Ni kipi kianze kati ya Katiba Mpya au Kuitoa CCM Madarakani?

Tuwe wakweli hapa, hata ikichukua CDM, TLP au CUF kwa katiba hii kamwe hawawezi na hawatakuja kubadirisha kuoata katiba mpya why?.

Katiba hii ni nzuri nyie watanzania yaani ukiwa nje ya huwezi kujua uzuri wake na ndiyo maana wanaCCM wanaikodolea macho na kutoa machozi ya uzuni kwamba ibadilishwe kweli?.

Wakirudi huku wanasikilizia ile tunaita mwangwi wa wananchi!.
 
Mbona hata sisi tunakuona wewe unayeiponda Serikali na CCM kama chawa wa upinzani tu!!??
 

Unaitoa kwa kitu gani, maana ipo tangu Uhuru! Itoe basi ili sisi tupoge vigelegele!
 
CCM kuondoka madarakani inaondoka.. Tena kwa urahisi sana.. Kuiondoa CCM madarakani iwe ndio kipaumbele cha kwanza.. Katiba itafuata.. Tunashindwa kuiondoa CCM madarakani kwa sababu wengi wetu hatupigi kura.. Hii nchi sio ya kutawaliwa na Rais aliyeshinda kwa kura milioni sita.. Ukifuatilia idadi ya wapiga kura miaka yote, ni chini ya theluthi mbili.. Wapiga kura wengine wapo wapi..?? Siku itakapofika tuhamasishane kwa umoja wetu twende kwenye sanduku la kura tukaikatae CCM .. Inawezekana.. Mara zote wakati sisi tunasusia uchaguzi na kuwahamasisha wanachama wetu wasishiriki uchaguzi wenzetu huwa wanawahamasisha wanachama wao kupiga kura.. Na hakuna wanachama waaminifu kama wanachama wa CCM .. Tuhamasishane tukapige kura kuikataa CCM.. CCM kuondoka madarakani kwa sanduku la kura inawezekana..
 
Kuna zee moja la ccm linasema kwamba,ili kuitoa madarakani ccm kwanza wananchi waachane na Simba na Yanga hapo sasa ndo kwa mbaali sana inawezekana kuitoa ccm madarakani.
 
Katiba mpya kwanza halafu polepole CCM itajiondoa yenyewe.

Na lengo isiwe kuiondoa CCM napenda kiwe Chama cha Upinzani na Wabunge wake kiduchu.

Na sisi tusiwe kama Chiluba kufanya Siasa za visasi.

Hata tukipata serikali ya mseto sio mbaya.
Kama lengo ni kuitumikia Nchi yetu pendwa chuki za nini?
 
Pia tunahitaji "Tojan Horse" ili tuiondoe madarakani from within.
 
Ccm ni janga la kitaifa
 
H
Hakuna Mwananchi anayeielewa CCM kama huamini, itisha mkutano wa hadhara, usitumie magari kusomba Watu, usiwape bodaboda Petrol, Wala usihonge pesa Wala usitumie wasanii then tuone mkutano wa Nani utafanikiwa.
Huu ni ukweli wa wazi. NAKED Truth
 
Duh,

Hii ni mada kabambe. Mada nzito sana ambayo ni ngumu kuijengea hoja kama ulivyoonyesha hapa.

Ninakubaliana nawe; kama ipo njia ya kuiondoa madarakani CCM kabla ya kutengeneza katiba mpya, hilo ni jambo jema zaidi.
Nadhani wengi wetu tunakimbilia katiba mpya tukidhani kwa kufanya hivyo ndiko kutakako rahisisha kuiondoa CCM madarakani, kwa vile hawatakuwa wamehodhi mifumo yote inayosimamia uchaguzi wa kuwaondoa madarakani.

Kwa hiyo swali linalotakiwa kujibiwa na mada hii ni jinsi ya kuiondoa CCM madarakani. Jinsi ya kuwazuia CCM kutumia vyombo vya kitaifa kuendelea kuwabakisha madarakani.
 
chama mfu kitoke halafu tupate katiba mpya tuanze kurejesha mali za umma zilizoibiwa na hiki chama.
 
Unaijua vizuri tume ya uchaguzi mzee

Ova
 
Ni sawa na ungeuliza Katiba ndio inaleta mabadiliko, au mabadiliko ndio yanaleta Katiba?

Kwangu naona ile Rasimu ya Warioba ndio ingeleta mabadiliko, lakini ile Katiba pendekezwa ingeleta machafuko ambayo ndio yangeleta mabadiliko.

So, chaguo ni lao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…