ml bado wanauliza wakitoka akae nani? sijui tulipigwa na nini mpaka tunaona bora kuyazoea matatizo, kumtetea mtanzania ni ngumu mno bora kuwaacha tuu hivyo walivyo.
 
Ccm iondolewe tu kwani hiki chama kimenitoka sana moyoni baada utapeli wa kutoza mafao yangu
 
Je Deep State wetu ni Wazaledo halisi au wapigaji?
Je nani wa kuivunja ndoa ya TISS?
Je Chama kipi kwa sasa kina viongozi wengi Wazaledo, makini, weledi wenye kuichukia rushwa kwa dhati, wenye kuwahurumia wananchi wake hasa walio wengi wanyonge na wa kipato cha kati?
Kama kipo chama hicho sawa au Kizaliwe Chama Kipya kwa hivi sasa tofauti na hivi vilivyopo sasa vyenye mapandikizi kila mahali.
 
Mm ni mwanaccm ninayekukatalia hoja yako waulize waokuwa ktk sensa ndo utayagundua yaliyojificha.
Hata hili la kuzuia mikutano tunaona ni mtaji kwetu lakini ndo mwisho wa akili ya viongozi tulionao.
Labda tuombe Lisu asirudi kwani sioni wa kumzuia kuichukua nchi na kuitawala.
Kwa ujumla tumechokwa kwa kuongoza kijinga na kuwaona watanzania ni wajinga kumbe sisi tunaowaongoza ndo wajinga kwani tumeshindwa kuwaonfolea matatizo yanayowazunguka hapa tunawakosea sana Watanzania
 
Umesema haihitaji kuingia barabarani na kuhatarisha usalama hapo CCM itaendelea kubaki madarakani bila nguvu ya kuingia barabarani...tutakua tunajidanganya tu

Uko sahihi kabisa, nimekuwa nasisitiza kila siku, bila machafuko CCM haiwezi kutoka madarakani. Hatua ya kwanza ya kususia kupiga kura imeanza kufanikiwa, hatua ya machafuko ndio inayopaswa kufuatwa.
 

Wanaosema CCM ikitoka nani akae, ni hao hao CCM katika mazingira ya kujilinda bila kutumia nguvu. Wanajua kabisa watu wamewachoka, hivyo wanapumbaza watu kuwa hata wao wako tayari kutoka, ila hawaoni mwenye uwezo zaidi yao.
 
Mimi sina shida na CCM kuwatoa madarakani je chama kitaingia ambacho kina kwaajili ya kusimamia maslahi ya wananchi, kina demokrasia nzuri, chenye viongozi wenye vision na pia chenye viongozi wenye maadili

Enzi KANU hapo Kenya inatawala kama CCM, lugha zilikuwa hizi hizi kuwa hakuna chama kinaweza kuongoza Kenya. Leo hii KANU ni maiti hai, na kila uchaguzi Kenya kuna chama kingine. Lakini bado Kenya ina uchumi mzuri kuliko sisi makondoo wa Tanzania.
 

Mafanikio katika jambo lolote ni matokeo ya utekelezaji wa mikakati iliyoratibiwa sawa sawa kwa ajili ya kufanikisha jambo.

Hapa tulipo ni muhimu kutenganisha CCM, utawala na katiba mpya.

Elimu? Ambao hawahitaji katiba mpya hawahitaji elimu hao hawataki. Hakuna haja ya kupoteza muda nao.
 
Katiba mpya itangulie,ili tuwe na Tume Huru,matokeo ya uchaguzi yataamua nani anaongoza nchi!
Ccm imechakaa
 
Hivi hii nchi yetu ya Tanzania ina wazee kweli wastaafu walio litumikia hili taifa, waliotumika kwenye ngazi za juu sana za uongozi, wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama, mawaziri wakuu, magavana nk?
Kama wapo ipi nafasi yao kwa Taifa na uongozi wa sasa na ujao kwa hivi sasa kwa maslahi makubwa na mapana ya taifa letu?
Kama wapo wanafurahia na kinachoendelea kwa Taifa letu?
Je hawaoni umhimu wa kuachana na katiba ya miaka 44 iliyopita na kuja na katiba ya rasimu ya Mzee Warioba, hawaoni umhimu wa kuwa na jeshi la Usalama wa taifa lenye maboresho na mabadiliko?
Hawaoni umhimu wa Usalama wa taifa wasiwe na ndoa na chama chochote?
 
Reactions: RNA
Vile CCM huwa wanajibu wakiulizwa ni kwa nini nchi hii ni masikini ndani ya utawala wao ndani ya miaka 60 tokea uhuru
Your browser is not able to display this video.
 
Mimi sina shida na CCM kuwatoa madarakani je chama kitaingia ambacho kina kwaajili ya kusimamia maslahi ya wananchi, kina demokrasia nzuri, chenye viongozi wenye vision na pia chenye viongozi wenye maadili.
hata tukibadili katiba ccm wakigoma kuifuata ?
 
Hakika
 
Katiba mpya hasa ile ya Rasimu ya WARIOBA ikipatikana yaani ccm itafia usingizini....
 
Ianze kwa kudai Tanganyika yenu ni bora zaidi ya vyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…