Ni kitanda gani kizuri; mbao, chuma au sofa?

Ni kitanda gani kizuri; mbao, chuma au sofa?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Ni kitanda gani kizuri na sifa zake nikanunue

Hatimaye kama nilivyonuia kwamba mwezi wa tisa hautaisha bila kuwa na kitanda ni karibia mwaka Sasa mimi na mama mtoto wangu tunatupa godoro yetu chini asanteni

Wote mlionipa matumaini tokea siku ya kwanza nilipolalia mabox

MUNGU ASIFIWEEEE
 
Mbao haitokua na mpinzanii,
Chuma kikianza kulika kwenye maungio ni kelele tuu,
Sofa ndio kabisaa, kuchanika, kuchafuka, kufubaa, bado hujataja uimara na mbao za hovyo zilizofunikwa na kitambaa....

Kuwa makini na mbao za siku hizi wanazoita mbao ngumu, mbao inapewa jina mfano Mninga, mkongo n.k, akisema mbao ngumu tuu shtuka.
Hayo ni ma play wood, MBF ya kichina likiingia maji unaokota pumba chini.

NOTE : Epuka furniture iliyopigwa Rangi kabla hujaona mbao yenyewe, utapewa furniture ya Pine shtuka wewe.
 
Kitanda ya Mbao na iheshimiwe wakuu
1695588359885.jpg
1695588315104.jpg
 
Cha chuma ni kizuri ila sijawai kuvielewa mbele ya mbao.
Cha chuma ni gharama kiasi, kizito rahisi kuharibu sakafu na kizito kuhamisha. Usipokifunga vizuri ndiyo kilileta asili ya neno kwichii kwichii! Kama unakumbuka vitanda vya zamani vya chuma na springs. Vilikuwa na minesoneso Ila makelele ya kwichii kwichiii. Super Nova!😂😂😂
 
Cha chuma ni gharama kiasi,kizito rahisi kuharibu sakafu na kizito kuhamisha.Usipokifunga vizuri ndiyo kilileta asili ya neno kwichii kwichii!Kama unakumbuka vitanda vya zamani vya chuma na springs.Vilikuwa na minesoneso Ila makelele ya kwichii kwichiii.Super Nova!😂😂😂
Sidhani kama kitanda cha chuma ni ghali kuliko mbao mengineyo nakubaliana nawe
 
Kanunue cha mbao, kitanda cha mbao au bidhaa ya mbao inaweza kudumu hata miaka 40, sio lazima zile mbao za bei kubwa kama mninga au mkongo, zipo mbao unaweza kupata kitanda kizuri muundo mzuri na wa kisasa kunzia laki na nusu mpaka laki tatu kulingana na mkoa ulipo.
 
Back
Top Bottom